Vatican News
Baba Mtakatifu ameteua Mheshimiwa Padre Ildevert Mathurin Mouanga kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Kinkala, Jamhuri ya Congo. Baba Mtakatifu ameteua Mheshimiwa Padre Ildevert Mathurin Mouanga kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Kinkala, Jamhuri ya Congo.  (Vatican Media)

Mh. Pd. Ildevert Mathurin Mounga: Askofu mpya wa Jimbo la Kinkala

Askofu mteule Ildevert Mathurin Mouanga alizaliwa tarehe 27 Mei 1966. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 16 Agosti 1998 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Kati ya mwaka 1998 hadi mwaka 2000 alijipatia uzoefu na mang’amuzi ya shughuli za kichungaji Jimboni Kinkala. Kati ya Mwaka 2000 hadi 2004 alijiendeleza katika Masomo ya Sayansi ya Biblia mjini Roma.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kutaka kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu Louis Portella Mbuyu wa Jimbo Katoliki Kinkala, Jamhuri ya Watu wa Congo. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Mheshimiwa Padre Ildevert Mathurin Mouanga, wa Jimbo Katoliki Kinkala kuwa Askofu mpya. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule alikuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya Kardinali Emile Biayenda, huko Brazzaville. Askofu mteule Ildevert Mathurin Mouanga alizaliwa tarehe 27 Mei 1966.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 16 Agosti 1998 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Kati ya mwaka 1998 hadi mwaka 2000 alijipatia uzoefu na mang’amuzi ya shughuli za kichungaji Jimboni Kinkala. Kati ya Mwaka 2000 hadi 2004 alijiendeleza katika Masomo ya Sayansi ya Maandiko Matakatifu kwenye Taasisi ya Kipapa ya Biblia, Roma na kuanzia maka 2004-2009 akahamia kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana na hatimaye kujipatia Shahada ya Uzamivu katikaTaalimungu ya Maandiko Matakatifu. Kati ya Mwaka 2009-2013 alikuwa ni mlezi na Jaalimu wa Maandiko Matakatifu Seminari kuu ya Kardinali Emile Biayenda, huko mjini Brazzaville. Kuanzia mwaka 2014 hadi uteuzi wake, amekuwa ni Gambera.

Jimbo Katoliki la Kinkala
05 March 2020, 13:19