Vatican News
Yesu alifufuka kaburi li wazi Yesu alifufuka kaburi li wazi 

Kufa katika Kristo

Katika makala ya tano yenye kichwa "shajara la mgogoro",Padre Lombardi anaandika kuwa kwake Yesu hakuna kifo kilicho sahulika,hakuna sehemu yoyote ya dunia na katika historia,hakuna pembe yoyote ya dunia ambayo kifo kimesahulika.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika makala ya tano ya  Padre Federico Lombardi aliyoipatia kichwa:" shajara la mgogoro"anajikita kutafakari toleo hili kuhusu "kifo katika Kristo". Kwa mujibu wa Padre Lombardi amesema moja ya mambo yaliyoanzishwa kiroho ya Mtakatifu Yohane Paulo II ilikuwa ni ile ya kutuhimiza tuwe na chachu na kuhifadhi kumbu kumbu ya wafia dini wa karne ya XX, moja ya karne iliyokuwa na ghasia zaidi ya kihistoria. Kwa hakika anaandika, akikimbuka mbele ya Mungu mashahuda wengi wa imani ambao tunaalikwa kuwakumbuka hasa waathirika wengi na kwa kiasi kikubwa wanawake na wanaume wa kila rangi na kabila, kila wakati na hali halisi ambayo walipoteza maisha yao kwa majanga mbalimbali kama vile, katika nchi kavu na baharini, katika vita na amani, mbali na kutiwa moyo kibinadamu, waathirika wa ghasia  sisizo na maana, au majanga yasiyo tabirika, au kuachwa peke na upweke.

Padre Lombardo anaandika kuwa kilio kikuu cha uchungu ambacho kinaonekana kuinuka katika ukimya wa vumbi za kila pembe ya nchi kwa yule mwenye kuwa na masikio ya kusikia akikumbuka mamilioni mamilioni ya waliosahulika. Aidha  ni katika janga la kiumbe ambaye anahisi kunguka kwenye giza la utupu wa mauti. Kwa ajili yao pamoja na,  Padre Lombardi  anaandika, kuwa "tunataka kuinua kilio na kuomba huruma". Kwa kukumbusha hali halisi iliyojitokeza katika nyakati hizi za janga, Padre Lombardi anaandika kuwa, picha ya msululu wa majeneza katika makanisa ya Lombardia nchini Italia, au kwa kutazama kabui la pamoja karibu na jiji la  New York, mawazo ya watu wengi, kwa namna ya pekee ya watu wazee ambao wamekufa katika hali ya upekwe na kuwachwa katika mchakato wa miezi hii ya mwisho imetugusa kwa kina.

Padre Lombardi aidha anongeza kuandika kuwa siyo tu ule uchungu wa ndugu ambao hawakuweza kukaa karibu na wapendwa wao kwa kuwapa moyo kibinadamu na kikristo lakini pia hata kwa marehemu wenyewe ambao  wamekufa kwa upweke bila wa kuwasindikiza kwa dakika za mwisho. Yote hayo ameandikia yametufanya tutambue kwa mara nyingine tena ni  jinsi gani ilivyo na thamani kubwa ya ukaribu na upendo wa dhati katika kipindi cha udhaifu, kipindi cha uzee na katika magonjwa. Vile vile hata kutufanya tuwe na tafakari kuwa kila kifo, ikiwa pamoja na kifo chetu, kinapelekea daima ukuu wa upweke. Kwa sababu mwisho wa kila tulizo na ukaribu wa wengine, unageuka kutokuwa na maana na zaidi uwezo wa kuondoka katika ile hatua ya mwisho.

