Tafuta

Vatican News
Ilikuwa ni tarehe 4 Februari 2019 wakati wa Mkutano wa kidini ambapo Papa Francisko na Imam di Al-Azhar walitia sahihi katika Hati ya Udugu wa Kibinadamu huko  Abu Dhabi. Ilikuwa ni tarehe 4 Februari 2019 wakati wa Mkutano wa kidini ambapo Papa Francisko na Imam di Al-Azhar walitia sahihi katika Hati ya Udugu wa Kibinadamu huko Abu Dhabi.  (AFP or licensors)

Ni mwaka mmoja baada ya sahihi ya Hati ya Udugu Kibinadamu!

Ilikuwa ni tarehe 4 februari 2019,Papa Francisko na Imam di Al-Azhar walitia sahihi katika Hati ya Udugu wa Kibinadamu huko Abu Dhabi.Huu ni mwaliko wa nguvu wa kugundua kwa upya udugu ili kuhamasisha pamoja haki na amani,kuhakikisha haki za kibinadamu na uhuru wa kidini.Tutazame mambo muhimu ya kuzingatia katika hati hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 4 februari  2019, Papa Francisko  na Imam di Al-Azhar walitia sahihi katika Hati ya Udugu wa Kibinadamu huko  Abu Dhabi,  wakiwa wanatoa mwaliko wa nguvu wa kujigunduwa kwa upya na kuhamasisha pamoja haki na amani, kuhakikisha haki za kibinadamu na uhuru wa kidini.  Baadhi ya masuala muhimu katika hati hiyo ni kwamba “Hati ya Udugu wa Kibinadamu, iliyotiwa sahaii ni mwaliko kwa waamini wa dini zote  duniani, kuungana na kushikamana, ili kufanya kazi katika umoja na udugu, katika kujenga na kudumisha misingi ya haki, amani na mapatano kati ya watu.

Kukumbatia haki, ukweli na uwazi

Hati hii inataka watu wote wakumbutie kwa hakika ukweli na uwazi ili hatimaye kudumisha amani duniani! Licha ya tofauti zao msingi zilizopo Hati hii inawataka waamini wawe na ujasiri wa kushirikiana na kushikamana kwa ajili ya huduma kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Hati hii inawataka  waamini wote kila pembe  za dunia na kila mantiki katika kujikita kutenda mema; kuendeleza na kudumisha majadiliano ya kidini; kwa kuheshimiana na kuthaminiana kama ndugu wamoja.

Hati inaonesha kujenga mazingira ya kuishi

Katika hati hiyo pia inaonesh ni kwa jinsi gani ya kujenga mazingira yatakayowawezesha watu kuishi katika ulimwengu unaosimika mizizi yake  katika haki, upendo na mshikamano.  Kwa kufanya hivyo inawezekana kabisa kuondoa kufuru kwa njia ya kutumia jina la Mungu kwa mafano binafsi. Na zaidi ni katika kutafuta mema ili kuondokana na kuanzisha vita, ghasia, chuki na migongano ya kijamii.

Kulinda familia na maisha

Katika hati hiyo viongozi wanakumbusha jinsi gani familia ilivyo muhimu na kuheshimi maisha. Kupinga vikali na kuhumu mitindo yote inayotishia maisha kama vile kuua , matendo ya kigaidi, kufukuza kwa kulazimisha , biashara aramu ya kibinadamu, utoaji mimba, euthanasia na sera za kisiasa zinazoungwa mkono mambo hayo.

Uhuru wa kidini

Katika hati hiyo inasema haki ni msingi wa kila mtu  na kila mtu lazima afaidike kwa uhuru wa imani na mawazo. Wingi wa dini, utofauti wa dini, rangi, kabila na lugha ni hekima ya Mungu. Kwa maana hiyo wanalaani vikali tendo la kulazimisha watu wakubali dini nyingine kwa nguvu au kulazimisha utamaduni na mtindo wa ustaarabu wa wengine kwa nguvu.

Ubaguzi dhidi ya walio wachache

Hati hiyo pia inathibitisha kwamba kuna ulazima wa kuwa na msimamo katika jamii zwtu kwa mantiki ya uzalendo na kukataa kila aina ya matumizi ya ubaguzi kwa kile kiitwachio uchache na ambao unapelekea mbegu za kuhisi upekwe na kudharauliwa.

Utambuzi wa haki  ya mwanamke

Katika hati hiyo pia ni muhimu wa utambuzi wa haki ya mwanamke katika elimu, kazi, zoezi la haki za kisiasa, kwa kutafuta kumkomba dhidi ya mikandamizo ya kihistoria,na kijamii kinyume na misingi ya imani na hadhi yake.

Elimu katika ngazi za mashule ya vyuo vikuu

Hatimaye kuna swali moja ambalo Hati hiyo imekuwa ni sababu ya kutafuta na kutafakari katika mashule yote, vyuo vikuu, taasisi za elimu na mafunzo na kuwa kama ishara ya mkono wa kupokea kati ya Nchi za Mashariki na magharibi,  Kaskazini na Kusini.

03 February 2020, 17:12