Tafuta

Vatican News
Papa amekutana na wanadiplomasia kutoka nchini Azerbaijan Papa amekutana na wanadiplomasia kutoka nchini Azerbaijan  (ANSA)

Papa Francisko amekutana na Rais wa Azerbaijan!

Mazungumzo ya kiutamaduni na kidini ni kati ya mada zilizoguswa katika mkutano na Papa Francisko na Rais Ilham Aliyev, wa Jamhuri ya nchi ya Azerbaijan mjini Vatican.

VATICAN

Tarehe 22 Februari 2020  Papa Francisko na amekutana na Rais Ilham Aliyev, wa Jamhuri ya nchi ya  Azerbaijan mjini Vatican ambapo mara baada ya mkutano huo, amekutana pia na Katibu wa Vatican  Kardinali Pietro Parolin akiambata na  Katibu wa Mahusiano na Ushirikiano na nchi za Nje Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher.

Kwa mujibu wa  msemaji wa vyombo vya habari Vatican wanathibitisha kuwa katika mazungumzo yao na Katibu wa Vatican kwa  sehemu zote mbili  wamoneshwa kupendwa na maendeleo ya uhusiano wao kwa namna ya pekee suala la ushirikiano katika mantiki ya utamaduni na kupongezwa kwa shughuli zitolewazo na  Kanisa Katoliki katika nchi hiyo.

Katika mantiki nyingine zilizoguswa kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican  ni kuhusiana na masuala ya kikanda na kimataifa hasa juu ya umuhimu wa majadiliano ya kiutamaduni na kidini ili kukuza amani kati ya makundi tofauti ya kidini na kikabila.

22 February 2020, 14:12