Tafuta

Vatican News
2020.04.15 A.I.F Mamlaka ya habari za Fedha  2020.04.15 A.I.F Mamlaka ya habari za Fedha   (Vatican Media)

Dk.Giuseppe Schlitzer ni mkurugenzi mpya wa AIF

Kardinali Pietro Parolin amepyaisha mwongozo wa Mamlaka ya Ushauri wa Fedha mjini Vatican kwa kumteua Dk.Giuseppe Schlitzer.

VATICAN NEWS

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari Vatican Dk. Giuseppe Schlitzer ndiye Mkurugenzi mpya wa AIF, yaani Mamlaka ya Habari ya kifedha Vatican katika mapambano dhidi ya utapeli wa pesa, ubadilifu na ufadhili wa kigaidi. Dk .Schlitzer aliyeteuliwa na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican anachukua nafasi ya ya Dk. Tommaso Di Ruzza ambaye alimaliza kipindi chake cha miaka mitano tarehe 20 Januari. Aidha Kardinali Pietro Parolin amemteua hata Mkurugenzi msaidizi wa Mamlaka ya ushauri wa Fedha Dk. Federico Antellini Russo.

Majiundo ya Schlitzer ni shahada ya uchumi na Biashara katika Chuo Kikuu cha Federico II cha Napoli, Italia na kuendelea na shahada ya juu ya uchumi katika Chuo Kikuu cha Chicago na Chuo Kikuu cha George huko Washington Marekani. Amekuwa Profesa wa usimamizi wa Fedha Kimataifa katika chuo kikuu LIUC cha Cattaneo, Castellanza. Ni mwandishi wa vitabu vingi kuhusu mada za  uchumi na fedha, utabiri wa uchumi, utawala na maadili ya biashara. Aidha ameshika nafasi mbalimbali za uongozi katika sekta husika ya uchumi.

15 April 2020, 17:03