Tafuta

Vatican News
2020.04.16 CARITAS INTERNATIONALIS 2020.04.16 CARITAS INTERNATIONALIS 

Caritas Internationalis:Wema na wepesi katika kusaidia walio hatarini!

Bwana Aloysius John,Katibu mkuu wa Caritas Intenationalis anaeleza kwamba wao ni sehemu ya tume baada ya Covid-19 iliyopendekezwa na Papa.Kwa njia hiyo wameunda Mfuko kwa ajili ya kusaidia Nchi zilizo na matatizo kwa sababu ya janga hili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Watu wote matatizo mengi  ambayo yamejionesha katika ulimwengu na ugonjwa wa virusi vya corona, lakini walio wengi hawana njia na zana sawa kuweza kupambana. Zaidi ya hayo siyo rahisi kuwaomba watu waheshimu kanuni za sheria zilizowekwa kufuatwa na jamii ikiwa wana njaa na hawajuhi ni wapi wanapate chakula. Au kuzingatia viwango vya afya ikiwa hakuna maji safi. Na ni katika pengo hili kwamba Caritas Internationalis inafanya kazi kwa kina, hata zaidi katika janga hili na zaidi ya yote kwa sababu Papa amewaomba wao moja kwa moja. Bwana Aloysius John amefafanua juu ya kwenda kukutana na Papa Francisko ili kumwakilishia matendo ya kazi baada ya covid-19 na akawambia kuwa, “Ninyi muwe wema na wepesi na kuendelea kupeleka mbele kazi yenu. Ikiwa hamfanyi ninyi, je ni nani atafanya hivyo”.

Baraza la kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungani ya watu katika harakati

Shirikisho la Caritas Intarnationalis limetawanyika katika sayari zaidi ya miundo 160 ya eneo hilo ambalo limetangaza kuwa sehemu ya Tume iliyoanzishwa na Papa Francisko kwa kuongozwa na Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya watu. Baraza hili litakuwa katika kukundi  cha kwanza cha kufanya kazi ya Tume itakayojikita katika kusikiliza na kusaidia Makanisa mahalia.

Daima Caritas Internationalis inatafuta kutoa majibu

Imekuwa inajikita kuwa mstari wa mbele , anakumbushwa Bwana John na mgogoro wa dunia ambao umeletwa na virusi kwa hakika una tabia ya dharura hasa. Zaidi ya Mabaraza ya Maaskofu 140 yameeza kujibu masawali yaliyolewa kwa kuelekeza ni mahitaji yapi  ya dharura kulingana na Nchi husika na ni mipango kiliyopo ya kushughulikia kuthibiti usambaaji  wa janga. Bwana John ameongeza kusema “hii itaturuhusu katika mkakati kwa kushirikiana na  Baraza  kutoa majibu ya kutosha.

Umakini wa hali ya juu kwa nchi zenye umaskini zaidi

Akiendelea kuelezea katibu wa Caritas Internationalis amesema kuwa “umakini uko juu zaidi, kwa nchi hizo ambazo kuenea kwa janga hilo kungekuwa na athari mbaya zaidi kuliko zile ambazo tumeshuhudia huko Ulaya". Na hapa  ndiyo maana kumezaliwa wazo la kuwa na “Mfuko kwa ajili ya Kujibu COVID-19", ambayo ni  njia ya kukusanya michango ili kuweza kusambaza huduma kuhusu kuzuia maambukizi na kudhibiti, ufikiaji wa huduma za usafi, ugavi wa vifaa vya kinga vya kibinafsi (vibarakoa, glavu, nk), usalama wa chakula.

Maeneo mengine hawafuatilii hatua za usalama

Aidha amefafanua Bwana John kuwa “Kwa bahati mbaya kuna maeneo ambayo janga hilo linachukuliwa kuwa ni ubaya ulio mdogo kabisa  hasa kwa idadi ya watu walio katika mazingira magumu. Nchini Rwanda, kwa mfano, katika maeneo mengine watu hawafuatilii hatua za usalama kwa sababu ya uhaba mkubwa wa chakula. Wanatuambia kuwa “tunapendelea kufa na Covid kuliko njaa”. Mfano mwingine unatoka Caritas Yerusalem,  kule Palestina ambapo kuna hatari kubwa ya fedha za kuweza kusaidia usambazaji wa chakula na vifaa vya usafi binafsi kwa familia 500 kwenye shida .

Kuungana pamoja kwa njia ya mshikamano

Wito wa Bwana Aloysius John ni ule wa kuchangia: “ Leo sisi sote tunaunganishwa na hofu, lakini tunatakiwa hata kuuungana katika mshikamano kwa njia ya udugu ulimwenguni. Moja ya njia ya ya kushinda janga hili ni ile ya kuungana kwa pamoja ili kukabiliana na changamoto kubwa ya kibinadamu.

Hata hivyo kwa mujibu wa Caritas Internationalis inatoa taarifa kuwa inawezekana michango kutolewa kupitia tovuti yao

https://www.caritas.org/donation/covid-19-response-fund/

Vinginevyo, unaweza kutumia akaunti iliyowekwa ya Taasisi ya shughuli za Kidini IBAN: VA29001000000020179007

16 April 2020, 16:31