'Querida Amazonia',Mpendwa Amazonia ni Wosia wa Papa Francisko baada ya Sinodi ya Amazonia,ulioandikwa kama barua ya upendo,unamsaidia msomaji kujua uzuri wa ajabu wa Kanisa na hali halisi ya Amazonia 'Querida Amazonia',Mpendwa Amazonia ni Wosia wa Papa Francisko baada ya Sinodi ya Amazonia,ulioandikwa kama barua ya upendo,unamsaidia msomaji kujua uzuri wa ajabu wa Kanisa na hali halisi ya Amazonia  

Ndoto kubwa za Papa Francisko kwa ajili ya Amazonia!

Mtazamo wa Papa kuhusu Kanda ya Amazonia ni njia za kweli kwa ajili ya ekolojia ya kibindamu ambazo zizingatie maskini,kwa ajili ya kuthamanisha utamaduni na kwa ajili ya Kanisa la Kimisionari lenye uso wa kiamazonia.

Na Andrea Tornielli - Vatican 

Ndoto ni fursa na  muafaka wa kutafuta ukweli. Hata Mungu mara nyingi alichagua kuzungumza katika ndoto. Haya ni maneno yaliyototamkwa na Papa Francisko  Desemba 2018 katika mahubiri ya Mtakatifu Marta kuhusiana na Mtakatifu Yosefu aliyekuwa mwanamme mkimya, na dhati, ambapo unatusaidia kuelewa mtazamo wa Papa kuhusu Amazonia kwa njia ya Wosia baada ya Sinodi. Ndivyo anavyoanza, Profesa Andrea Tornielli, Mkurugenzi wa Uhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican kuhusiana na tangazo la kutolewa kwa  ‘Querida Amazonia’, yaani “Mpendwa Amazonia”, Wosia wa Papa Francisko kuhusu Amazonia.  Profesa  Tornielli anaandika kuwa huu ni Wosia ulioandikwa kama barua ya upendo mahali ambamo kuna wingi mashairi ambayo yanamsaidia msomi kuingia moja kwa moja na kuona uzuri wa ajabu wa Kanisa hilo lakini pia hata majanga yake ya kila siku.

 Je ni kwa nini Askofu wa Roma alipendelea kufanyika kwa Sinodi inayozunguka kanda hiyo peke yake katika thamani ya ulimwengu? Kwa nini Amazonia na hatima yake inatuhusu?   Katika kujibu Prof Tornielli anandika kuwa, kwa kufungua kurasa moja  baada ya nyingine ya Wosia wake, ndimo jibu linapatikana. Awali ya yote  kila kitu kinaunganishwa kwani anasema usawa wa sayari yetu unategemea  hata na afya yenyewe ya Amazonia. Na kwa kuwa utunzaji wa watu na ule wa mazingira hauwezi kamwe kutenganishwa, hivyo hatuwezi kubaki na sintofahamu  na wala uharibifu wa utajiri wa kibinadamu na utamaduni wa watu asilia na wala  kuona sera za kisiasa zinararua na kutaka  kuharibu msitu. Lakini pia kuna jambo jingine linalofanya Amazonia iwe ya ulimwengu. Kwa namna nyingine ni mwendelezo wa hali halisi ambayo inajionesha ya changamoto nyingi zilizo karibu nasi. Matokeo ya uchumi wa utandawazi na mifumo ya kifedha ambayo daima siyo endelevu  katika maisha ya watu na mazingira: Kuishi kati ya watu na tamaduni  zake kwa kina zilizo tofauti; uhamiaji; mahitaji ya kulinda kazi ya uumbaji ambayo iko hatari ya kukosa ukarabati wa majeraha yake.

 Querida Amazonia kama kiongozi wa barua ya upendo wa Papa Francisko Profesa Tornielli anaandika kuwa, unawakilisha awali ya yote changamoto za Kanisa, linalo alikwa kutafuta njia mpya za uinjilishaji, wa kutangaza  moyo wa ujumbe wa kikristo  yaani Kerygma inayofanya Mungu awepo na huruma  ambayo ilimfanya apende ulimwengu sana hadi kumtoa sadaka Mwanae juu ya msalaba. Mtu  katika Amazonia siyo mgonjwa wa kupambana ili kutibu mazingira. Watu asilia wa Amazonia wanapaswa wahifadhiwe na tamaduni na mila zao.  Wao pia wanayo haki hata ya kushuhudiwa Injili. Hawawezi kubaguliwa kwa utume, uchungaji wa Kikanisa ambao unawakilishwa vizuri na sura yao nzuri yenye kuunguzwa na jua  kwa  wale wamisionari wengi wazeee, wenye uwezo wa kupiga kasia kila siku  ili kukutana na makundi ya watu na kupeleka kwao huruma na upendo wa Mungu pamoja na faraja ya Sakramenti inayotoa uhai.

Katika  Wosia wake  Papa Francisko aidha anashuhudia mtazamo mmoja ambao unaingilia na kuzima  mivutano   mingi ya maneno na ambayo iliishia kufikiria kuwa sinodi ilikuwa kama bunge la maoni kuhusu suala la kuweka wakfu wa wanaume waliooa.   Ni suala lililojadiliwa kwa kipindi kirefu na ambacho labda kinawezekana kuendelea hata wakati ujao anabainisha Prof Tornielli . Na hii ni kwamba siyo uhakika wa asili yenyewe ya ukuhani, kama unavyothibitisha Mtaguso wa II wa Vatican. Hata hivyo ni suala ambalo Mfuasi wa Petro, mara baada ya kusali na kutafakari ameamua kujibu bila kutazamia mabadiliko au uwezekano wa  kubadilisha sheria. Kutokana na imani ya kuishi na kwa upyaisho kina wa mchakato wa kimisionari ipo neema ya kuachia nafasi ya matendo ya Mungu na wala siyo katika mikakati ya masoko au kiufundi wa mawasiliano na shinikizo la kidini.

Mpendwa Amazonia, inatualika kuwa na jibu maalum na ujasiri  katika kufikiria kwa upya namna ya kuratibu na utoaji wa huduma ya kikanisa. Kwa kuwaalika wahusika wa Jumuiya nzima Katoliki Papa anawaonyesha kuhusu majerha ya watu wale na matatizo ya jumuiya nzima ya kutokuweza kuadhimisha Ekaristi wakati wa Dominika. Kwa maana hiyo anaomba wajibu wa ukarimu hasa  kuwatuma wamisonari wapya, kuthamanisha karama za wote na kuchuchumalia huduma mpya zaidi na huduma ya walei kwa maana anatambua pia mchango mkubwa walei na wanawake. Kwa kkutazama zaidi mchango wa dhati wa watu hawa, Papa Francisko anakumbusha kuwa imani  katika Amazonia, imeoneshwa na kuendelewa uhai wake, shukrani kwa uwepo wa wanawake wenye nguvu na ujasiri bila kupitia kuhani yoyote katika maeneo hayo.

PROF.TORNIELLI
12 February 2020, 12:05