Tafuta

Vatican News
Safari katika maisha ya kitawayanahitaji ujasiri wa kumfuasa yule aliyewaita kwa njia ya huduma hai! Safari katika maisha ya kitawayanahitaji ujasiri wa kumfuasa yule aliyewaita kwa njia ya huduma hai! 

Wanawake wa Kanisa duniania:safari katika maisha ya kitawa!

Katika toleo la wanawake wa Kanisa Duniani litolewalo kila mwezi,kwenye Gazeti la Gazeti la Ossevatore Romano,toleo la tarehe 26 Januari 2020,limejikita katika mada ya Watawa wenye dalili za burnout yaani ugonjwa wa mfadhaiko wa kazi:kujenga jumuiya jasiri.Kardinali João Braz de Aviz anasema baadhi ya mambo ya maisha ya kitawa lazima yabadilishwe.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Miito inapungua, kazi, manyanusa na muda wa kusali kwa watawa lakini pia hata dalili za burnot, yaani dalili za mfadhaiko wa wakazi. Ndizo taarifa zinazoonekana katika Wanawake wa kanisa ulimwenguni , ambapo ni maka ya wanawake kwenye Gazeti la Osservatore Romano ambalo linatolewa tarehe 26 Januari 2020 kwa kujikita katika mada ya Maisha wa Kitawa. Umoja wa Mamama wakuu kimataifa wanazungumza katika gazeti makala hiyo.  Hivi karibunu  Muungano wa Mashirika ya Kitawa ya Mama wakuu kimataifa, walifanya semina ya juu ya matatizo mjini Roma na ili kuwamua namna ya kuunda tume ya miaka ya miaka mitatu mitatu kwa ajili ya  utunzaji wa watu, kwa kesi hiyo watawa ambao wameacha mashirika  kwa ushirikiano wa Muungano huo na Mama wakuu.

Lazima kujenga jumuiya iliyo jasiri: Sr. Maryanne Lounghry, mtawa kutoka Australia na mtaalam wa kisaikolojia na ambaye alikuwapo kutoa mafundisho katika semina hiyo amesema  kuwa “lengo  letu ni kujenga jumuiya ye kijasiri. Sio lazima tujiwekee mipaka ya kuingilia kati ya kesi hiyo kibinafsi, lakini tujifikirie ndani ya mfumo wa kiikolojia. Kutengana kijinsia ni moja wapo  ya fundo ambalo lazima tujiulize kinachotokea katika Kanisa letu na katika nchi ambamo tunatoa huduma”.

Matatizo ya maisha ya kitawa: Kuhusiana na matatizo ya maisha ya kitawa kwa wanawake hasa kuhusiana na upungufu la miito, makonveti yanayofungwa, unyanyasaji wa kijinsia na madaraka ya nguvu katika usimamizi wa mali, uzito wa miundo  ya majengo ambayo wakati mwingine bado yameongozwa kama karne zilizopita Makala  ya Wanawake wa Kanisa inaonesha majibu ya Kardinali João Braz de Aviz, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la mashirika ya Kitawa na Vyama vya Kitume na kusema kuwa “Ulaya inapitia kipindi kigumu sana.  Nyumba nyingi za kitawa zimefungwa na nyingi zimeachwa, japokuwa Maisha ya kitawa yana mzizi wa nguvu sana,  lakini haikubainika mapema kwamba mambo kadhaa ya kitana yanahitaji kubadilishwa kwa sababu wamezeeka. Mafunzo awali ya yote, baadaye usimamizi wa kindugu na mwisho uhusiano kati ya mamlaka na utii.

Kuna haja ya kuwasaidia watawa walioacha mashirika: Bila kusahau uhusiano kati ya mwanaume na mwanamke, ni  kwa sababu waliowekwa wakfu wawe  kike au kiume wanatenganishwa namna hii? Kardinali anazingumza hata namna ya matumizi ya mamlaka ndani ya mashirika.  “tumekuwa na kesi za wakuu wa mshirika  ambao, mara moja baada ya kuchaguliwa, hawajawahi kuacha nafasi zao”. Kardinali anasema kuwa: “ uamuzi wa Papa ni kuunda mjini Roma nyumba ya kuwapokea watu ili kuwatoa barabarani baadhi ya watawa waliofukuzwa na sisi au wakuu wa mashirika kwa namna ya pekee katika kesi ya wageni”.  Na kuhusu kesi ya unyanyasaji kijinsia Papa anaomba uwazi kabisa”.

Makala ya Wanawake wa Kanisa ulimwenguni ni Mchakato wa safari kupitia maisha ya kitawa na ambao tarehe 2 Februari kama ilivyo kila Mwaka ni kuadhimisha Siku ya Watawa dhiniani iliyoanzishwa kunako 1997 na Mtakatifu Yohane Paulo II. Kwa njia ya kuwahoji watawa watatu ambao kama anavyo sema Papa Franciko kuwa   “hawachezi kwenda chini na Mungu, bali wanakabiliana na baadhi ya mantiki ya Maisha ya Kitawa na baadhi ya masuala ambayo yako katika mjadala mkubwa ni ndhiri, utawa wa ndani, na usawa kati ya wanawake na wanaume ndani ya Kanisa. Watawa hao waliohojiwa ni kutoka Paris Ufaransa anazungumza Sr. Anne Lécu, mtawa wa Kidominikani, Daktari  ambaye anafanya kazi katika Gereza lenye usimamizi wa juu cha usalama la Fleury-Mérogis, gerrza kubwa zaidi katika Ulaya; na Roma katika Monasteri ya Wagositiniani wa ndani huko Santi Quattro Coronati, Sr.  Fulvia Sieni na mwenzake Sr. Ilaria; Poland, katika Monasteri ya  Żarnowiec,  Małgorzata Borkowska, ya Kibenediktini ambao baada ya miaka 50 ya maisha ya kitawa amendika Kitabu kiitwacho  “L’asina di Balaam” (bado hakijatafsiriwa kwa lugha ya),  “Wito kwa makuhani.”   

25 January 2020, 10:31