Tafuta

Vatican News
Papa Francisko ameunda Jipya Jipya la Kontangora nchini Nigeria na kumteua Padre Bulus Dauwa Yohanna kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Kontangora. Papa Francisko ameunda Jipya Jipya la Kontangora nchini Nigeria na kumteua Padre Bulus Dauwa Yohanna kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Kontangora.  (Vatican Media)

Jimbo Katoliki la Kontangora: Askofu mteule Pd. Bulus Yohanna

Jimbo jipya la Kontangora, Nigeria litaongozwa na Askofu Myeule Bulus Dauwa Yohanna na litakuwa chini ya Jimbo Kuu la Kaduna. Jimbo linaundwa na eneo la Niger na Kebbi; maeneo yaliyoko Kaskazini mwa Nigeria yanayohudumiwa na Shirika la Wamisionari wa Afrika, S.M.A. Wakati huo huo, St. Michael ndilo litakalokuwa Kanisa kuu la Kiaskofu na Makao makuu ya Askofu Jimbo.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameunda Jimbo jipya la Kontangora, lililoko nchini Nigeria na kumteua Mheshmiwa Padre Bulus Dauwa Yohanna kuwa Askofu wake wa kwanza. Jimbo Katoliki la Kontangora litakuwa chini ya usimamizi wa Jimbo Kuu la Kaduna, Nigeria. Jimbo hili linaundwa na eneo la Niger na Kebbi; maeneo yaliyoko Kaskazini mwa Nigeria yaliyokuwa yanahudumiwa na Shirika la Wamisionari wa Afrika, S.M.A. Wakati huo huo, St. Michael ndilo litakalokuwa Kanisa kuu la Kiaskofu na Makao makuu ya Askofu Jimbo.

Jimbo linaundwa na Parokia17 na Makanisa 3 ya Kimisionari yanayohudumiwa na Mapadre 25 wa Jimbo na Watawa 10. Jimbo lina watawa 29 na Waseminari 13. Lengo la kuanzisha Jimbo Jipya ni kutaka kusogeza huduma za shughuli za kichungaji kwa watu wa Mungu. Kumekuwepo na ongezeko kubwa la waamini katika eneo hili, jambo ambalo limechangia uamuzi wa Baba Mtakatifu kuunda Jimbo jipya la Kontangora, huko nchini Nigeria.

Jimbo Jipya Nigeria

 

03 April 2020, 11:52