Tafuta

Harakati za madaktari nchini Uhispania wakati wa covid-19:Papa Francisko ametuma zawadi ya mashine za kupumulia katika hospitali ya Mtakatifu Rafaeli huko Madrid Harakati za madaktari nchini Uhispania wakati wa covid-19:Papa Francisko ametuma zawadi ya mashine za kupumulia katika hospitali ya Mtakatifu Rafaeli huko Madrid 

Ask.Mkuu Auza atoa shukrani kwa Papa Francisko!

Katika mji mkuu Madrid nchini Hispania,ambao umekuwa kitovu cha janga la Covid-19,Askofu Mkuu Bernardito Auza amekabidhi katika Hospitali ya Mtakatifu Rafaeli mashinde tatu za kupumulia kwenye vyumba mahututi kama zawadi kutoka kwa Papa Francisko kwa jengo hilo,linaloongozwa na shirika la Mtakatifu Yohane wa Mungu.

Na Sr.Angela Rwezaula – Vatican.

Tangu kuenea ghafla kwa janga la virusi vya corona au covid-19 wamesaidia wagonjwa 3000, na miongoni mwao 450 wako katika wadi  na 23 katika vyumba mahututi ambao wanahitaji utunzaji mkubwa, kwa kuzidisha uwezo wa kawaida wa mapokezi. Hii ni  Hospitali ya Mtakatifu Rafaeli huko Madrid,nchini Hispania iliyoanzishwa mnamo 1892, na inasimamiwa na Shirika moja la Kidini la Mtakatifu Yohane wa Mungu,ambalo Papa  ametuma mashine tatu kubwa za kupumulia ili kukabiliana na shida iliyopo kwa sasa  kutokana na virusi vya corona au  Covid- 19.

Alikuwa ni Balozi wa Kitume Askofu Mkuu Bernardito Auza pamoja na Askofu Mkuu wa Madrid, Kardinali Carlos Osoro, waliokabidhi mashine hizo akiwepo Meya wa mji huo mkuu, Bwana José Luis Martínez-Almeida na askofu msaidizi José Cobo. Wakati wa hafla ya kukabidhi Balozi wa Kitume nchini humo, Askofu Mkuu Auza ameelezea ukaribu na upendo mkuu wa Papa Francisko hata wasiwasi wake kwa ajili ya waathirika wa janga hili na zaidi hata matokeo yake hasi,  katika sekta ya uchumi na kijamii ambavyo vitajiwakilisha wakati wa kuanza kwa upya shughuli zao.

Akihojiwa na Vaticannews, Askofu Mkuu  Auza ameonyesha ile furaha yake kubwa na shukrani kwa zawadi ya Papa Francisko. Amesimulia hata ukarimu uliooneshwa katika hospitali hiyo, jengo ambalo limefanya kazi kubwa bila kikomo tangu mwanzo wa mlipuko wa janga la corona katika mji mkuu huo. Hata hivyo hospitli hiyo kimekuwa ndiyo kituo kikuu cha janga la corona nchini Uhispania hata kama kwa sasa amethibitisha kuwa hali inaendelea kuboreka na wakati huo huo mashine za kupumulia hazitoshi. Kwa Askofu Mkuu Auza pia amerudia kutoa shukrani kubwa kwa  Papa kwa sababu amesema amewakumbuka hata wao.

Pamoja na waliopokea mashine hizo alikuwapo  Padre Amador Fernández, Mkuu wa Provinsi ya Castiglia ya Shirika la Mtakatifu Yohane wa Mungu. Naye akizungumza kwa simu amesema ni msaada mkumbwa, na msingi katika wakati huu. Mashine hizo zitawasaidia kuendeleza huduma bora kwa watu ambao kwa wiki zijazo wanaweza kuwa bado wanahitaji msaada huo. Aidha amebainisha kuwa juhudi za wahudumu wote katika hospitali hiyo imewawezesha kuwepo na ni uwepo wa Kanisa. Kadhalika Padre Fernández amekumbusha ni kwa njia zipi kwa haraka katika wiki zilizopita wameweza kuwa na mabadiliko ya kina hasa kwa kutumia nguvu zao zote kuuguza wagonjwa wa virusi vya corona.

 

27 April 2020, 16:26