Tafuta

Balozi Louis Lèon Boguy Bony kutoka Ivory Coast hivi karibuni amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko. Balozi Louis Lèon Boguy Bony kutoka Ivory Coast hivi karibuni amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko. 

Balozi Louis Lèon Bony awasilisha Hati za Utambulisho kwa Papa!

Balozi Louis Lèon Boguy Bony aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa mwakilishi wa Ivory Coast mjini Vatican, hivi karibuni amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko. Balozi Louis Lèon Boguy Bony alizaliwa tarehe 9 Novemba 1957, huko Paris, nchini Ufaransa. Ameoa na kubahatika kupata watoto wawili. Ni mzoefu katika mausuala ya mahusiano na mafungamano ya kimataifa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni amepokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Louis Lèon Boguy Bony aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa mwakilishi wa Pwani ya Pembe "Ivory Coast" mjini Vatican. Balozi Louis Lèon Boguy Bony alizaliwa tarehe 9 Novemba 1957, huko Paris, nchini Ufaransa. Ameoa na kubahatika kupata watoto wawili. Balozi Bony alijipatia Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Abijan; Shahada ya Uzamivu katika historia, Chuo Kikuu cha Paris na baadaye akajiendelea na hatimaye, kujipatia Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Siasa. Katika maisha yake, amewahi kuwa mkufunzi Chuo Kikuu cha Paris; Mfanyakazi wa UNESCO, Mwandishi wa habari katika magazeti maarufu ya “Jeune Afrique”, “Jeune Afrique Economique” Telex Confidentiel, Paris.

Balozi Louis Lèon Boguy Bony amewahi pia kuwa Mkurugenzi msaidizi wa masuala ya siasa, Umoja wa Mataifa; Wizara ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa; Mkurugenzi mkuu wa mawasiliano Baraza la Mawaziri. Mshauri wa masuala ya ufundi na Umoja wa Ulaya; Mshauri wa Rais na baadaye aliteuliwa kuwa Mshauri wa Masuala ya Diplomasia. Kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2010 aliteuliwa kuwa Balozi wa Pwani ya Pembe "Ivory Coast" nchini Canada. Baadaye aliteuliwa kuwa Mkurigenzi wa Uhusiano wa Uchumi Kimataifa, kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2017.

Pwani ya Pembe

 

26 March 2020, 10:07