Tafuta

Papa Francisko akiwa anapanda ngazi katika uwanja mtupu wa Mtakatifu Petro Ijumaaa tarehe 27 Machi 2020. Papa Francisko akiwa anapanda ngazi katika uwanja mtupu wa Mtakatifu Petro Ijumaaa tarehe 27 Machi 2020. 

Maombi ya Papa Francisko:Ni katika hofu na uchungu wa ulimwengu mzima!

Sala ya Papa Francisko katika uwanja wa Mtakatifu Petro ili janga la virusi vya Corona liishe,imeunganisha watu wengi waamini wa mataifa na wenye mawazo tofauti.Na kwa pamoja wamejikuta wameunganika kwa pamoja na katika mtumbwi mmoja.

Sala ya ukimya katika uwanja ambao ulikuwa kama jangwa, ulijazwa kiroho na waamini na wasio waamini ulimwenguni kote. Ni sala ya ulimwengu ambayo inafanya roho itike njie na maneni ya hofu lakini kwa machozi mengi yasiyoelezeka ya roho hiyo. Hakuna lebo zinazohitajika: Mungu ndiye Baba wa wote. Hofu na maumivu vinaweza kushirikishwa zaidi, lakini wanaweza kuwaunganisha watu tofauti zaidi bila kutarajia. Ndivyo anaandika Bwana Sergio Centofanti makamu mkurugenzi  wa Uhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican kuhusiana na tukio la siku ya tarehe 27 Machi, Sala ya Papa Francisko na baraka ya Urbi et Orbi.

Katika uwanja uliokuwa wazi na mtupu vilisikika vilio vya ubinadamu. Ilionesha vilio vya wasio mjua Mungu, wale ambao hawajali Mungu mbele ya Msulibiwa anayejaa damu, na kilio cha kuomba msaada kutoka kwa watoto karibu na picha ya Mama Maria. Sisi sote tu tofauti lakini inapotokea dhoruba, wote tunapaza sauti tukisema, tunaangamia! Tunajigundua namna hivi tulivyo saw, katika udhaifu wetu hivyo tunavyoshiriki wote hatima ya pamoja kwa sababu tunajikuta katika mtumbwi mmoja kaka, dada na dada wenye imani haba.

Katika kipinid hiki, viwanja vyetu vya alaika viko wazi vinasikiliza tu vilio vinavyosikika mbinguni. Hata Yesu alilia, alilia kwa ajili ya kifo cha rafiki yake. Alilia  mji ambao haukuweza kutambua yule aliyekuwa anaupenda hadi kufikia kutoa maisha kwa ajili yake.  Lakini licha ya dhoruba zetu, bado leo hii anasema “ jipe moyo ni mimi msiwe na hofu”

Anatutia moyo kwa kisema “ Bwana ni mwanga wangu na wokpvu wangu ni mwogope nani? Bwana ni mlinzi wangu je ni mhofu nani? (Zab 27); “katika saa ya hofu yangu nina mtumainia (zab 56). Kwa maana hiyo tunaweza kusali  ewe, Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana; Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.

Kharifa wa kwanza wa Kristo anatuakualika kukabidhi kwa Mungu kila aina ya wasi wasi wetu, kwa sababu Bwana anasikiliza kilio na kututunza. Kwa hakika hata katika Misa ya tarehe 28 Machi 2020 katika Kanisa la Mtakatifu Marta, Papa ameanza na wimbo wa zaburi akisema “Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nalimwita Bwana, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake. ( Za 18)

Katika kitabu cha Ufunuo, Mungu anajionesha kwa watu wake kwa kuonesha ni kitu gani amewahifadhia na kusema:  “Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita “(Uf 21, 3-4).

28 March 2020, 13:55