Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amemteuwa Askofu Giorgio Demetrio Gallaro kuwa katibu mkuu mpya wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki Papa Francisko amemteuwa Askofu Giorgio Demetrio Gallaro kuwa katibu mkuu mpya wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki 

Uteuzi: Askofu George Dmitry Gallaro: Katibu Mkuu Baraza la Kipapa: Makanisa ya Mashariki

Askofu mkuu mteule George Dmitry Gallaro alizaliwa mwaka 1948 huko Pozzallo Sicilia, Kusini mwa Italia. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 27 Mei 1972 Akaamteuwa kuwa Askofu hapo tarehe 31 Machi 2015 na kuwekwa wakfu hapo tarehe 28 Juni 2015. Ilipofika tarehe 25 Februari 2020, akateuliwa kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Makanisa ya Mashariki.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu George Dmitry Gallaro kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule George Dmitry Gallaro alikuwa ni Askofu msimamizi wa waamini kutoka Albania huko Sicilia na mshauri katika Baraza hili. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule George Dmitry Gallaro alizaliwa tarehe 16 Januari 1948 huko Pozzallo Sicilia, Kusini mwa Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 27 Mei 1972 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Baba Mtakatifu Francisko akaamteuwa kuwa Askofu hapo tarehe 31 Machi 2015 na hatimaye, kuwekwa wakfu hapo tarehe 28 Juni 2015. Ilipofika tarehe 25 Februari 2020, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu. Huyu ni kiongozi ambaye amepata uzoefu mkubwa katika masuala ya shughuli za kichungaji katika ngazi mbali mbali za kimataifa. Amewahi kuwa Gambera na baadaye Mlezi wa Mashemasi wa Kudumu. Ni mwandishi mashuhuri wa vitabu vya Sheria, Kanuni na Taratibu za Kanisa. Amebobea katika masuala ya Kanisa la Mashariki na Majadiliano ya Kiekumene.

Katibu Mkuu

 

28 February 2020, 14:53