Tafuta

Vatican News
Katika uwakilishi wa viitabu vya Padre Antoni Spadaro vyenye kichwa "kuwa wa kimeditaranea"wamezungumza Kardinali Pietro Parolin na Waziri Mkuu wa Italia Bwana Giuseppe Conte Katika uwakilishi wa viitabu vya Padre Antoni Spadaro vyenye kichwa "kuwa wa kimeditaranea"wamezungumza Kardinali Pietro Parolin na Waziri Mkuu wa Italia Bwana Giuseppe Conte 

Kard Parolin:uzalendo ni katika kufungamanisha wahamiaji Ulaya!

Kardinali Parolini wakati wa kuwakilishi vitabu vyenye kichwa cha habari: “kuwa wa kimediterania na udugu” vilivyotolewa na “la Civiltà Cattolica” anasema kuwa bado haujajulikana mchango wa wahamiaji katika maendeleo ya nchi walizomo hasa Kaskazini Ulaya. Waziri Mkuu wa Italia Bwana Conte amesema,suluhisho halitokani na utaifa,bali uwajibikaji katika kushirikishana Ulaya nzima.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican katika uwakilishi wa vitabu viwili vya Civilta Cattolica” yaani ‘Ustaarabu Katoliki’ vyenye kichwa cha habari “kuwa wa kimediterania na udugu”, amesema:“Uraia ni ufunguo wa neno kwa ajili ya kukuza mchango wa ufungamanishaji kwa wale ambao wanaingia katika fukwe zetu na kuzuia matukio ya ubaguzi ambayo zaidi ni kama kutengeneza kiota cha kukuza vurugu”. Kardinali amerudi katika mada inayohusu wahamiaji wanaokuja Ulaya na Italia, ambapo akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa Italia Bwana Giuseppe Conte wameweza kutoa hotuba zao juu ya vitabu hivyo viwili vilivyotolewa na  “Civiltà Cattolica”. Bwana Conte Waziri Mkuu wa Italia amesema “suluhisho halitokani na utaifa, bali uwajibikaji wa kushirikishana kwa Ulaya nzima”.

Mwaka mmoja baada ya Hati ya Udugu kibinadamu

Kardinali Parolin amesema mkutano  huo unafanyika katika kufikisha mwaka mmoja mara baada ya Kutiwa sahihi ya Abu Dhabi, kuhusu Hati ya Kihistoria ya Udugu wa Kibinadamu kwa ajili ya amani duniani na kuishi kwa pamoja kwa upande wa Papa Francisko na Sheiki Ahmad al-Tayyib, imam di Al-azhar,tarehe 4 Februari 2019.

Shughuli za wahamiaji hazitambuliki

Katika mijadala ya hivi karibuni, Kardinali Parolin  amebainisha kuwa  hakuonekani au kutambuliwa mchango wa wahamiaji katika maendeleo ya nchi ambazo wanakwenda,  hasa Kaskazini mwa Mediterane. Na  chombo hata kisheria cha kufuata ni kile cha Udugu hata kwa wale mbao wanavuka mipaka na kuingia Ulaya. Kuhusiana na masuala ya wahamiaji, Kardinali Parolin anasema “mbele yetu ulaya hatuna utambuzi na zaidi ule uhai halisi uliopo, huo  hasa unatazama kwa baadhi ya nchi katika Umoja wa Ulaya na ambao wanatishia hata kufungua migawanyiko”.

Kuhusiana na mkutano wa “Kimediterania, mpaka wa amani”

Kadhalika Kardinali amekumbusha katika hotuba yake juu ya mkutano ujao utakaofanyika kuanzia tarehe 19-23 Februari 2020  huko Bari wa maaskofu  wa Italia kuhusu mada ya “Mediteranea, mpaka wa amani na ambapo utahitimishwa na ziara ya Papa Francisko. Meditranea ni mahali pa makutano anasema Kardinali na  wakati huo huo  hata mahali pa migongano kati ya watu na utamadini wa mabara matatu kadhalika na dini kuu tatu zinazoamini Mungu mmoja. Kwa maana hiyo anakazia kwamba “lazima kutoa sauti kwa wale ambao wanatarajia na matumaini kwa watu wote. Hakuna anayebaguliwa. Ni kutafatua mahali ambapo panazaliwa thamani, utamaduni na mawazo licha ya tofauti na pia migogoro.

Kusikiliza vilio vya wakristo , waslam na wayahudi

Kardinali  Parolini kadhalika  ametazama mada na matatizo mengi ya mediterania, yanayotazamwa katika Hati ya udugu wa kibinadamu na kurudia kusema kuwa kile ambacho kimetendwa hadi sasa na wataalam katoliki, kiorthodox,  kiislam na wayahudi ni lazima  kusikilizwa  sauti yao wote.

03 February 2020, 15:43