Tafuta

Padre Cantalamessa akiwa katika tafakari ya tatu katika kipindi cha kwaresima ambapo ametazama sura ya Mama Maria chini ya miguu ya msalaba wa Yesu Padre Cantalamessa akiwa katika tafakari ya tatu katika kipindi cha kwaresima ambapo ametazama sura ya Mama Maria chini ya miguu ya msalaba wa Yesu 

Pad.Cantalamessa:Kwaresima:tumaini likisimama kila kitu kinasimama!

Katika tafakari ya tatu ya Kwaresima ambayo imerekodiwa katika Kikanisa cha Redemptoris Mater,Mhubiri Mkuu wa nyumba ya Kipapa anawaalika waamini kutafakari juu ya Maria chini ya miguu ya Msalaba na kuanza ushiriki wa mateso ya Kristo.Maria ni kama mama wa matumaini ambayo ni fadhila na kama oksijeni kwa kila mtu na kwa ajili ya safari ya Kanisa.

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Chini ya Msalaba alikuwapo Mama yake Yesu, dada yake Maria wa Cleofa na Maria Magdala. Haya ni maneno ya Injili ambayo Padre Raniero Cantalamessa amependekeza leo hii tarehe 27 Machi 2020  katika kutafakari kwa ajili ya  Papa na Sekretarieti yote ikiwa ni mchakato wa tafakari ya tatu katika kipindi cha Kwaresima 2020 na ambayo kwa mujibu wa sheria na kanuni za kiafya, tafakari hiyo ilikuwa ni kwa njiaya moja kwa moja kupitia vyombo vya mawasiliano.

Maria hakwepi Kalvari

Maria yuko juu ya Kalvari pamoja na wanawake wengine lakini yeye ni Mama. Aliona mateso makali, na kudhihakiwa kwa Mwanaye na kusulibishwa kwake na kama alivyokuwa wamefanya Yesu kwa watu wote, hata yeye aliombwa asamehe. Katika tafakari hii amethibitisha Padre Cantalamessa  kuwa ikiwa Maria aliweza kujaribiwa kama ilivyokuwa hata kwa Yesu jangwani, kwake yeye Maria tukio lilijitokeza chini ya Msalaba wa Yesu. Ni kishawaishi hiki cha kina kwa Yeye aliyeamini kuwa Yesu alikuwa ni Mwana wa Mungu, lakini akiwa chini ya msalaba analimwona Yesu ambaye hakuweza kufanya lolote ili kujikomboa. Kwa maana hiyo hata Mama Maria alibaki kimya.

Padre Cantalamessa akiendelea na tafakari amethibitisha kwamba kwa kuzungumza kiubinadamu, kulikuwapo na sababu za Maria  hata kuweza kumkaripia Mungu akisema “ulinidanganya!  Au kama alivyopaza sauti siku moja Nabii Yeremiah akisema “ uliniadaa nami nikaadaika! Na angeweza hata kukimbia kutoka juu ya kalvari. Kinyume chake Mama Maria hakukwepa, bali alibaki pale chini ya msalaba kwa ukimya na kwa kufanya hivyo ndipo inajionesha maana maalum ya kuwa mfiadini wa imani, shuhuda wa kweli wa imani katika Mungu na akiwa nyuma ya mwanae.

Kama Maria hata Kanisa

Juu ya Kalvari Mama Maria alikuwa ameungana katika msalaba wa Yesu na alikuwa ndani ya mateso yake, kwa maana hiyo Padre Cantalamessa amebainisha na kutoa: Je ikiwa Maria alikuwa ni picha na kioo cha Kanisa, mwanga wake na mfano wa kuigwa, je ni kitu gani alitaka kuliambia Kanisa kupitia Roho Mtakatifu na kwa kufanya namna ambayo maandishi Matakatifu, yanaelezea uwepo wake karibu na msalaba? Katika kujibu amesema kuwa: “hii ina maana kwamba anatuelezea kile ambacho tunapaswa kufanya kila siku kama waamini katika kuiga, yaani kukaa karibu na Maria chini ya Msalaba wa Yesu na kama alivyobaki Mtume wake aliyekuwa anampenda sana”.

Kukaa karibu ma msalaba wa Yesu

Padre Cantalamessa ameweza kufafanua wazi kwa  kusema kwamba inabidi kutambua  na kutofautisha katika ya karibu na msalaba na kukaa  kando ya msalaba wa Yesu na kwamba hilo ni muhimu. Haitoshi kuelekea katika msalaba, yaani katika mateso bali kukaa hata ndani mwake kwa kimya. Hii utafikiri peke yake ni kitu cha kishujaa na kumbe siyo kitu muhimu. Inawezekana kuwa bure. Lakini jambo msingi ni kukaa karibu na msalaba wa Yesu. Kwa maana  hiyo kinacho hesabika siyo msalaba tu kwa urahisi, bali ni ule msalaba wa Kristo. Siyo suala la kuteseka bali kuamini na kwa namna ya kufananisha na mateso ya Kristo. Katika muktadha huo suala msingi ni imani. Jambo kubwa zaidi la Mama Maria akiwa chini ya msalaba lilikuwa ni imani yake na zaidi tena mateso yake!

