Tafuta

Vatican News
Mara nyingi Papa Francisko amesema wazee siyo watu wa kubagua bali ni kama warithishaji wa imani,katika mazungumzo na vijana na walinzi wa mizizi ya watu. Ni lazima kuthamanisha uzee wao. Mara nyingi Papa Francisko amesema wazee siyo watu wa kubagua bali ni kama warithishaji wa imani,katika mazungumzo na vijana na walinzi wa mizizi ya watu. Ni lazima kuthamanisha uzee wao. 

Wazee siyo watu wa kubagua ni utajiri wa kuthamanisha!

Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha wameandaa Kongamano la kwanza kimataifa la Uchungaji kuhusu Wazee kwa kuongozwa na mada“utajiri wa miaka”.Wazee siyo watu wa kubagua ni utajiri wa kuthamanisha.Kongamano hilo limeanza tarehe 29-31 Januari 2020 ambalo linaona washiriki 550 kutoka nchi 60 duniani kote.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara nyingi Papa Francisko katika hotuba zake, tangu aanze utume wake kama Papa amekuwa akisisitizia juu ya nafasi muhimu waliyo nayo wazee na kama warithishaji wa imani, katika mazungumzo na vijana  na walinzi wa mizizi ya watu. Papa Francisko amekuwa akisema wazee ni miti ambayo inaendelea kuzaa matunda, huku wakishuhudia kuwa kila kipindi cha maisha ni zawadi ya Mungu, ni ipini cheye uzuri wake na umuhimu wake.

Kufuatia na msisitizo wa Papa Francisko kwa watu hawa ambao kwa maneno mengine wanaitwa kipindi cha umri wa tatu, Baraza la Kipapa la Walei, Familia na maisha wanataka kutoa jibu kwa njia ya Kongamano la Kimataifa la wazee , kwa kuongoza na mada ya “ utajiri wa miaka”. Kuanzia tarehe 29 hadi 31 Januari 2020, karibia wataalam na wahudumu 550 wa kichungaji kutoka nchi 60 duniani wanaungana katika Kituo cha Mikutano “Augustinianum”mjini  Roma kwa ajili ya kutafakari kwa kina kuhusu mantiki tofauti.  Ni kwa mara ya kwanza Baraza la Kipapa hili limeandaa tukio la namna hii , likiwa na lengo la kufanya tafakari ya kichungaji kwenye mada ambayo imewekwa alama ya maisha ya kijamii na Kanisa kwa miongo kadhaa ijayo.

Mada za Kongamano: Kongamano hili limegawanyika katika mantiki tatu: ya kwanza imejikita katika upingano kulingana na utamaduni wa ubaguzi na kujikita kwa kina jinsi gani ya kukabilana, kwa njia tofauti kulingana na muktadha wa kiutamaduni wa jamii, Kanisa linajidhihirisha uso wake ya huruma ikibaki kidete daima karibu na wazee wote. Mada ya pili itaangazia familia na majukumu yao mbele ya mababu na wazee. Na  hawa wameitwa kutambua zawadi ya maisha na imani inayorithishwa kwa kuishi na uongofu wa kichungaji ambao unazingatia kutoa shukrani. Kanisa haliwezi kukubali kuona wazee  wanabaki nyuma na kukosa hali nzuri katika muktadha wa familia na mahali popote walipo, na kwa maana hiyo Kanisa linahisi kuingilia kati ndani ya familia hasa kwa wote ambao wanaishi na upweke. Mada ya tatu inakita juu ya utume wa wazee ndani ya Kanisa. Hata hivyo kuongezeka kwa matarajio ya maisha na uboreshaji kwa jumla katika hali halisi ya afya kumewapa watu wengi msimu mmoja wa maisha marefu zaidi: huru baada ya kumaliza muda wao wa  kazi, lakini wakiwa bado wana afya njema.

Wazee na uinjilishaji: Kongamano kuhusu utajiri wa miaka ya maisha  umewakilishwa Jumanne  28 Januari 2020 katika vyombo vya habari Vatican. Kwa mujibu wa Ripoti ya mwisho ya “World Population Ageing”  ya Umoja wa Mataifa  inabishania kuwa kunako 2019 wazee wenye umri wa miaka 65 na zaidi walikuwa ni milioni 703 . Kwa miongo mitato ijayo, idadi ya watu wazee duniani inatafikia mara mbili hadi zaidi ya bilioni 1,5 mwaka 2050. “Kuongezeka kwa matarajio ya maisha na uboreshaji kwa jumla wa hali ya afya kunatoa fursa mpya na changamoto, pia katika uwanja wa uinjilishaji” kwa mujibu wa Bwana Vittorio Scelzo kutoka  Ofisi ya Huduma ya kichungaji ya Wazee Kwenye Baraza la Kipapa la Walei , Familia na Maisha amesisitiza na kwamba ni maisha marefu ya wazee.

29 January 2020, 15:53