Tafuta

Vatican News
Kardinali Konrad Krajewski Msimamizi wa Sadaka ya Papa amezindua nyumba ya kulala watu wasio na makanizi huko Calabria nchini Italia Kardinali Konrad Krajewski Msimamizi wa Sadaka ya Papa amezindua nyumba ya kulala watu wasio na makanizi huko Calabria nchini Italia  

Krajewski huko Calabria amezindua nyumba ya maskini ya kulala!

Imekuwa siku nzima kwa ajili ya maskini wa Praia karibu na bahari kwenye en eo karibu na fukwe zaCosenza. Ndiyo shughuli ambayo tarehe 1 Februari Kardinali Konrad Krajewski, Msimamizi wa Sadaka ya Kitume amejikita nayo kwenye Parokia ya Mtakatifu Paulo Mtume na kupeleka msaada na ukaribu wa Papa Francisko.Amezindua pia nyumba ya kulala ya Rut yenye vitanda 13.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Padre Marco Avenà, mwenye umri wa miaka 35 na Paroko wa Kanisa la Praia karibu na bahari huko Cosenza nchini Italia amezungumza na Vatican News, kueleza hali  halisi  ya ugeni kwamba ugeni huo “ni kama kutiwa  muhuri kwenye kazi yetu na  ishara ya ukaribu mkubwa na baraka tele kwa kutembelewa katika parokia yake na Kardinali Konrad Krajewski msimamizi wa Sadaka ya Kitume Vatican. Hata hivyo hii ni siku ambayo Msimamizi wa Sadaka ya Papa ameichagua kutembelea huko Calabria  na kukabiliana na safari ndefu kwa gari, lakini yenye shauku ya kupelekea kwa hakika mkono mwema wa msaada wa Papa Francisko  katika Jumuiya hiyo.

Zana nyingine za kusaidia hata chakula

Katika sanduku la mizigo kwenye gari lake kulikuwapo na vitu vingi ambavyo ni muhimi kuanzia na chakula kama ambavyo yeye na kundi zima mjini Vatican wanafanya wakizungukia maeneo mbali mbali usiku wa kila Jumanne na Alhamisi kuwapatia chakula watu wasio kuwa na makazi na maskini, kwa njia hiyo ni shughuli yake ya kipindi kirefu. Aidha amepeleka hata rosari alizopewa na Papa. Rosari zitaweza kukabidhiwa na kufanyiwa kama hija ya mmoja kwa moja na ambaye taweza kuchukua rosari hiyo anaweza kusali masaa 24, kwa ajili ya Kanisa, kwa ajili ya Papa na wale wote wenye kuhitaji msaada katika dunia nzima, na kumkabidhi mwingine kwenye mikononi ili kama anataka aendelee hivyo hivyo.

Nyumba ya Rut

Kardinali  Krajewski mchana baada ya kupokelewa na Askofu wa Leonardo Bonanno wa Mtakatifu Marco Argentano – Scalea, na viongozi wa eneo hilo amebariki nyumba ya Rut a mahali pa kulala watu 13, iliyoandlaiwa kwa msaada wa fedha za Caritas ya Italia na chama cha “otto per mille”. Saa 12.00 jioni  ameadhimisha Misa na baada ya misa amepata mlo pamoja na watu zaidi ya 30 wanaosaidia Padre Marko katika utekelezaji wa chakula na kuandaa Parokia. Na hii kila mara baada ya chakula, lazima kuondoa kila kitu kwa ajili ya katekisimu na hali halisi nyingine ya kiparokia. Padre Marko amesema kwa sasa kuna maskini 5 wanaoishi hapo. Licha ya hayo Padre Marko amesema kuna watu ambao wanaishi hapo kwa miaka sasa miwili ndani ya  roulotte.

Msaada ni wa bure

Maskini wanawatia moyo katika wito wao anasema Padre Marko hasa kukaa nao karibu kwa maanaanagusa kweli uwepo wa Kristo karibu. Na wakati mwingine anasema kuna ugumu na hasa kwa wale ambao labda usiku walikuwa wanatoroka, na kumsababishia naye atoke usiku ili aweze labda kuzuia kama mtu huyo alikuwa anataka kuingia katika njia mbaya. Upendo na hisani unafanyika bure  kwa maana imetokea hasa wengine kuondoka bila kusema asante. Na hiyo ndiyo Injili. Ni kusaidia bila kusubiri lolote la kubadilishana na thawabu zaidi itatolewa na Bwana na ndiyo baraka sasa inajionesha kwa jitihada za watu wa kujitolea familia nzima ambazo zinajitoa bure kusaidia wengine. Upendo unaambukiza kidogo na kubadili hisia za wengi. Upendo unabadilisha moyo mahali ambayo kuna hisia za kutoaminiana na ambazo zimejaa katika maeneo mengi, upendo unafungua mlango na kusaidia wanaoteseka na mateso na uchungu amesema.

01 February 2020, 18:55