Tafuta

Vatican News
mamia elfu ya vifuniko vya uso vimetumwa nchini China,shughuli iliyoanzishwa na mfu wa kitume wa Papa na kituo cha kimisionari cha Kanisa la China nchini Italia na ushirikiano wa duka la madawa Vatican mamia elfu ya vifuniko vya uso vimetumwa nchini China,shughuli iliyoanzishwa na mfu wa kitume wa Papa na kituo cha kimisionari cha Kanisa la China nchini Italia na ushirikiano wa duka la madawa Vatican  

Vatican imetuma vifuniko vya uso nchini China kuzuia uenezi wa virus vya corona!

Kwa mujibu wa ofisi ya vyombo vya habari Vatican imeeleza kwamba Vatican imetuma nchini China mamia elfu ya vifunika uso kwa ajili ya kuzuia kuenea kwa virus vya corona.

Kutoka Vatican wametuma nchini China mamia elfu ya vifunika uso kwa ajili ya kusaidia watu kuzuia uenezi wa virus  vya corona. Kwa mujibu wa ofisi ya habari Vatican, inathibitisha kuwa vifunika uso hivyo vimetumwa katika wilaya za Hubei, Zhejiang na Fujian.

Hii ni shughuli iliyoongezwa katika Mfuko wa Sadaka ya Kitume pamoja na Kituo cha Kimisionari cha Kanisa la China kilichopo Italia, kwa ushirikiano na Duka la Madawa la Vatican.

03 February 2020, 15:19