Padre Lombardi anauliza swali: ni jinsi gani tunaweza kuondokana na hali hii katika wakati ambao tunafafanana wote na ambapo kwa ajili ya waathirika wa virusi viliwakumba,  hata hivyo mbele yao  ni kama mbele yetu? Ni jinsi gani ya kukwepa uchungu unaotugusa? Katika kufafanua  amesema: "Siku chache tumekuwa na neema ya kushi uzoefu wa kifo cha Yesu. Kila siku tunaishi tukiungana kisakramenti na kiroho na Yesu katika komunio. Lakini Ijumaa Kuu na Jumamosi Kuu inaleta neema maalum. Kifo cha Yesu ni kifocha kweli na cha ukatili mkubwa sana ambacho kinaonyesha uzoefu wote e wa kuachwa pekee na watu na hata fumbo la kuachwa kwa upande wa Baba yake, kama isemavyo Zaburi , ambayo Yesu alitamka juu ya msalaba. Kifo ni cha kweli ambacho kinaingiza  maiti katika kaburi siku ya Jumamosi….

Yesu kutoka katika wafu, ni kusema kwamba yeye anajifanya kuwa karibu na ndugu wote ambao wameshuka kuzimu katika mauti. Hasahau hata mmoja. Kwake yeye Yesu hakuna hata kifo kimoja kilichosahulika  na wala katika sehemu yoyote ya nchi na katika historia, hakuna hata katika kona yoyote iliyoguswa na janga. Yesu kiukweli alikuwa kama wao na pia nao. Baada ya kifo cha Yesu na  kushuka kwake kuzimu na ufufuko wake, kifo siyo kama kile cha awali. Na ndipo Paulo anauliza swali: je huko wapi ushindi wako we kifo? Kifo sasa kinaweza kufanyiwa uzoefu na Yesu, anaye onyesha upendo  wa Mungu kuwa wenye nguvu zaidi ya kifo. Hii inakwenda zaidi ya upweke kuibinadamu. Kifo hata ambacho hakijulikani na kusahauliwa kinaweza kugeuka na  kukabidhi roho katika mikono ya Baba.

Siku chache zilizopita, Papa Francisko akitafakari neno katika kikanisa cha Mtakatifu Marta, kuhusiana na mazungumzo kati ya Yesu na Nikodemu, aliwaalika waamini wote kutazama Msalaba. Ni kitovu cha imani na maisha ya kikristo, amesisitiza Padre Lombardi. Aidha anakumbusha kwamba "Aliyeona hawezi kusahau sura ya Mtakatifu Yohane Paulo II akikumbatia msalaba katika kikanisa kidogo siku chache kabla ya kifo chake, wakati watu wa Mungu walikuwa wameunganika pamoja katika Colosseo kwenye sala ya Njia ya Msalaba Ijumaa Kuu.  Kwa maana hiyo anathibtisha kwamba "Hakuna njia nyingine ya kujiandaa kuishi kifo kama siyo kutazama kwa roho yote msalìaba ambao unakufa nasi na kwa ajili yetu na ubaki umekumbatiwa na Yeye kwa moyo wote.

Kwa maana hiyo, kufanya uzoefu wa kifo na Yesu,  Padre Lombardi anabainisha kuwa, unaweza kupoteza uso wake wa kuogopesha na kuacha kutambua fumbo la upendo na huruma. Na kwa kufanya hivyo labda tutaweza kuhisi ule msisitizo wa kukataa wazo na kulifuata katika maisha yetu ya kila siku na zaidi kwa imani na kadiri muda unavyoisha ndivyo tutaweza kuona kama ndugu na hatimaye kuwa kama “dada” kama alivyoita Mtakatifu Francisko wa Assisi. Kwa kuhitimisha Padre Lombardi anaandika kuwa hata katika dunia iliyo na utandawazi, kifo kinafika, kwa virusi vya corona au kwa namna nyingine. Lakini tusisahau kuwa kwa neema ya Yesu Kristo, kifo hakina neno la mwisho, bali kila kifo hata kilichosahuliwa na upweke hakitapotei, bali ni yumo katika mikono ya Baba.

   

28 April 2020, 17:26