Tafuta

Vatican News
Mwezi Oktoba 2022 itafanyika Sinodi ya XVI ya Maaskofu kwa mujibu wa taarifa kutoka  Mkutano wa Sekretarieti ya Sinodi iliyofanyika tarehe 6-7 Februari 2020. Mwezi Oktoba 2022 itafanyika Sinodi ya XVI ya Maaskofu kwa mujibu wa taarifa kutoka Mkutano wa Sekretarieti ya Sinodi iliyofanyika tarehe 6-7 Februari 2020.  (AFP or licensors)

Papa:Sinodi ya maaskofu ijayo itakuwa Oktoba 2022!

Mwezi Oktoba 2022 itafanyika Sinodi ya XVI ya Maaskofu.Papa Francisko ameamua hivyo wakati wa Mkutano wa Sekretarieti ya Sinodi iliyofanyika tarehe 6-7 Februari 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Sonodi ya Maaskofu ijayo inatafanyika kunako mwaka 2022 ambapo taarifa zimetolewa mapema kwa ajili ya kutaka kuhakikisha utekelezaji wa Kanisa lote katika maandalizi na katika maadhimisho ya tukio hilo. Ni uamuzi wa Papa Francisko ambaye aliudhuria kikao cha mchana tarehe 6 Februari wakati wa Mkutano wa XV wa Baraza la Sekretarieti kuu ya Sinodi ya Maaskofu. Aliyetangaza tukio  hili ni Katibu wa wa Baraza hilo, Kardinali Baldisseri.

Mada za siku

Katika kazi ya mkutano wa Sekretarieti  ya sinodi ya Maaskofu ulioendelea hata siku ya tarehe 7 Februari 2020 wameuandaa kwa kufuata mapendekezo ya Papa Francisko kuhusu mada za kuweza kukabilinana nazo wakati wa Sinodi ijayo ya XVI ya Maaskofu pia kukabiliana na masuala  ambayo yametimizwa baada ya Sinodi kuhusu vijana iliy fanyika 2018 hata yatokanayo na Wosia wa Kitume wa “Christus vivit” baada ya Sonodi hiyo.

Kusaidia wahamiaji

Papa Francikso aidha ameweza kuwakilisha hata mawazo ya uwezekano wa mada ya Sinodi ijayo ambayo bado iko kwenye mchakato wa mwisho.  Vile vile katika mjadala wao wa mchana huo wamejikita katika kutazama dharura ya mshikamano kwa ndugu, kaka na dada ambao wamekumbwa katika janga la uhamiaji wa kulazimisha

Kazi ya mkutano

Mwanzoni mwa ufunguzi wa mkutano huo Katibu Mkuu Kardinali Lorenzo Baldisseri, amebainisha kwamba, kufuatia na kutangazwa kwa Kardinali Luis Antonio Tagle kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Unjilishaji wa watu, nafasi yake imewekwa Kardinali Joseph Coutts, Askofu Mkuu wa Karachi, nchini  Pakistan. Katika taarifa amebainisha kuwa, Baba wa Sinodi  kutoka Asia ndiye aliye nyakua kura nyingi. Kwa maana hiyo Kardinali Baldisseri  baada ya kutangaza hilo aliendelea kuwakilisha matokeo  juu ya mada ambazo zinaweza kukabiliwa katika kipindi chote cha  mwaka 2019, ambapo kumefanyika   mabaraza ya maaskofu, Sinodi za makanisa Katoliki ya Mashariki kuhusu iuris, Mabaraza ya Kipapa Katoliki na Umoja wa Mama wakuu wa mashirika. Na pia kubainisha kwamba kuhusiana na hiyo  wameweza kuwa na mjadala wenye nguvu zaidi, iwe  katika mkutano, pia hata katika makundi kufuatia na lugha. Aidha siku iliyofuata Kardinali Kevin Joseph Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha aliweza kuonesha  shughuli zao baada ya Sinodi inayopelekwa mbele na vijana kwenye  matendo dhati kuhusu Wosia wa Kitume Christus vivit baada ya Sinodi

15 February 2020, 14:00