Tafuta

Vatican News
Baba Francisko amekutana na Kiongozi Mkuu wa Papa Bosnia na Erzegovina na ujumbe wake wote Baba Francisko amekutana na Kiongozi Mkuu wa Papa Bosnia na Erzegovina na ujumbe wake wote  (ANSA)

Papa amekutana na Rais aliyeko madarakani wa Bosnia-Erzegovina!

Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican amethibitisha kuwa Papa Francisko amekutana na Bwana Željko Komšić, Rais aliyeko katika zamu ya Urais wa chi za Bosnia na Erzegovina.

Katika nyumba ya kitume ya mjini Vatican tarehe 15 Februari 2020, Papa Francisko  amekutana na Bwana Željko Komšić, Rais aliyeko katika zamu ya Urais wa chi za Bosnia na Erzegovina. Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican amethibitisha kuwa mara  baada ya mkutano huo pia amekutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akisindikizwa na monsinyo Miroslaw Wachowski, Katibu msaidizi wa Vatican wa Mahusiano na ushirikiano na nchi za nje.

Katika mazungumzo yake na Katibu wa Vatican, yameonesha uwepo wa mahusiano mema baina na nchi hizi mbili kwa namna ya pekee kwa ndani ya nchi juu ya umakini wa hali halisi ya jumuiya Katoliki.  

Katika mazungumzo yao pia wamebainisha juu ya ulazima wa kuhakikisha kuheshimu haki wazalendo wote   hasa katika usawa wa watu wa aina tatu wanaoijumuisha nchi hizo. Hatimaye wamegusia baadhi ya mada zinazotazama mantiki ya kimataifa na kikanda ikiwa ni amani na usalama, mahitaji ya kukuza michango ya majadiliano ili kukabiliana na changamoto za nchi hizo za Mashariki na matarajio ya Kanda hiyo kujipanua ndani ya Umoja wa Ulaya

15 February 2020, 14:44