Tafuta

Vatican News
Kardinali Mario Zenari Balozi wa Kitume nchini Siria anahimiza watu wa Mungu kutokana tamaa katika kipindi hiki cha majaribu. Kardinali Mario Zenari Balozi wa Kitume nchini Siria anahimiza watu wa Mungu kutokana tamaa katika kipindi hiki cha majaribu.  (Vatican Media)

Siria#coronavirus:Balozi Zenari:Katika mateso hakuna kukata tamaa!

Kwa mujibu wa Balozi wa Vatican nchini Siria amesema mateso ya Kristo ni ya muda mrefu katika watu ambao wamekwisha choka lakini hawapaswi kuvunjika moyo.Bwana yupo pamoja nao kama alivyoshikwa huruma kwa umati uliokuwa umechoka na najaa,kama alivyomfufua Lazaro na mtoto wa mjane huko Naim aendelee kuwa na huruma hata watu wote.

Na Angela Rwezaula – Vatican

Tunatafuta kwenda mbele kwa mambo muhimu ya Pasaka, katika mateso, kifo na ufufuko wa Kristo kwa kutazama kona nyingine ile ya mateso ambayo yamekumba kwa muda mrefu watu maskini ambao wamechoka kwa muda wa miaka tisa ya vita. Na kwa sasa ni wasiwasi na hisia za unyong’onyevu wa ndani dhidi ya adui hasiye onekana yaani virusi vya corona. Kwa yote hayo hatupaswi kukata tamaa.

Katika mwanzo wa Wiki Kuu Takatifu, Kardinali Mario Zenari, Balozi wa Kitume nchini Siria amesema maneno hayo  kwa Nchi ya Siria na watu wa Mungu nchini Siria. Katika ujumbe wake anasema “miaka hii 9 ya vita, tumekuwa tukiadhimisha ibada za Wiki Kuu Takatifu. Ilitokea hata kuweza kuadhimisha Mkesha wa Pasaka wakati jua linawaka kabla ya kuingia usiku, kutokana hofu ya hatari ya mabomu na makombora. Wakati huu hatuwezi kusherehekea kwa maana makanisa yote yamefungwa na jambo ambalo hatujawahi  kujaribiwa na kuona. Kabla ya machafuko kulikuwa na mahujaji wengi waliokuwa wanatoka kila pande ili kuweza kushiriki ibada tofauti zilizopo nchini Siria.

Mwaka huu utajiri na uzuri wa ibada hizi umefungwa kutokana na virusi vya corona. Tutafute kwa namna hiyo kwenda mbele kwa kile ambacho ni muhimu kwa ajili ya Pasaka, katika mateso, kifo na ufufuko wa Bwana, huku tukitazama kwa upande mwingine. Ni mateso ambayo yamedumu kwa muda mrefu kwa watu hawa ambao wamecho kwa miaka 9 ya vita. Kardinali Zenari amesema Pasaka ni ushindi wa Kristo dhidi ya kifo na Siria pia ni nchi ya Mtakatifu Paulo ambaye anawahimiza kutumaini kwa kila tumaini na kwa maana hiyo Balozi wa Kitume anasisitiza kuwa hawapaswi kukata tamaa. “Bwana yupo pamoja nanyi na kama alivyoshikwa na huruma kwa umati ulikuwa umechoka na kwa njaa na kama alivyo mfufua Lazaro na mtoto wa mjane huko Naim aendelee kuwa na huruma hata kwetu sisi”.

Wapo watu wengi ambao katika migogoro ya Siria wamekuwa wema , wamekuwa wamekuwa wenye huruna , ni wasamaria wengi, ni wakirene wengi, ni waveronika wengi na ambao tumeweza kushuhudia kwa mambo mengi waliyotenda na  ambao bado wanaendelea kutoa msaada. Tunashuhudia ambao wanaendelea kutoa maisha yao kwa ajili ya jirani. Amesema Kardinali Zenari na kwa kuhitimisha amesema, “tunawaona hata nchini Italia wale wote ambao wanajitoa maisha yao kwa jili ya waathirika wa virusi vya corona.”

06 April 2020, 12:12