Tafuta

Vatican News
2020.04.02 Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican 2020.04.02 Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican  

Vatican yaongeza muda hadi Mei 3 katika hatua za kupambana na Covid-19

Kuanzia tarehe 13 Aprili iliyokuwa ya mwisho,wamepyaisha tena muda wa siku nyingine ishirini hivi za sheria katika harakati za kudhibiti maambukizi ya janga la corona.

Hatua zilizopitishwa na Vatican, sanjari na hatua za serikali ya Italia za kuepusha kuenea kwa janga la Virusi vya Corona itaendelea hadi Mei 3. Uongezwaji wa muda  huo umewasilishwa  tarehe 14 Aprili 2020 katika Chumba cha Vyombo vya Habari Vatican kama ilivyo kawaida ya fursa nyingine.

Kwa  nji hiyo shughuli za mamlaka ya Vatican zitaendelea, japokuwa kwa mahudhurio  ya watu wachache ili kupunguza kwa kiasi fulani  cha watu na kuhimiza kufanya kazi wakiwa mbali iwezekanavyo katika kupunguza mizunguko ya safari ya wafanyakazi na wakati huo huo kuwezesha uhakika wa huduma ya kharifa wa Mtume Petro kuendelea.

Hata hivyo kama ilivyokuwa imeanishwa katika hati ya Aprili 2, iliyosainiwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican ya kusimamishwa kwa shughuli za mahakama katika mji wa Vatican hadi Mei 4, mwanzoni ilikuwa imewekwa  tarehe ya mwisho kuwa Aprili 3.

14 April 2020, 16:51