Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Francisco Montecillo Padilla kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Guatemala. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Francisco Montecillo Padilla kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Guatemala. 

Askofu mkuu Padilla ateuliwa kuwa Balozi nchini Guatemala

Askofu mkuu Francisco Montecillo Padilla alizaliwa mwaka 1953 Jijini Cebu, Ufilippini. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, 21 Oktoba 1976. Tarehe 1 Aprili 2006 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea na Visiwa vya Solomon. Tarehe 23 Mei 2006 akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu na Kardinali Ricard J. Vidal.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Francisco Montecillo Padilla kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Guatemala. Kabla ya uteuzi huu Askofu mkuu Padilla alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Kuwait, Yemen, Bahrein na kwenye Nchi za Falme za Kiarabu na Qatar. Askofu mkuu Francisco Montecillo Padilla alizaliwa kunako tarehe 17 Septemba 1953 Jijini Cebu, Ufilippini. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 21 Oktoba 1976. Tarehe 1 Aprili 2006 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea na Visiwa vya Solomon. Tarehe 23 Mei 2006 akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu na Kardinali Ricard J. Vidal.

Tarehe 10 Novemba 2011 akateuliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI kuwa Balozi wa Vatican nchini Tanzania! Tarehe 5 Aprili 2016 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi wa Vatican nchini Kuwait na Mwakilishi wa Kitume kwenye Kisiwa cha Kiarabu. Tarehe 26 Aprili 2016 akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Bahrain na Falme za Kiarabu. Tarehe 30 Julai 2016 akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Yemen. Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 6 Mei 2017 akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Qatar. Na hatimaye, tarehe 17 Aprili 2020 akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Guatemala.

Guatemala
17 April 2020, 14:17