Kila saa sita kamili kila siku katika kipindi hiki cha dharura ya corona Kardinali Comastri Msimamizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro anasali sala ya Malaika wa Bwana na kufuata rosari. Kila saa sita kamili kila siku katika kipindi hiki cha dharura ya corona Kardinali Comastri Msimamizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro anasali sala ya Malaika wa Bwana na kufuata rosari. 

Malaika wa Bwana:coronavirus-19:Kard.Comastri,Yesu Msulibiwa utuhurumie sisi wadhambi!

Kardinali Angelo Comastri msimamizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kila saa sita mchana kila siku anaongoza sala ya Malaika wa Bwana na Rosari Takatifu.Ijumaa tarehe 3 Machi 2020 wakati wa sala na rosari amesema Yesu msulibiwa utuhurumie sisi wadhambi hasa katika kipindi hiki. uwasaidie wahudumu wa afya na makuhani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Yesu msulibiwa utuhurumie sisi wadhambi hasa katika kipindi hiki. Ndivyo alivyosema Kardinali Angelo Comastri, msimamizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Na wakati wa kuhitimisha sala ya Rosari inayotanga     zwa moja kwa moja katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican baada ya sala ya Malaika wa Bwana  Ijumaa tarehe 3 Aprili 2020 ameoba kusali kwa ajili ya majuhani, madaktari na wahumudu wote ambao wako ktika harakati za kusaidia waonjwa wa corona.

Katika tendo la kwanza la Uchungu, Yesu ambaye katika bustani ya mizetuni ambaye anasali, anateseka na kutokwa damu, anachukua mabegani mwake ule uzito wa dhambi zetu, amesema Kardinali Comastri. Aidha “sisi ndiyo watesa  Mungu lakini Mungu  anajionesha na upendo mkubwa dhidi ya ukatili wetu, Wewe uliingia katika historia ya kibinadamu na kukutana na kizingiti.”ametafakari trndo la Pili, Hii ni hali halisi inayo umiza moyo kwa sababu tumeitengeneza sisi, hasa kwa njia ya dhambi zetu za kuburi, ametafakari katika tendo la tatu la Uchungu na ambao anasema tunatafakati Yesu akiwa amevikwa taji la miiba, anadharauliwa anachekwa hadi kupigwa kofi na mtumishi wa kuhani.

Upendo uko kwetu sisi sasa unageuka kuwa baridi, ee Mungu tusaidie ili tujitambue sisi katika upendo wa kweli, amesisitiza Kardinali Comasti na kwa upande wa Tendo la nne la Uchungu ambao Yesu anabeba msalaba wake kuelekea Kalvari  na kusaidiwa na  wakati huo huo kutiwa moyo na uwepo wa mama yake Maria.

Katika Tendo la tano la uchungu, unatuonyesha juu ya Kalvari, mahali ambapo Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya upendo wetu. Tangu wakati huo ulinazidisha  kububujika upendo mkubwa ambao hata lep unabisha hodi  katika  milango ya mioyo yetu  na huku ukisubiri jibu amesema Kardinali Comastri. Na hatimaye  sala kwa Matakatifu Malaika Mikaeli,” amesema: “Tusali kwa ajili ya makuhani ambao pamoja na madaktari na wahudumu wa afya, wako wanaonyesha wema wa ajabu na kujikita kwa dhati katika kusaidia wagojwa. Uwapatie nguvu wote ambao wanawakimbilia wagonjwa katika janga hili kubwa”.

03 April 2020, 14:11