Tafuta

Vatican News
Papa amemteua Padre Flavio Pace kuwa katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki Papa amemteua Padre Flavio Pace kuwa katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki  

Padre Pace ni katibu mpya msaidizi wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki!

Padre Flavio Pace mwenye umri wa miaka 42 wa Jimbo Kuu Katoliki la Milano Italia ameteuliwa na Papa Francisko tarehe 3 Februari 2020 akiwa tayari ndani ya Baraza la Kipapa ambalo amekuwa akitoa huduma yake.

VATICAN

Papa Francisko amemteua Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki Padre Flavio Pace,ambaye alikuwa tayari anatoa huduma katika ofisi hiyo.

Padre Flavio alizaliwa huko Monza Italia kunako tarehe 29 luglio 1977 na kujiunga na Seminari ndogo kunako mwaka 1996. Alipata daraja la Ushemasi kunako 2001 na Upadre 2002. Shughuli zake za kichungaji kama Paroko msaidizi wa  Abbiategrasso, katika kutoa huduma ya kichungaji kwa vijana na kufundisha dini katika Shule ya taifa na  kama msimamizi wa Kanisa dogo la Hospitali.

Majiundo mengine zaidi ni masomo ya  kiislam katika Taasisi ya Kipapa la Mafunzo ya Kiarabu na Kiislam huko Roma 2010, na wakati huo huo akishirikiana na baadhi ya shughuli mbalimbali za mahusiano ya kiislam na Jimbo Kuu la Milano. Amekuwa katika Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki tangu 2011  pia kuwa msimamizi wa moja ya  kanisa dogo la  watawa, Roma.

03 February 2020, 15:01