Imani inatakasa mateso

Kuamini kiukweli katika msalaba wa Kristo, anasema Padre Cantalamessa ni kuchukua msalaba na kwenda nyuma ya Yesu; na katika ushiriki wa mateso yake siyo kukubali kijuu juu tu bali kuyaishi kwa ari katika muungano na Kristo. Kwa hivyo imani kwa kifupi ni imani katika msalaba wa Kristo ambayo inahitaji kupitia mateso na ili kuwa ya kweli. Na amefafanua kwamba mateso yanaunganisha msalaba wa Kristo kwa njia halisi, na ni aina ya njia yaani na aina ya njia ya msalaba wa Kristo, siyo sawa na imani, lakini ni katika kutengeneza njia moja katika hilo.

Fadhila ya matumaini

Padre Cantalamessa amweza  pia kutoa utangulizi wa matumaini. na katika hili amesema kwamba kwa mujibu wa Injili ya Yohane, anaendeleze tukio la Kalvari, kwamba msalab wa Kristo siyo tu kipindi cha kifo cha Kristo, bali ni utukufu wake na ushindi. Katika hili tayari umekwisha fanyiwa kazi ufufuko. Juu ya Kalvari Maria alishirikishana na Mwanaye  siyo tu kifo lakini hata ukuu wa ufufuko. Sura ya Maria chini ya Msalaba ambayo inamwonesha kuwa ni mwenye huzuni, mwenye kuteswa, analia, kama wimbo wa Stabat  Stabat, yaani  Yeye  peke yake akiwa na huzuni ingekuwa hajakamilika. Juu ya  Kalvari, yeye siyo  Mama wa huzuni tu , bali  pia ni Mama wa tumaini, (Mater spei), kama Kanisa linavyo muomba katika moja ya nyimbo zake. 

Mama wa kila tumaini

Kama Ibrahimu hata Maria chini ya Msalaba aliamini kwa kila hali kuhusu matumaini. Maria aliamini kuwa Mungu alikuwa na uwezo wa kumfufua Mwanaye hata katika wafu na kama yeye, hata Kanisa linaisha ufufuko wa matumaini. Kama Maria alivyokuwa na Mwanaye aliyesulubiwa, ndivyo Kanisa linaitwa kuwa pamoja na wasulibiwa wa leo hii kama vile maskini, wateswa, wanyonge na wanaodharauliwa ili kukaa na tumaini. Haitoshi kuhurumia maumivu yao au hata kujaribu kuipunguza amesisitiza Padre na kwamba hiyo ni kidogo sana. Kila mtu anaweza kufanya hivyo, hata wale ambao hawajui ufufuko. Kanisa lazima litoe tumaini, likitangaza kwamba mateso siyo upumbavu, lakini yana maana, kwa sababu kutakuwa na ufufuo kutoka kwa wafu. "Kanisa lazima litoe sababu ya tumaini lililo ndani yake"

Bila tumaini kila kitu kinasimama

Matumaini ni muhimu na kama okisijeni ya maisha ya kila mtu hata kwa Kanisa, hata kama matumaini kwa kipindi kirefu hadi sasa  imekuwa kati ya fadhila za kitaalimungu, na kama dada mdogo, ndugu masikini. Amesema hayo akitaja mshairi Charles Péguy ambaye anasema imani, matumaini na upendo ni dada watatu, ambao ni wakuu na hata mdogo hadi sasa. Ni lazima kutembea kwa kumshika mkono mtoto ambaye ni tumaini na ndiyo kitovu. Wote tunafikiria kwamba ni watu wakubwa wanaopaswa kuwashika au kubeba mtoto. Huko ni kukosea, anasema mshairi. Ni Mtoto Tumaini ambaye anashikiliwa na dada wengine wawili kwa sababu akisimama Tumaini, kila kitu kinasimama! Kama anavyoshauri Mshairi, Padre Cantalamessa ameongeza kusema,“tunapaswa kugeuka wadau wa mtoto Tumaini.

Kutumaini ni kugundua kuwa bado kuna jambo la kufanya

Kufuatana na mantiki ya  tumaini, Padre  Cantalamessa amesema, inamaanisha kumruhusu Mungu usikate tamaa, kukudanganya hapa, mara nyingi kama anavyotaka na hivyo uruhusu kufanya tendo la tumaini zaidi na kila wakati mgumu zaidi. Tumaini, hata hivyo, anaonya Padre Cantalamessa siyo tabia ya mambo ya ndani tu, lakini pia ni  kuweza kugundua kuwa bado kuna kitu ambacho kinaweza kufanyika. Hata ikiwa inaonesha kuwa hakuna kitu zaidi cha kufanya kwa upande wetu ili kubadili hali ngumu, bado kuna uwezekano na inabaki kuwa kazi kubwa ya kutekeleza, kama vile kutufanya tuwe na shughuli na kuweka mbali zaidi ya mahangaiko kwa kuvumilia hadi mwisho. Hii ndiyo  ilikuwa kazi kubwa ambayo Maria alitimiza, akitumaini, chini ya msalaba na kwa njia hiyo Yeye yuko tayari pia kwa sasa kutusaidia.

Biblia inaonesha mifano mingi ya matumaini

Kwa kuhitimisha Padre Cantalamessa amesema, Biblia inaonyesaha mifano mingi kuhusu matumaini ambayo yanabadilisha majanga zaidi. Kwa mfano Nabii Yeremiah ambaye alitambua upweke wa kina wakati ambao Nabii huyo aliweza kuamua kurudia tumaini kwa kubadili malalamiko kuwa imani na kumtegemea na kusaidiwa na Mungu. Amehitimisha akiwaalika kutazama wimbo wake Maria usemao: “salam Mama wa huruma, Mama wa Mungu Mama wa Msamaha, Mama wa Matumaini na Mama wa Neema, Mama uliyejaa furaha Takatifu, Ee Mama Maria!

27 March 2020, 14:24