Papa Francisko anatarajia kutembelea eneo la Acerra kusini mwa Italia tarehe 24 Mei katika fursa ya kumbukumbu ya mwaka wa 5 wa Wosoa wa Laudato si' Papa Francisko anatarajia kutembelea eneo la Acerra kusini mwa Italia tarehe 24 Mei katika fursa ya kumbukumbu ya mwaka wa 5 wa Wosoa wa Laudato si' 

Ziara ya kichungaji ya Papa huko Acerra Mei 24!

Kutoka kwa msemaji wa vyombo vya habari amethibitisha juu ya ziara ya kichungaji ya Papa Francisko itakayofanyika tarehe 24 Mei 2020 huko Acerra kunini mwa Italia katika fursa ya kumkumbu ya mwaka wa 5 wa Laudato si', ili akutane na watu wanaoishi katika eneo liitwalo ardhi ya moto (Terra dei fuochi)kutokana na uchafuzi wa mazingira.

VATICAN

Ikiwa ni miaka mitano tangu kutangazwa kwa Wosia  wa Kitume wa Laudato Si , unaohusu utunzaji wa mazingira nyumba yetu, Papa Francisko ametumia fursa hiyo kuadhimisha kumbu kumbu tarehe 24 Mei 2020 kwa kutembelea huko Acerra,  Italia na ambapo kiukweli ni katikati ya wilaya hizo zilizochafuliwa kati ya Napoli  na Caserta, ambapo inakumbukwa kunako mwaka 2014 katika kitabu cha mahojiano, Papa alisema kuwa  “ilikuwa tukio la kutekelezwa, ambalo lilinisukuma na tangu wakati huo limeendelea kukua kupitia taarifa, na ufahamu pole pole”.

Kwa mujibu wa Askofu  Antonio Di Donna wa  Acerra, baada ya taarifa hizo amesema “Uwepo wa Papa Francisko katika ardhi zetu na kwa namna ya pekee katika jimbo letu  la Acerra ni neema maalum. Papa anakuja kusikiliza pamoja na maaskofu hasa ya majimbo yaliyoathiriwa zaidi na uchafuzi wa mazingira, mateso ya watu wetu, na kukumbuka Nchi nyingine za moto  Italia”. Aidha amesema: “Ziara hiyo kwa ajili yetu ni tukio la kihistoria ambalo linatujaza furaha, ni kama kudungwa sindano ya uaminifu na tumaini kwa familia, kwa namna ya pekee watoto na vijana walioathiriwa zaidi  na magonjwa” . Kwa uhakika  papa atatoa chachu na kiini kipya cha safari ambayo majimbo katika Baraza ya maaskofu wa Campana wanaendelea kufanya kwa matendo  kwa ajili ya elimu kwa wakristo, watu wazima  na watoto, kuhusu haki, amani na utunzaji wa mazingira”.

Askofu ameongeza kusema “ikiwa ni mwaka wa 5  tangu kutolewa kwa  Wosia wa Laudato si, kwa upande wa Acerra, lakini itakuwa ni kama ushauri na kutathimini hali halisi  na kuongeza bididi katika mapokezi ya Wosia huo wa kinabii. Vile vile askofu amesema kuwa, ziara ya Papa ina tamko la nguvu kwa Taasisi za umma ili hatimaye ukweli uweze kuonekana wa ardhi zao hasa katika kuhakikisha maendeleo ya kweli  ya ardhi yao na kujikita katika matendo hai hasa kuweka kiini cha mwanadamu na maendeleo fungamani inayoendana na wito msingi na asili wa kilimo, kieolojia na utalii, anamaliza Askofu  Di Donna akiwaalika kila mtu aombe kuanzia wakati huu maalum wa neema.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka msemaji wa Vatican, Papa Francisko anatarajia kundoka mapema asubuhi Siku ya Jumapili tarehe 24 Mei 2020 kwenda Acerra; baada ya kupita mji atakutana na Maaskofu, Maparoko, madiwani wa miji ya ardhi ya moto na wawakilishi wa familia ambazo ni waathirika wa uchafuzi wa mazingira; itatuata maadhimisho ya Ekaristi Takatifu katika Uwanja wa Calipari na baadaye Sala ya Malkia wa Mbingu. Baadaye Papa Francisko anatarajia kurudi mjini Vatican.

08 February 2020, 17:50