Tafuta

Vatican News
Maaskofu katika Mkutano kuhusu Mediterane mpaka wa amani huko Bari wakati wa misa katika Kanisa la Mtakatifu Nicola Maaskofu katika Mkutano kuhusu Mediterane mpaka wa amani huko Bari wakati wa misa katika Kanisa la Mtakatifu Nicola 

Kard.Sandri fursa ya Ukulu wa Petro ni ishara ya Utume wa Kanisa!

Mtume Petro,umoja wa Watu wa Mungu na mtindo wa kuongoza na kukuza safari ya Injili ndiyo kiini cha mahubiri ya Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki wakati wa misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Bari mahali ambapo wanamsubiri Papa Francisko kuungana nao siku ya Jumapili tarehe 23 Februari 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Jumamosi tarehe 22 Februari 2020 Kardinali Leonardo Sandri Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki ameadhimisha Misa Takatifu  katika Kanisa  Kuu la Bari mahali ambapo wanapomsubiri Papa Francisko tarehe 23 Februari 2020 kwa maaskofu ambao wamejikita katika Mkutano kuhusu “ Mediterranea Mpaka wa Amani” huko Bari nchini Italia, ulianza tarehe 19 Februari. Ni katika muktadha wa Siku Kuu ya Ukulu wa Mtakatifu Petro mtume, Kardinali Sandri  mejikita kutazama hija ya Papa Paulo VI katika Nchi Takatifu ili kufafanua juu ya siku zilizobarikiwa za Mkutano wa usikivu na sala katika tukio hili. Katika mahuburi yake anasema ni Siku kuu ambayo ni kumshukuru Mungu kwa ajili ya utume wa Mwalimu na mchungaji aliyokabidhwa na Kristo hivyo ni sikukuu ambayo kwa hakika inafungamaishwa kwa njia ya utamaduni wa kiliturujia katika makanisa yote.

Aidha Kardinali Sandri amesema kuwa wachungaji waliounganika hapo Bari wamebeba uchungu, matatizo na uzoefu wa watu mahali wanpotoka, lakini vile vile wanaangzwa na  mwanga wa matumaini kwa upya na upendo mkuu ambao ni mwanga wa ukarimu, taa ya moto unaoangaza  watu waliokombolea hadi kufikia mahali penye usalama kama Neno la Mungu linavyowaelekeza.

Kama Kristo alijitoa mwenyewe, mchungaji hawezi kutokuwa kama Nta ya Mshumaa wa maisha yake yanayomalizika wakati yanawaka kwa kutoa  mwanga wake unaoangaza giza la dunia. Katika Siku kuu ya Ukulu wa Mtakatifu Petro, Mtume ambaye anaunganisha pwani mbili za Mediterania, yaani ile ya Kanisa Kuu la Antiokia, (Uturuki ya sasa) na ya  Mtakatifu Petro, Roma, Kardinali amependa kumwombea Papa Francisko atayaka yewafikia Jumapili tarehe 23 Februari 2020 kwa ajili ya wito wake, utumishi wa kazi yake ya kipapa ili aweze kuendelea kutoa mwanga, matumaini na neema katika kipindi kigumu cha nyati zetu.

Kardinali Sandri hata hivyo kabla ya kuanza mkutano huo kuhusu 'Mediteranea mpaka wa amani' alikuwa amebainisha juu ya kupendezwa na pendekezo la Baraza la Maaskofu kwa kuanzishwa kwa Mkutano kuhusu na kusema kwamba “ bahari yetu isiwe ukuta bali ile kama daraja kwa hali zote za kikristo na siyo kwamba wachungulie katika fukwe tu. Suala hili ni nyeti kwa sababu linawahusisha wachungaji wetu wote wa Makanisa Katoliki na yale ya Mashariki”.  Aidha alisisitiza kwamba “Lengo liwe kweli kama la kuishi kipindi cha usikivu na neema ya utambuzi mkubwa wa matatizo katika eneo la kimediteranea na kwa namna gani ya kuweza kukabiliana hasa kipeo cha kibinadamu cha uhamiaji ambao wanalazimika kuacha ardhi zao na nchi zao ambazo wakati mwingine zimekumbwa na vita, ukosefu wa msimamo, majanga mbalimbali ya tabianchi na umaskini wakati wao wanataka wapate mahali penye amani na usalama”.

22 February 2020, 13:29