Uteuzi wa Washauri wa Tume ya Mahusiano ya Kidini na Waislam!
VATICAN
Papa Francisko amewateua washauri wa Tume kwa ajili ya Uhusiano wa Kidini na Waislam wafautao: katoka Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini ni Padre Joseph Olawale OGUNDIPE, wa jimbo katoliki la Oyo (Nigeria); Padri Laurent BASANESE, S.I. (Francia), Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Kidini ya Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, Roma; Padre Heru PRAKOSA, S.I. (Indonesia), Mshauri kwa ajili ya Majadiliano na Uislam kutoka katika Ofisi ya Katibu kwa ajili ya Uekumene na Majadiliano ya Kidini kwa Wajesuit, Profesa wa Kitengo cha Taalimungu katika Chuo Kikuu cha Sanata Dharma cha Jogyakarta; Dk. Martino DIEZ, Mtafiti wa lugha na maandiko ya kiarabu wa Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu cha Milano na Mkurugenzi wa Kisayansi wa Mfuko wa Kimataifa wa Oasis (Italia); Dk. Timo GÜZELMANSUR, Mkurugenzi wa Christlich-Islamische Begegnungs-und Dokumentationsstelle CIBEDO wa Francofurt (Shirikisho la Ujerumani); Dk. Gabriel SAID REYNOLDS, Profesa wa Mafunzo ya Kiislam na Taalimungu katika Chuo Kikuu cha Notre Dame (Mama yetu) nchini Marekani.