Jitihada za kukuabiliana na maambukizi ya virusi zinafuatwa katika mji wa Vatican Jitihada za kukuabiliana na maambukizi ya virusi zinafuatwa katika mji wa Vatican  

Covid-19:Kesi mbili mpya mjini Vatican:zaidi ya vipimo 170 vimefanyika!

Matokeo ya vipimo vilivyofanyika yamethibitisha uwepo wa maambukizi kwa baadhi ya wanaoishi katika nyumba ya Mtakatifu Marta..Zimechukuliwa hatua zote muhimu japokuwa Papa na wasaidizi wake wa karibu hawahusiki,

VATICAN NEWS

Kesi mpya za maambukizi ya covid.19 mjini Vatican zimegunduliwana. Hayo yamethibitishwa na  Msemaji mkuu wa vyombo vya habari Vatican, Dk, Matteo Bruni ambaye amethibitisha  kuwa katika siku zilizopita katika mantiki ya ukaguzi  wa kitengo cha afya katika  mji wa Vatican, kufuatia na maelekezo juu ya dharura ya virusi vya corona, ameonekana mtu mwingine mwenye maambukizi ya Covid19. Ni afisa mmoja anayeishi katika Nyumba ya Mtakatifu Marta, ambaye ameonesha dalili na ambaye mara moja amejitenga na hatua zote muhimu zimechukuliwa.

"Kwa sasa hali yake ya kiafya sio mbaya sana, lakini kama tahadhari mtu huyo amelazwa katika hospitali ya Roma chini ya uchunguzi, na kwa mawasiliano ya karibu na viongozi wa Kurugenzi ya Afya na Usafi ". amethibitisha. Kufuatia na ushauri huo hatua zilichukuliwa kulingana na protokali za afya zilizowekwa kwa upande wa sehemu zote mbili kuhusu usafi wa mazingira,  yaani mahali pa kazi na makazi ya mhusika aliyeambukizwa na kwa kufuatilia wote ambao amekuwa na mawasiliano katika siku zilizotangulia.

Mamlaka ya afya ilifanya majaribio kwa watu walio karibu na mwenye kuambukizwa  na matokeo yalithibitisha kutokuwepo kwa kesi nyingine kati ya wale wanaoishi katika nyumba ya Mtakatifu Marta, na mmoja aliye chanya  kati ya wafanyakazi wa makao makuu Vatican ambaye alikuwa  anawasiliana karibu  na afisa huyo. Aidha Msemaji mkuu wa vyombo vya habari amesema kuwa "Kama tahadadhi  hatua sahihi za usafi zimepitishwa na vipimo vipya vimekamilika, kwa jumla zaidi ya wafanyakazi wa vatican 170  wakazi wa yumba hiyo. Vipimo  vyote vinaonesha kuwa hasi.

Watu walioathirika na Covid-19hadi sasa  kati ya wafanyakazi wa Vatican  na raia wa Jiji la Vatican wamefikia 6 kwa sasa. “Ninaweza kudhibitisha , nahitimisha Dk, Bruni kwamba "Baba Mtakatifu hajaambukizwa na wala wahudumu wake wa karibu”.

Kutoka Msemaji mkuu wa vyombo vya habari Vatican amethibitisha kwamba bado wanasubiri tena majibu ya vipimo vilivyofanywa kabla ya kutoa taarifa nyingine zaidi na hali halisi kamili  ili tuweze kuwajulisha  kulingana na matokeo na hatua zilizochukuliwa" na kwamba "kwa sasa makazi ya Mtakatifu Marta na ofisi za Katibu wa Vatican ziko salama".

 

28 March 2020, 17:26