Tarehe 27 Machi 2020 Papa Francisko ataongoza sala maalum katika uwanja wa Mtakatifu Petro bila kuwapo na waamini na mwisho atatoa Baraka ya URBI ET ORBI.Wote mnaalikwa kushiriki kiroho. Tarehe 27 Machi 2020 Papa Francisko ataongoza sala maalum katika uwanja wa Mtakatifu Petro bila kuwapo na waamini na mwisho atatoa Baraka ya URBI ET ORBI.Wote mnaalikwa kushiriki kiroho. 

Jinsi gani ya kufuatilia Papa kwa Baraka ya Urbi et Orbi tarehe 27 Machi?

Sala na baraka ya 'Urbi et Orbi' ya Papa Francisko, katika kipindi hiki cha dharura ya virusi vya corona, itatangazwa moja kwa moja kupitia Vyombo vya habari vya Radio Vaticana.Kwa wale wote ambao wanataungana naye na kushiriki kiroho kwa njia ya vyombo vya habari watapokea rehema kamili maalum kwa mujibu wa Hati ya Kitengo cha Kitume cha Kitubio iliyoidhidinishwa hivi karibuni. Saa12.00 kamili jioni majira ya Ulaya wote mnaalikwa.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Kuna matarajio makubwa ya ushiriki wa waamini duniani kote katika muda wa saa 12 jioni masaa ya Ulaya  ambapo Papa Francisko alipendekeza yeye binafsi wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Jumapili iliyopita na kurudia tena kusema wakati wa Katekesi yake jamatano hii.

Ni katika dharura ya virusi vya corona au covid-19 ambayo imeenea duniani kote na ambapo kutokana na janga hili, Papa Francisko ataongoza kwa dhati maombi na Baraka ya 'Urbi et Orbi' kwa dunia nzima. Tukio  hili la kipekee litakalotangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari Vatican News ambao wengi waamini wengi wanatarajiwa kushiriki kikamilifu na Papa Francisko!.  Kwa wale wote ambao wanataungana naye na kushiriki kiroho kwa njia ya vyombo vya habari watapokea  rehema kamili  maalum kwa mujibu wa Hati ya Kitengo cha Kitume cha Kitubio Vatican iliyoidhinishwa hivi karibuni. Ni maombi kwa dunia nzima kumwomba Mungu mwenyezi aweze kusitisha hili janga baya ambalo limeikumba dunia mzima.

Tamko la kwanza kwa wakristo  ambalo alisema papa kwa wote limetimizwa Jumatano tarehe 25 Machi 2020 , kwa kumwomba Mungu mwenyezi kwa njia ya maneno ya Baba Yetu , ikiwa ni sambamba na viongozi wakuu wa Manisa na viongozi wa Jumuiya mbalimbali za Kanisa walishiriki duniani kote.

Tarehe 27 Machi 2020 ndiyo hatua ya pili ya maombi hayo ambapo wakatoliki wot, wakristo wote na watu wenye mapenzi mema duniani wanaombwa saa 12 kamili kuungana kiroho m kwa njia ya vyombo vyote vya habari, radio, lunginga na Papa Francisko ambaye ataongoza wakati huo wa sala ambayo inatarajia kudumu karibu kwa saa limoja, katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican. Uwanja huo utakuwa wazi, kama jinsi yeye mwenyewe alivyotangaza tarehe 22 Machi 2020 baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana.

Maneno ya Papa Francisko alisema: “Tutasikiliza Neno la Mungu, tutainua sala zetu, tutaabudu Sakramenti Takatifu na hatimaye nitatoa Baraka ya Urbi et Orbi, ambapo kutakuwa na fursa ya kupokea rehema kamili.”

Kwa mujibu wa Msemaji wa vyombo vya habari anajulisha kuwa katika fursa hii maalum, katika gate ya kati ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, watawekwa Picha ya Salus Populi Romani yaani ya Bikira Maria Afya wa Waroma na Msalaba.

Baada ya kusikiliza somo la Neno la Mungu, Papa Francisko anatatoa tafakari yake. Sakramenti Takatifu itakuwa umewekwa juu ya altare ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, baadaye itafuata maombi na kuhitimishwa kwa Baraka ya Ekaristi  “Urbi et Orbi”.  Kardinali Angelo Comastri, msimamizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro atasoma kanuni ya Rehema kamili. Katika tovuti ya Radio Vatican unaweza kufuatilia katika lugha ya Kiswahili: https://www.vaticannews.va/sw.html, Kingereza:https://www.vaticannews.va/en.html ; Kiitaliano: https://www.vaticannews.va/it.html

27 March 2020, 10:19