Tafuta

Nia ya za maombi ya Papa kwa mwezi wa Februari 2020 ni kusikiliza kilio cha wahamiaji Nia ya za maombi ya Papa kwa mwezi wa Februari 2020 ni kusikiliza kilio cha wahamiaji 

Nia za maombi ya Papa mwezi Februari 2020 ni kusikiliza kilio cha wahamiaji!

Kama kila mwezi,Papa Francisko anatoa ujumbe kwa njia ya video ambapo kwa mwezi wa Februari 2020 nia ya Maombi ya Papa ni kusikiliza kilio cha wahamiaji.

Vatican

Papa Francisko kwa maana hiyo katika ujumbe wake kwa njia ya video amesema, "Wahamiaji mara nyingi ni wahanga wa biashara haramu ya binadamu. Kati ya sababu nyingi, hii inatokea kwa sababu ya utoaji rushwa upande wa watu ambao wapo tayari kufanya kitu chochote kwa madhumuni ya kujipatia fedha".

Aidha amesema "fedha zinazotokana na biashara chafu na ya udanganyifu ni fedha ya usaliti". Sitii chumvi", amesisitiza na kwamba " ni fedha ya usaliti".  Kwa kuhitimisha amesema, "Tunaomba ili kilio cha kaka na dada zetu wahamiaji, wahanga wa rushwa  na uhalifu wa biashara ya binadamu, kiweze kusikika na kuangaliwa".

06 February 2020, 17:12