Vatican News
TAHARIRI TAHARIRI  (© Vatican News)

Tahariri ya Tornielli:dharura ya janga na hamu ya jamuiya ya mwili na damu!

Katika mahubiri ya Papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta: “uzoefu wa kifamilia wa wakristo na Bwana daima ni wa kijumuiya,ni wa kibinafsi lakini katika jumuiya.Uzoefu wa kifamilia bila jumuiya,bila mkate,bila Kanisa,bila watu,bila sakramenti ni hatari”.

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Dk. Andrea Tornielli, Mhariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano katika tahariri yake kuhusu Injili ya Siku ya Ijumaa tarehe 17 Aprili 2020 kwa mujibu wa Papa ameanza kwa maneno yake: “Uzoefu wa kifamilia bila jumuiya, bila mkate, bila Kanisa, bila watu na bila sakramenti ni hatari”. Papa Francisko katika mahubiri yake katika  Kikanisa cha Mtakatifu Marta, Vatican, asubuhi kama kawaida yake ya kusindikiza na kuwatia moyo milioni ya watu ambao kwa kipindi hili wamelamika kujitenga  na ili kuwasaidia wabaki wameungana kiroho katika jumuiya na pia amezungumzia juu ya hatari ya imani inayoweza kujitokeza katika kuishi mtindo kama huu.

Tafakari ya Papa anaendelea Dk. Tornielli kuwa, inaanzia na simulizi ya Injili ya Yohane: "Yesu akiwa anasubiri wafuasi wake fukweni katika ziwa la Tiberiade", Yeye aliweza kubaki nao, kula pamoja nao samaki wa kuchomwa. Hii ni hali ya kifamilia inayojionesha kupitia njia ya kukaa mezani nao na kujadiliana kwa pamoja. Mtindo wa kikristo, ameeleza Papa Francisko ni uzoefu wa kila siku na Bwana, kama yule ambaye ukaa mezani wakati wa kufungua kinywa na kuzungumza kwa kawaida kile kitokacho rohoni. Huo ndio uzoefu wa kifamilia ambao daima ni wa kijumuiya, licha ya kwamba ni wa kibinafsi na wa kiundani.

Kwa sababu hii, anaendelea Dk. Tornielli, kunukuu mahubiri ya Papa kuwa, uzoefu wa kifamilia usio wa jumuiya, bila uhusiano wa kibinadamu, bila kushirikishana mkate, bila sakramenti, unaweza kuwa wa hatari katika kugeuka kwenda mbali na usio na mshiko. Hii ikiwa na maana ya kuangukia katika uhusiano wa familia binafsi ambayo imetengana na watu wa Mungu. Na wakati zoefu uliofanywa na mitume wa Yesu daima ulikuwa ni wa jumuiya ya kifamilia, ambao waliuishi na walifanya uzoefu mezani  ambayo ni ishara ya jumuiya na sakramenti na mkate. Tendo la kutengwa tulolazimishwa kwa wakati huu kwa sababu ya janga, ya kutoweza kushiriki katika sherehe ya Ekaristi katika hali hii ya dharura, isipelekee hatari ya kuishi imani kama vile ya kujitosheleza. Mamilioni ya watu leo huunganika kupitia vyombo vya habari ili kutafuta namna ya kuishi, kama kushiriki kijumuiya pamoja kupitia skrini, bila kuwa pamoja kimwili.

Ni mtindo wa lazima kwa wakati huu na ndiyo njia pekee inayowezekana katika dharura ambayo sisi sote  tunatumai itaisha mapema. Lakini hiyo haiwezi kutusahulisha kuwa Kanisa, Sakramenti na Watu wa Mungu ni halisi. Uzoefu wa kifamilia kwa njia ya vyombo vya mawasiliano ni msaada na vinawakilisha leo hii kwa mujibu wa Papa, ule  mtindo wa kuweza kuondoka katoka katika  handaki na wala siyo kukaa humo. Papa Francisko aidha anatuliaka zaidi tusifikirie mtindo huu kuwa wa kawaida , japokuwa unaendelea kuwasaidia watu wengi katika wiki hizi za mwisho, katika  kuwaondoa kwenye upweke na katika majaribu. Wakristo wamo ndani ya Jumuiya ya watu wa Mungu kwa dhati kwa maana ya kuwa  Watu mwenye mwili na mfupa ambao wanamega mkatew, wanasikiliza Neno, wanashirikishana upendo na kuwatangazia mmoja, mmoja kwa njia ya ushuhuda wa maisha na uhalisi ule uthabiti wa ukaribu na furaha ya Injili.

Watu wanatumia fursa za ubunifu wote utolewao na teknolojia mpya ili kuwaweka katika mawasiliano na kuwafikishia wale wote wanaoishi katika upweke, lakini ni wenye matarajio, kwamba wataweza kukutana kimwili katika Karamu ya ekaristi. Mhariri Tornielli aidha amehitimisha akiandika kuwa, watu wanaishi kila siku huku wakisindikizwa na Papa na ambapo Yeye anawatazama kwa shukrani kubwa makuhani wengi, watawa, watu wa kujitolea ambao katika siku hizi wanapata namna ya kukaa karibu na watu wanaokufa, wagonjwa, waliobaguliwa na kuokoa maisha yao na siyo kesi chache hata kwa kujisadaka maisha yao.

17 April 2020, 18:04