16-04-2016 Ziara ya Papa Francisko kwa wakimbizi na wahamiaji katika kisiwa cha Lesvos, Ugiriki 16-04-2016 Ziara ya Papa Francisko kwa wakimbizi na wahamiaji katika kisiwa cha Lesvos, Ugiriki 

Miaka minne iliyopita Papa alitembelea wahamiaji huko Lesvos!

Papa Francisko mnamo Aprili 16, 2016 alitembelea wahamiaji kisiwa cha Uigiriki huko Lesvos kwenye Bahari ya Aegean.Hisia za siku hiyo kwenye mahojiano ya Askofu Mkuu Nikólaos Printezis na Padre Ryszard Taraszkiewicz bado ziko hai hadi leo hii na Papa bado anaendelea kuwakumbuka kwa kutoa mshikamano wake.

Na  Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Sitaki kusahau kisiwa cha Lesvos,  ni katika maneno  hayo wakati wa siku  ya Pasaka 2020, Papa Francisko alitaka kukumbuka mateso mengi ya wahamiaji na wakimbizi, wengi wao wakiwa ni  watoto, waliohifadhiwa kwenye kisiwa cha Ugiriki. Katika makambi ya wakimbizi hao, ni hatua chache kufika katika  baharí ya Uturuki, ambapo Papa Francsiko alikwenda hasa miaka nne iliyopita, ambayo ilikuwa ni tarehe 16 Aprili 2016 katika Kambi ya wakimbizi ya Moria. Siku hiyo alikuwa na Patriaki  wa Kiekumene wa Konstantinople, Bartholomew na Askofu mkuu Ieronymos wa Athene na Ugiriki yote.

Pamoja na kutembelea kisiwa hicho lakini u uhusiano wa karibu  haukukatika kamwe ule wa Papa na kisiwa cha bahari ya  Aegean, ambacho leo ni kambi  ya Moria,  kambi isiyo rasmi  iliyoibuka nje ya mji ambayo hukaribisha watu wasiopungua 19,000, wengi wao ni kutoka Afghanistan, lakini pia wakimbizi kutoka Iraq, Iran, Siria, Yemen na Afrika ya Kaskazini. Makambi haya hayana uwezi wa kufanya mapokezi na katika dharura kama hii ya Covid-19 wakimbizi  maelfu katika masaa haya wako wanahamishwa kwa muda na mamlaka ya Ugiriki kwenda kwenye hoteli za kawaida. Kesi nane za Covid-19 kati ya idadi ya watu zimetambuliwa huko Lesvos na moja kwenye kisiwa cha Samos.

Askofu Mkuu Printezis

Msipoteze matumaini, ulikuwa ndiyo ujumbe wa Papa Francisko aliopendelea kuwaachia wahamiaji wa Lesvos kabla ya kurudi Italia akiongozana kwa mshangao mkubwa na familia tatu za wanaoomba hifadhi kutoka Siria. Ilikuwa ni ziara iliyokuwa na shauku ya nguvu, si tu kwa wahamiaji peke yake lakini pia  hata kwa wazalendo wa Lesvos. Amethibitisha hayo katika simu ya  Vatican News,  Askofu Mkuu  Nikólaos Printezis, msimamizi wa kitume wa Jimbo Chios, Lesvos na Samos, aliyefutalia kwa karibu sana maandalizi yote na Siku ya Ziara ya Papa Francisko katika Kisiwa hicho kunako tarehe 16 Aprili 2016. Katika kukumbuka siku hiyoAskofu Mkuu anathibitisha ni kwa jinsi gani walikuwa wamendaa ziara hii kwa shauku kubwa,  hata watu wengine waliofika kutoka Upatriaki wa Costantinoples wa Athene na Roma. Watu wote hao walikuwa na furaha kubwa, wawe wakatoliki hata waorthodox, lakini zaidi kwa wakimbizi na wahamiaji.

Tayari ni miaka minne  imepita lakini ni kama ilivyokuwa na dharura ya wakati ule. Leo hii hali kwa bahati mbaya zimedharauriliwa na kuwa mbaya, zaidi. Ndiyo  Serikali imefanya kila liwezekanalo anasema Askofu Mkuu  hata kwa kuwahamisha wengine mahali pengine, kwa sababu kisiwa ambacho kinakaribisha mamia elfu ya wakimbizi , katika kambi hiyo ina uwezo wa kupokea watu 800 tu,  lakini hadi sasa ni zaidi ya watu 15,000! Ameshuhudia Askofu Mkuu Printezis. Hawa ni watu ambao kiukweli wanaishi bila nyumba halisi, bila vyoo hivyo kuna shida kati ya watu ambao hawatoki nchi moja, ambao wangependa kurudi nyumbani au kwenda Jimbo lingine la Ulaya kutafuta maisha bora.

Utume wa Kardinali Krajewski

Ikumbukwe ilikuwa mwezi Mei na baadaye mwezi Desemba mwaka jana 2019 ambapo Papa Francisko amlimtuma huko Lesvos Kardinali Konrad Krajewski, msimamizi wa Sadaka ya Kitume ambaye alipeleka huko mshikamano wa Papa kwa wahamiaji akisindikizwa na Kardinali Jean-Claude Hollerich, Askofu Mkuu wa Luksemburg na Rais wa Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya (Comece), Askofu Mkuu Sevastianos Rossolatos, wa Jimbo Kuu la Athenes na wahudumu wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ambao wanajikita katika kutoa huduma ya kisiwa hicho.

Ushuhuda wa Padre Taraszkiewicz

Papa pia anaendelea kutoa matumaini kwa wahamiaji wa Lesvos ili kuendelea mbele kwa hali yoyote ile,  anathibitisha Padre Ryszard Taraszkiewicz, makamu  Jimbo la Chios na Paroko wa Parokia ya Maria  Mama Yetu Mpalizwa  huko Samos. Katika ziara ya Papa kunako  2016, Padre huyo anakumbuka hisia kubwa iliyokuwa inajionesha kwenye nyuso za wahamiaji, iliyoongozwa na mtu ambaye aliwakilisha kilio chao  baharini, licha ya bahari zilizoko duniani. Padre aidha amesema katika hali hii, hata bila  virusi vya corona leo hali ni janga, ni aibu kwa sababu ni hali ya maisha ambaya siyo ya hadhi kwa yoyote yule na wamba siyo vigumu kutweza kufikiria hasa kwa yule ambaye anaisha nje ya Ulaya. Amehitimisha Padre Ryszard

16 April 2020, 16:05