Tafuta

Vatican News
Kardinali Parolin ameongoza Misa kwa ajili ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio wakati wa kukumbuka  miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo Kardinali Parolin ameongoza Misa kwa ajili ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio wakati wa kukumbuka miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo 

Kard.Parolin:Juhudi za Jumuiya ya Mtakatifu Egidio:chumvi na mwanga!

Katika liturujia ya kushukuru miaka 52 tangu kuanza kwa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio iliyofanyika Jumamosi tarehe 8 Februari 2020 katika Kanisa la Mtakatifu Yohane Laterano,Roma Kardinali Parolin amethibitisha juu ya msimamo wa Jumuiya hiyo katika kupeleka Injili kwa dhati katika maisha ya watu.Amefananisha Jumuiya hiyo kama chumvi na mwanga.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Gazeti la Osservatore Romano, limeandika juu ya Maadhimisho ya miaka 52 tangu kuanza kwa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, ambapo Misa ya shukrani ilifanyika jioni ya tarehe 8 Februari 2020 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano, kwa kuongozwa na Kardinali Pietro Paroli Katibu wa Vatican.  Wanajumuiya ya  Mtakatifu Egidio  ikiwa ni watu wa kila rika, waitaliani pamoja na wahamiaji na wakimbizi wapya wa ulaya na marafiki wengi  walikusanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Yohane ili kuadhimisha maisha ya Jumuiya hiyo. Chumvi na mwanga wa Injili unasambaa katika miji yote kuanzia Roma kwa namna ya pekee chumvi ni ile amani ambayo inasambaa katika nchi nyingi duniani, amethibitisha Kardinali katika mahubiri yake.

Jumuiya ilianza iliwa kijana kabisa kwenda pembezoni na duniani

Katika kuadhimisha Jumapili ya 5 ya kipindi cha mwaka A, Kardinali Parolini amefafanua jitihada za mchakato wa safari ya jumuiya ya Mtakatifu Egidio akiangzwa na Injili na ambayo anasema kama Jumuiya imekuwa chumvi na mwanga wa Injili kwa mataifa.  Wao wakiwa vijana kabisa walianza kwenda pembezoni mwa jamii na kuishi kwa upendo. Hawakusimama tu Roma, bali walitazama hata upnade  mwingine na kuanza  safari kwenye miji mingi ya dunia, wakiwa karibu na wote wenye kuhitaji chumvi na nuru.

Mwanga katika matendo mema

Kardinali hata hivyo amebainisha kwamba  hataki kuzungumzia wanacho fanya bali kuelekeza roho unayowaongoza ile ya upendo mkuu kwa upande wa maskini, waliobaguliwa na kuwa kama jiwe jipya la pembeni. Katika dunia iliyo jaa ubinafsi, migawanyiko na kuta, wakati huo huo chuki zikisambaa katika mishipa ya kijamii, Kardinali anasema jibu lake ziyo upinzani bali , bali la kuangaza tena kwa mara nyingine ule mwanga wa matendo mema ambayo yanabadilisha, yanapindua upweke na kuwa na umoja migogoro  na kuwa na amani, kukata tamaa katika kuwa na matumaini ya wakati mpya endelevu.

Nyumba ya pamoja

Kardinali Parolin aidha amesema Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inahisi na kutamani dunia iweze kuwa nyumba ya pamoja na nchi ya ulimwengu mmoja kwa watu. Kwa kutoa mifani anasema “ hii inajionesha hata katika mapokezi, ufungamanishwaji wa wakimbizi na wahamiaji, kwa wote wanaofika italia kupitia mikondo yao ya kibinadamu.  Jumuiya ambayo ilizaliwa Roma lakini inaishi roma katika ulimwengu. Kwa maana hiyo si katika kufungia na utafia au ubinafsi ambao kwa uhakika anaulinganishja kama tabia za kitoto mbele ya dunia kubwa. Badala yake, Jumuiya ya Roma inageuka kuwa ya uliwengu na kujifungula katika ukweli wa kuzaliwa kwa upya.

Na hii ndiyo Papa Francisko anazidi pia kusisitizia  hivyo Kardinali Paroli anasisitiza kwamba  tusimwache na ahatutaki awe peke yake. Hii ndiyo maana ya kutangaza Injili na kufanya vema kama Yesu alivyo fanya. Ni kushikamana na Yeye”.  Aidha amesema Mtakatifu Egidio anapata tena nafasi yake ambayo Papa anassitiza kwa kusema: “ endeleeni kutembea katika maeneo ya uchungu na pembezoni”.

Salam kutoka kwa Papa Francisko

Kwa kuhitimisha Kardinali Parolin ameshukuru Mwanzilishi wake Andrea Riccardi, na Mwenyekiti wa Sasa Bwana, Marco Impagliazzo. Pia amewza kuwapatia salama kutoka kwa Papa Francisko akiwahimiza kuendeleza na kupeleka matunda ya kiroho, kimshikamano na Amani na kuwakumbusha alivyo wambia akiwa huko Msubiji , “ili kuonesha upendo wa Mungu, daima wakiwa tayari kutoa maisha na matumaini mahali ambao panatawala kifo na mateso” . Kati ya shughuli za Jumuiya ya Mtakatifu Egidio pia amekumbusha kuhusu  Mkataba wa hivi karibuni wa ufunguzi wa majadiliano ya Sudan Kusini.

MAADHIMISHO YA MT.EGIDIO
11 February 2020, 10:21