Tafuta

Vatican News
Tafiti zilizo fanywa wakati wa kufikia kilele cha siku ya wanawake duniani imebainisha kuwa idadi ya nafasi ya uongozi wa wanawake pia Vatican imeongezeka na haijawahi kuwa kubwa kama leo hii. Tafiti zilizo fanywa wakati wa kufikia kilele cha siku ya wanawake duniani imebainisha kuwa idadi ya nafasi ya uongozi wa wanawake pia Vatican imeongezeka na haijawahi kuwa kubwa kama leo hii. 

Wanawake Vatican:Uwepo wa sura ya wanawake Vatican inazidi kuongezeka!

Idadi ya wanawake mjini Vatican imeongezeka siku hadi siku.Mwaka 2019 walikuwa ni 1,016 asilimia 22% ya wafanyakazi wote.Takwimu hii zimethibitishwa na utafiti wa Vatican News kupitia ofisi ya wafanyakazi katika Makao Makuu Vatican kufuatia na maadhimisho ya Kimataifa cha wanawake tarehe 8 Machi.Idadi ya nafasi ya uongozi wa wanawake pia Vatican inathibitishwa kuongezeka na haijawahi kuwa kubwa kama leo hii.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa miaka kumi ya mwisho kuna ongezeko la idadi  kwa asilimia ya wanawake ndani ya ujumla wa wafanyakazi katika huduma ya Papa  makao makuu Vatican. Kunako mwaka 2010 chini ya uongozi wa papa Mstaafu Benedikto XVI , walikuwa wafanyakazi 4.053 ambao kati yao wanawake walikuwa ni 697 karibia asilimia 17 tu. Kinyume chake, kunako mwaka 2019, Makao makuu na Mji wa Vatican kwa ujumla, ulikuwa na wanafanyakazi 4.618 na kati yao  wanawake ni 1.016 ambayo ni asilimia 22%. Kinachoshangaza kwa namna ya pekee ni katika miaka 10 ya mwisho kuwa na ongezeko la wanawake wanaofanya kazi katika Makao Makuu yaani katika Sekretarieti katika vyombo vyake vyote ambavyo vinasaidia Papa katika usimamizi wa Kanisa la ulimwengu. Mwaka 2010 wanawake waliokuwa wanafanya kazi makao makuu walikuwa ni 385, mwaka 2019 walikuwa tayari ni 649, kwa maana hiyo sehemu yao ya jumla ya wafanyakazi wa makao  makuu katika muongo uliopita imepita  kutoka asilimia 17.6 hadi zaidi ya asilimia 24%.

Katika mji wa Vatican kinyume chake ongezeko la wanawake katika muogo umekuwa dhaifu, hasa unatazama sehemu y anafasi duni kama vile wafanyakazi wa mauzo katika majumba ya makumbusho. Isipokuwa katika nafasi ya pekee kunako mwaka 2016 Papa Francusko alimteua mwanahistoria ya sanaa Bi Barbara Jatta kuwa Mkurugenzi wa Jumba la Makumbusho Vatican. Uamuzi huo  ulisababisha hisia katika ulimwengu wa sanaa ya kimataifa, kwa maana  hakuna jumba jingine la makumbusha na lenye ukubwa na umuhimu kuwa  mwanamke kama mshika hatamu ya uongozi. Mkusanyiko wa sanaa za mapapa ni miongoni mwa makumbusho matano yaliyotembelewa zaidi ulimwenguni.

Wanawawake wanne katika nafasi ya juu.Katika makano makuu hasa Papa Francisko amewaweka wanawake wengi katika nafasi ya juu. Kwa ngazi ya juu ambayo mwanamke ameweza kushika nafasi ya juu ni ile ya msaidizi wa katibu Mkuu. Sura ambayo inatokana na timu ya usimamizi wa Baraza la Kipapa lenye kuwa na washiriki watatu hadi wanne. Papa Francisko ameongeza mara mbili makatibu wasaidizi kutoka wawili hadi kufikia wanne. Mwzi Januari 2020 aliyetengazwa wa mwisho katika aina hiyo ni Bi Francesca Di Giovanni Ambaye amekuwa Katibu Msaidizi wa Kitengo cha Mahusianao na Ushirikiano na Nchi na kupewa kazi mpya.

