Vatican News
Ukurasa wa kufunika kitabu cha mahojiano ya Papa Francisko(Rizzoli-Lev)kitabu kinaitwa mimi ninasadiki,sisi tunasadiki Ukurasa wa kufunika kitabu cha mahojiano ya Papa Francisko(Rizzoli-Lev)kitabu kinaitwa mimi ninasadiki,sisi tunasadiki 

Papa Francisko:Kitabu kipya juu ufafanuzi wa Sala ya Nasadiki!

Tangu tarehe 3 Machi 2020 katika duka la vitabu,toleo la tatu la kitabu chenye jina “mimi ninasadiki,sisi tunasadiki”,kimetolewa.Ni ufafanuzi wa Sala ya Nasadiki kwa mujibu wa Papa Francisko katika mahojiano na Padre Marko Pozza msimamizi wa kikanisa cha Magereza na ambapo vitabu viwili vilikuwa tayari vimetolewa vya mahojiano kuhusu sala ya Baba Yetu na Salam Maria.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuanzia tarehe 3 Machi katika duka la vitabu toleo la tatu limetolewa likiwa na jina  “Mimi ninasadiki, sisi tunasadiki”. Ni kitabu kinachotoa tafakari juu ya mizizi ya imani yetu, ambapo Papa Francisko anasimulia kuhusu sala ya ‘Nasadiki’ kwa Padre Marco Pozza msimamizi wa kikanisa cha Magereza la huko Padua nchini Italia. Katika kitabu hili Papa anasema,“mara nyingi tunafikiria kwamba kwa kuhifadhi utamaduni maana yake ni kujenga jumba la makumbusho yenye vitu; na Kanisa linageuka kuwa jumba la makumbusho. Na kumbe “Hapana, kwani “utamaduni huko hai na siyo mkusanyiko wa mambo na ibada zake…ni hai. Utamaduni huo unakua na unapaswa ukue kama mzizi unavyofanya ukue mti na ili baadaye uchanua maua na kutoa  matunda yake”. Papa Francisko anakazia kwamba “Tunapaswa daima kurudi katika utamaduni ili tuweze kuchota ule uzuri wa kina  uzuri, ambao ni kiini  kinachofanya ukue”.

Katika mfululizo wa vitabu ni mwendelezo wa mara baada ya mchakato wa kufafanua sala ya “Baba Yetu” na “Salam Maria”, ambapo vitabu hivyo tayari vinapatikana katika maktaba, na kwa maana hiyo katika toleo hili la tatu ya  mazungumzo kati ya Padre Marco na Papa Francisko yanakabiliana na ukweli wa imani, wa matumaini na upendo ambao unajikita ndani ya ishara ya kizamani ya mitume. Kutokana na hili Papa anasema  ni kutafuta “ maana ya kila siku, ya maisha, au urahisi wa kina, na zaidi ule wa kuwa mwana wa Mungu na urafiki na ndugu wote katika imani na kwa ubinadamu wote”

Kusoma, kuishi, kusali sala ya Nasadiki  maana yake ni kushuhudia imani kwa Mungu Muumba, katika Mwana ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya wokovu wetu, katika roho na katika Kanisa. Hii ina maana ya kutazama kinachotuzunguka na  labda gerezani kama anavyosimulia Padre Marko Pozza katika sehemu ya pili ya kitabu, na kwamba ule ufufuko wa wafu ambao ni jaribio la jumla, maonesho ya ufufuko wa mwisho. Na zaidi ina maana ya kuamini Mungu aliye mgonjwa wa huruma.

Maneno ya Papa yanayogusa kwa kina ni yale ambayo yanatazama na kuona upeo wake wa mwisho wa maisha yake kwani anasema: ninafikiri wakati ule, siku itakapoisha, ya maisha nitakaribia kwa Mungu nikiwa ninavutiwa na uzuri ule, kwa moyo wa unyenyekevu, nikiwa nimeinamisha kichwa; ninawaza ule mkumbatio na mtazamo wangu utakaokuwa unatazamana na wake. Sitoweza lakini kuinua mtazamo wangu kwake. kabla ya kupata mkumbatio kutoka kwake”. Hiki ni kitabu kizuri cha tafakari ya kina kiroho katika maisha hasa ya kwa ajili ya kukiri imani yetu kwa Mungu kama wakristo.

05 March 2020, 12:20