Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 23 Februari 2019 amefanya hija ya kitume Jimbo kuu la Bari-Bitonto, Kusini mwa Italia. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 23 Februari 2019 amefanya hija ya kitume Jimbo kuu la Bari-Bitonto, Kusini mwa Italia. 

Jimbo kuu la Bari-Bitonto: Mji wa Kuombea Amani Duniani!

Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili tarehe 23 Februari 2020 amerejea Jimbo kuu la Bari, mji wenye ukarimu na unaowakutanisha watu kutoka sehemu mbali mbali za dunia kama sehemu ya mchakato wa majadiliano.. Jimbo la Bari-Bitonto linaendelea kujenga historia ya kuwakutanisha viongozi wa Kanisa kutoka Mashariki na Magharibi kwa ajili ya kuombea amani duniani.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Askofu mkuu Francesco Cacucci wa Jimbo kuu la Bari-Bitonto, lililoko nchini Italia, amemshukuru na kumpongeza Baba Mtakatifu Francisko ambaye kwa mara nyingine tena, Jumapili tarehe 23 Februari 2020 amerejea Jimbo kuu la Bari-Bitonto mji wenye ukarimu na unaowakutanisha watu kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Jimbo la Bari-Bitonto linaendelea kujenga historia ya kuwakutanisha viongozi wa Kanisa kutoka Mashariki na Magharibi kwa ajili ya kuombea amani duniani.

Askofu mkuu Francesco Cacucci ametambua uwepo wa Rais Sergio Mattarella wa Italia pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali na kidini. Masalia ya Mtakatifu Nicholaus wa Bari yamekuwa ni kiungo muhimu sana cha waamini wa Makanisa mbali mbali ya Kikristo. Jimbo kuu la Bari-Bitonto linayo furaha kubwa kwa sababu limewezeshwa kuwa ni mji wa amani na kwamba, wanatamani na hii ndiyo sala yao kwamba, amani iweze kutawala duniani kote!

Askofu mkuu Cacucci

 

23 February 2020, 14:17