Tafuta

2020.04.14 Kardinali Peter Turkson Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Watu 2020.04.14 Kardinali Peter Turkson Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Watu 

Kard.Turkson:Tunafikiria baada ya COVID-19 tusikutwe bila kujiandaa!

Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Watu anasisitizia jitihada zinazofanywa kwa ajili ya Makanisa mahalia ili kuokoa maisha ya binadamu na kusaidia maskini.Katika kukabiliana na hilo wameunda makundi matano ya kazi kwa ajili ya kukabiliana na dharura na kufikiria wakati endelevu.

Kanisa liko mstari wa mbele duniani kote katika kukabiliana na matokeo ya virusi vya corona. Haiitaji mipango ya afya tu, lakini hata uchumi na kijamii unaoelekeza muda mfupi na kipindi kirefu. Wakati wanaendelea na utafiti wa chanjo na matibabu ya kutokomeza COVID-19, utabiri wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa wa 2020 unazungumza juu ya kushuka kwa asilimia 3% ya bidhaa ya ndani ya ulimwengu. Kupungua  huko kunaweza kuwa mbaya zaidi kuliko mdororo mkubwa uliowahi kutokea kunako mwaka 1930. Kufutia na suala hili Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya watu anasisitiza kuwa mgogoro huu unahatarisha kufuatia mchakato mwingine na zaidi, ambao utalazimika kujifunza pole pole na kwa uchungu wa kutunza nyumba yetu ya pamoja kama vile Papa Francisko anafundisha hivyo katika unabii wa kitabu cha Laudato si.

Kardinali amesema hayo  wakati akihojiwa na Mwandishi wa habari wa Vatican News Massimiliano Manicheti. Akijibu swali kuhusu kukutana na Papa Francisko mara nyingi katika dharura ya virusi vya Corona ameeleza juu ya wasiwasi wake katika wakati huu , janga la kidunia linalotokana na COVID-19 na majanga mengine ambayo yanajionesha katika upeo. Papa ameagiza kwamba wasipoteze muda, bali wajikite mara moja katika kazi, kwa kuwa wao ni sehemu ya ya Baraza husika ambalo lazima waanze kwa haraka. Wanapaswa wafikirie baada ya janga hilo.

Kuhusiana na jukumu walilopewa na utume wao, Kardinali Turkson amesema kuwa Papa amewakabidhi majukumu msingi. La kwanza ni kutazama leo hii yaani kuona ulazima wa kuwa tayari, kuhamasisha na kuwa thabiti kama ishara ya dhati ya msaada kutoka kwa Baba Mtakatifu na kwa upande wa Kanisa. Lazima kutoa mchango wao katika kipindi hiki cha dharura. Hii ina maana yakujiktia katika kambi mara moja ya matendo ya kusaidia makanisa mahali ili kuokoa maisha ya watu  na kusaidia maskini zaidi.

Pili ni suala linalotazama baadaye, wakati ujao kuangalia mabadiliko. Papa anaamini kwamba tupo katika mabadiliko ya nyakati na yuko anafikiria kile kitakachokuja baada ya dharurua hii, juu ya matokeo ya uchumi na jamii ya janga, ni kwa namna gani ya kuweza kukabiliana hasa mambo  ambayo Kanisa linaweza kutafuta njia sahisi katika dunia yenye mahangaiko.  Kuchangia ufafanuzi wa wazo juu ya hilo pia na kazi yao ya pili amethibitisha.

