Tafuta

Vatican News
Mwenye Carlo Acutis na  Padre Rutilio Grande ni kati ya wale ambao hivi karibuni watatangazwa watakatifu Mwenye Carlo Acutis na Padre Rutilio Grande ni kati ya wale ambao hivi karibuni watatangazwa watakatifu 

Papa ameridhia kutangazwa kwa watakatifu wapya wa Kanisa!

Papa Francisko ameridhia Baraza la Kipapa la kuwatangaza watakatifu wapya wa Kanisa.Kati watakao tangazwa wapo walei wawili waliouwawa huko Salavodor.Watatangazwa wafidini wa India na sista Maria Franciska wa Yesu mwanzilishi wa Shirika la Watawa wakapuchini wa Loano pia kijana Carlo Acutis wa Italia na Padre Rutilio Grande García Mjesuit.

VATICAN

Mtumishi wa Mungu Carlo Acutis, alizaliwa tarehe 3 Mei  1991 London na kifo chake  12 Oktoba 2006  huko Monza. Huyu ni kati ya watakatifu ambao watatangazwa hivi karibuni kwa mujibu wa taarifa ya vyombo vya habari Vatican, ambapo Kardinali Angelo Becciu, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu amekutana na Papa Francisko tarehe 21 Februari 2020. Wakati wa Mkutano huo, Papa ameridhia kuwatangaza wengine kufuatana na miujiza ya maombezi ya menyeheri Beato Lazzaro, kwa jina maarufu  Devasahayam, mlei na mfiadini, alizaliwa tarehe 23 Aprili 1712 katika kijiji cha Nattalam (India) na kuwawa kwa chuki ya imani yake huko Aralvaimozhy (India), tarehe  14 1752;

Miujiza kwa maombezi ya Sista Maria Maria Francesca wa Yesu, Mwanzilishi wa Shirika la Watawa wa Kapuchini wa  Loano. Alizaliwa huko Carmagnola tarehe 14 Februari 1844,  na kifo chake Montevideo (Uruguay) tarehe 6 Agosti  1904; Wafiadini, watumishi wa Mungu Rutilio Grande García, Padre Mjesuit na wenzake wawili 2 walei waliouwawa huko El Salvador, kwa sababu ya chuki ya imani yao kunako tarehe 12 Machi 1977; Utambuzi wa fadhila za Mtumishi wa Mungu Emilio Venturini, padre wa Jimbo na mwanzilishi wa Shirika wa watawa wa kike waitwao 'watumishi waambuduo'. Alizaliwa huko Chioggia  kunako 1842 na kifo chake tarehe Mosi Desemba 1905.

Fadhila  za Mtumishi wa Mungu Pirro Scavizzi, Padre wa kijimbo. Alizaliwa huko Gubbio kunako tarehe 31 Machi 1884 na kifo chake huko Roma tarehe 9 Septemba 1964. Fadhila za Mtumishi wa Mungu Emilio Recchia, Padre wa shirika la Madonda ya Bwana wetu Yesu Kristo aliyezaliwa huko Verona,  Italia kunako tarehe 18 Februari 1888 na kifo chake tarehe 27 Juni 1969; Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Mario Hiriart Pulido, Mlei .aliyezaliwa huko Santiago ya Chile (Cile)  tarehe 23 Julai  1931 na kifo chake huko Milwaukee Marekani, kunako  tarehe 15 Julai 1964.

22 February 2020, 14:56