Tarehe 5 Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Agata mfiadini. Kardinali Sandri Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki ameongoza misa katika Kanisa Kuu Catania Tarehe 5 Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Agata mfiadini. Kardinali Sandri Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki ameongoza misa katika Kanisa Kuu Catania 

Kard.Sandri:Jamii ilinde nafasi ya wanawake wasiruhusu kamwe kubezwa!

Jamii ihakikishe kulinda nafasi ya wanawake na wasiruhusu hata wimbo mmoja uweze kukiuka hadhi ya wanawake kwa lugha chafu na zisizo na adhabu.Amesema hayo Kardinali Sandri Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki wakati wa mahubiri kwenye Kanisa Kuu la Catania wakati wa maadhimisho ya Siku kuu ya Mtakatifu Agata mfiadini tarehe 5 Februari 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jamii yetu inapaswa kukesha na kulinda nafasi msingi ya wanawake, na wala isirihusu hata wimbo mmoja uweze kukiuka hadhi yake kwa lugha chafu au zinazochochea vurugu na kutumia nguvu. Amesema hayo Kardinali Leonardo Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki wakati wa Maashimishai ya Siku Kuu ya Mtakatifu Agataha katika Kanisa Kuu la la Catania nchini Italia, wakati mama Kanisa anamkumbuka Mtakatifu Agata mfiadini tarehe 5 Februari.

Kwa kutazama juu ya sura ya Mtakatifu Agata mfiadini chini ya mateso ya wakristo  wakati wa utawala wa  Decio, Kardinali Sandri amekumbuka wanawake wote duniani ambao wamekiukwa hadhi yao na mama wengi wanaolia kwa ajili ya watoto wao, wenye ndoa waliotelekezwa, na wale ambao wananyonywa au wametupiliwa mbali na maisha yao  bila sababu msingi.

Kardinali Sandri aidha amekuunganisha ufiadini wa Mtakatifu Agata na ule wa mateso yanayokumbwa nayo wakristo wengine kwa ajili ya jina la Bwana, katika nchi za karibu na Mashariki kwa namna ya pekee nchini Siria, Iraq, na Burkina Faso . Katika maadhisho hayo pia walikuwapo hata maaskofu wanaotoka katika nchi za Afrika kutokana na kwamba Kanisa la Katania kwa miaka miaka ya hivi wameanzisha shughuli za miradi ya ushirikiano. Hata hivyo amesema “ hatutaki kusahahu ushiriki wa Kristo wa pamoja ambao umezaliwa  kisiwani Sicilia kwa njia ya kupamabania uhutu wa mtu hasa wa kizazi ca vijana na kuwaokomboa kutoka miko ya mitando mibaya sana. Kwa muktadha huo amekumbuka mwenye heri Padre Pino Puglisi.

Kanisa la Roma leo hii anasema linakumbuka miaka 14 tangu kuuwawa kwa Padre Andrea Santoro”. Kadhalika hakusahau kutazama hata Ulaya kwamba leo hii kurudisha kwa thamani za ukristo katika Bara letu kunawezekana  kwa njia ya maisha na ushuhuda aminifu kwa waamini katika sala na katika upendo: katika  uso wa mwingine hata kwa mgeni, inawezekana daima kutambua uso wa Kristo ambaye anajifanya kukutana nasi kila siku.

06 February 2020, 13:38