Papa ameomba kwa dhati na ubunifu, njia ya kisayansi na mawazo, fikra za ulimwengu na uwezo wa kuelewa mahitaji ya ndani. Kwa kufafanua juu ya shughuli hii Kardinali Kodwe anasema wameunda makundi ya kazi. Wamekwisha kukutana mara mbili na kikundi cha kazi na Baba Mtakatifu. Aidha wamumeunda kikundi cha kudhibiti na kuratibu mipango inayohusu hatua za leo hii na zile zinazohusu kuandaa kesho. Huduma yao ni katika vitendo na mawazo. Zinahitajika vitendo halisi sasa na utekelezaji wakweli. Amesisitiza kwamba wanahitaji kutazama upeo zaidi ya leo . Kwa kutofikiri ya kesho inawezekana wakakutwa bila kujiandaa na kutoweza kufanya lolote. Ni kuanza kufikiria ya  kesho na siyo mbadala. Hatujakabiliwa na "aut aut" lakini na "et et". Timu yetu tayari imeanzisha ushirikiano

Timu yao imeanza ushirikiano na Ofisi ya Katibu wa Vatican na Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Caritas Internationalis, Baraza la kipapa la Elimu na sayansi; Taasisi ya Kipapa ya Maisha na Sadaka Kuu ya Kitume, Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu na Duka la madawa Vatican. Kwa timu hii wameunda mitindo mbali mbali kwa maana ya upya wa ushirikiano kati ya mabaraza tofauti na ofisi mbalimbali za Vatican. Ni aina na nguvu kazi . Mtindo mpya wa utekelezaji wa matendo ambao ni ushuhuda wa ubinadamu na uwepo wa matendo ya Kanisa kwa mujibu wa Kardinali Turkson.

Tume imeundwa na makundi 5

Kundi la kwanza tayari liko kazini kuhusiana na dharura. Hawa wanafanya kazi na Caritas Internazionale.  Wameanzisha mfumo wa kusikiliza makanisa mahalia ili kuainisha mahitaji halisi na kusaidia maendeleo yanayostahili. Wameomba Mabalozi wa kitume na Mabaraza ya maaskofu ili kutoa taarifa ya masua ya kiafya na kibinadamu yanayohitajika kwa haraka. Inahitaji kuwa na mtazamo mpana. Inahitajika kwa sababu hasije sahaulika yoyote kama vile wafungwa na makundi ya wenye mazingira magumu. Inahitaji kushirikiana katika matendo mema.

Kundi la pili lina kazi kama ya usimamizi ili kutazma machweo. Ili kufanya hivyo ni kuleta pamoja na kuunganisha akili katika sekta za kiekolojia na inahitajika unabii na ubunifu. Inahitaji kutazama upeo zaidi kwa maana hiyo shughuli hii imekabidhiwa kufanya kazi karibi sana na Taasisi za kipapa za Elimu ya Masha, Taasisi ya Elimu ya Sayansi na Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Sayansi Jamii.

Kundi la tatu kazi yake ni kutoa na kuwasilisha kazi yao na kuijenga kwa njia ya mawasiliano kuhusu utambuzi mpya kuwaalika kwa njia ya kuawasilisha jitihada za ubunifu  shughuli iliyo kabidhwa kitengo cha Maendeleo  kibinadamu kuhusika na timu hiyo.

Kundi la nne linaendeshwa na Ofisi ya Katibu wa Vatican ambayo inajikita katika uwezekano mambo yote yanayotazama uhusiano na ushirikiano na Mataifa au mashirika ya kimataifa. Kuna haja hata ya kuwa na matendo ya dhati na unabii.

Kundi la tano litajikita kutafuta kwa namna iliyo wazi fedha za lazima ili kuhamasisha mzunguko huo wa utajiri.

Wako katika hatua za kwanza amesema Kardinali Turkson lakini pi wakitambua  kuwa kuna kazi ya kufanyanya. Watajitahidi kwa nguvu zao zote kwa kila iwezekanavyo.Tayari wamekwisha anza kuwahusisha hata taasisi nyingine ambazo kiutamaduni hadi sasa wamekuwa wakishirikiana na Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo ya watu kwa mfano Chuo Kikuu Georgetown , Chuo Kikuu Potsdam, Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu Milano na Taasisi ya World Resources(taasisi ya rasilimali za dunia) na nyingine pia.