Kunako mwaka 2017 Papa Francisko aliwateua  makatibu wawili ndani ya Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, Bi Gabriella Gambino na  Linda Ghisoni.  Wote wawili ni mama na wenye familia na watoto, haya ni mapya kwa Vatican katika ngazi hizi za uwajibikaji  Mtawa mmoja wa kihispanyola  Carmen Ros Nortes anafanya kazi kama katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na ni mwanamke wa tatu katika nafasi ya kazi hiyo. Aliyekuwa mtangulizi wale alikuwa ni Enrica Rosanna, ambaye alichaguliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kunako mwaka 2004. Ilikuwa ni mshangao mkubwa sana kwa watazamaji wengi kwani hadi wakati huo makatibu wote walikuwa ni makuhani.

Mara tatu katika miaka kumi wanawake wameongezeka: Hata katika Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican, mahali ambapo walei ndiyo wengi kuliko mabaraza mengine ya Vatican, wanawake wawili wanashika nafasi ya uongozi. Hawa ni Natasa Govekar kutoka Slovenia ambaye ni kiongozi mkuu katika Kitengo cha Taalimungu- Kichungaji na Cristiane Murray kutoka Brazil ambaye ni naibu mkurugenzi wa Ofisi ya Waandishi wa Habari Vatican. Mwishoni mwa mwaka 2019 jumla ya wanawake nane na kuongezeka mmoja Francesca Di Giovanni kufanya jumla ya 9 katika nafasi za jukumu fulani Vatican na walio juu ya kiwango cha kumi cha malipo katika Vatican. Miaka kumi iliyopita kulikuwa na watatu tu. Kwa maneno mengine, idadi ya wanawake walio katika nafasi za juu katika Sekretarieti imeongezeka mara tatu katika miaka kumi.

Marais wa Baraza la Kipapa siyo lazima wawe makuhani. Kwa jumla, ofisi tano kati ya ofisi 22 muhimu zaidi za Vatican (Sekretarieti ya Vatican, Sekretarieti ya Uchumi, Mabaraza matatu, Mashirika  tisa, Halmashauri tano, Mahakama tatu sasa wanawake kwenye timu ya usimamizi. Hata hiyo hakuna Papa yoyote aliyewahi kuchagua kiongozi mwanake  kama mkuu  wa Baraza la Kipapa. Na hata marais wa Mabaraza kwa sasa lakini siyo lazima wawe makuhani, na kwa kesi hii umejionesha wazi kama hiyo hata mlei kwa maana hiyo Papa Francisko mwaka 2018 alipomteua mlei Bwana Paulo Ruffini kuwa Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican. Papa Francisko alikuwa amesema hayo wazi juu ya ufunguzi wa mwanamke kushika nafasi ya Usais wa Katibu Mkuu wa Uchumi lakini badaye akachagua kuhani mjesuit Juan Antonio Guerrero Alves aliyeshika nafasi ya Kardinali George Pell.

Papa Francisko ambaye anakaribia kutimiza miaka saba tangu aanze Huduma yake kama kharifa wa mtume Petro siku chache zijazo mara nyingi amethibitisha kuwa Kanisa Katoliki linahitaji wanawake katika nafasi ya uongozi. Katika meneo yake mjini Vatican na katika sekretarieti nzima, kwa hatua anaandaa ardhi hiyo. Licha ya hayo Papa Francisko anasisitiza daima kuwa kuteuliwa tu, haitoshi, wanawawake ni muhimu kwa ngazi ya Kanisa Katoliki. Juu ya hilo anasema lazima kutafakari namna ya kina zaidi. Katika mtazamo huo kwa ujumla kuna  sura ya wafanyakazi wa kike katika Shughuli kipapa za Kimisionari. Kinyume chake inabaki takwimu za Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu. Sehemu zote mbili  hizi ni za Vatican, lakini kila moja ina utawala yake. Japokuwa  takwimu za mwaka wa 2019 zimedhamirishwa na Kusanyiko la Baraza la Uinjilishaji wa Watu ambapo kulingana na takwimu hizi, wanawake 55 wanafanya kazi humo, ambayo ni kama  asilimia 20.4 ya wanawake wote.

09 March 2020, 14:05