Aidha akizungumza juu ya mashirika ya kitawa na jumuiya mbalimbali na vyama vya kitume ambavyo vimejikita katika dharura na mshikamano wa kikanisa duniani Kardinali Turkison amesema kuwa mtandao wa Kanisa katika Nchi mbalimbali ni muhimu. Kazi inayotendwa na Caritas ni maalum. Kila kitu kitakachofanywa kitakuwa katika muungano kati ya Roma na Makanisa Mahalia. Ni timu kwa ajili ya huduma ya Papa na kwa Makanisa. Wote wako katika huduma ya kuhudumiana mmoja na mwingine. Siyo rahisi kutambua leo hii katika kipindi ikiwa hakuna hatua yoyote ifanyikayo. Kwa kufanya hivi ni kuonesha umoja wa Kanisa la Ulimwenguni.

Kardinali Turkson akifafanua kwa nini ni muhimu kufikiria juu ya matarajio ya siku za usoni? Anasema : "Kuwaza  mara moja juu ya kile kinachofuata ni muhimu ili tusije kukutwa bila kuwa na  utayari. Mgogoro wa kiafya tayari umesababisha mzozo wa kiuchumi. Na ikiwa mgogoro wa kiuchumi hautashughulikiwa mara moja, inahatarisha mgogoro wa kijamii. Shida ya hatari itafutana moja baada ya nyingine katika  mchakato ambao tutalazimika kujifunza pole pole na kwa uchungu kutunza nyumba yetu ya pamoja, kwani Papa Francisa anafundisha hivyo kwa unabii katika kitabu cha laudato si."

Kuna haja ya ujasiri, na unabii. Papa alisema hayo waziwazi katika ujumbe wake wa Urbi et Orbi. Huu sio wakati wa kutojali, wa ubinafsi, wa migawanyiko; kwa sababu ulimwengu wote unateseka na lazima tujikite katika umoja ili  kukabili janga hili. Badala ya kupunguza  vikwazo vya kimataifa ambavyo vinazuia uwezekano wa nchi zinazopokea kutoa msaada wa kutosha kwa raia wao. Ni wakati wa kupunguza, ikiwa sio kusamehe, deni ambalo lina uzito juu ya bajeti ya nchi masikini zaidi. Ni wakati wa kuamua suluhisho za ubunifu. Ni wakati wa kupata ujasiri wa kuunga mkono wito wa kukomesha mapigano ya ulimwengu na mara moja katika pembe zote za ulimwengu. Huu sio wakati wa kuendelea kutengeneza na kuuza silaha, kutumia pesa nyingi ambazo zinapaswa kutumiwa kuponya watu na kuokoa maisha.

Kardinali Kodwe akijibu swali ni jinsi gani ya kuishi mwanadamu katika majaribu anasema: Mwanadamu leo hii anagundua udanganyifu wake wote. Anagundua tena, awali ya yote, kwamba kuishi katika Dunia kama Nyumba ya pamoja inahitaji jambo kuu zaidi: inahitaji mshikamano katika kupata uzuri wa uumbaji kama "uzuri wa pamoja", na mshikamano katika kutumia matunda ya utafiti na teknolojia ili kutengeneza Nyumbani yenye kuweza kuihsi kila mtu.

Katika hili, mwanadamu anamtambua Mungu kwa mara nyingine  tena, ambaye amemkabidhi mwanadamu jukumu hili kwa mshikamano. Anagundua ni kiasi gani hatima ya kila mtu imefungamana na ile ya wengine. Anagundua tena thamani ya vitu ambavyo ni vya muhimu na isiyo ya thamani ya vitu vingi ambavyo tulidhani ni muhimu. Kama Papa alivyosema kunako Machi 27: "Dhoruba inaondoa kuathirika kwetu na  kuacha udhihirisho huo wa uwongo na ulio wa kijuu  juu ambao tumeundia ajenda zetu, miradi yetu, tabia zetu na vipaumbele vyetu."

15 April 2020, 17:23