Tafuta

Vatican News
Katika Toleo la 24 la Siku za Kimataifa  kwa ajili ya Mtakatifu Francis wa Sales,Tuzo ya “Padre Jacques Hamel” kwa 2020 ametunukiwa mwandishi Pierre Jovanovic Katika Toleo la 24 la Siku za Kimataifa kwa ajili ya Mtakatifu Francis wa Sales,Tuzo ya “Padre Jacques Hamel” kwa 2020 ametunukiwa mwandishi Pierre Jovanovic 

Tuzo ya “Padre Jacques Hamel” 2020 ametunukiwa mwandishi Jovanovic!

Tuzo ya “Padre Jacques Hamel” kwa 2020, ametunukiwa mwandishi wa habari Pierre Jovanovic katika siku ya 24 ya Kimataifa ya Mtakatifu Francis wa Sales.Ni katika Mkutano uliandaliwa na Shirikiko la Vyombo vya habari katoliki kwa kushirikiana na Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican kuanzia tarehe22-24 Januari 2020 huko Lourdes,Ufaransa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Siku tatu ziitwazao toleo la 24 la Siku za Kimataifa zilizowekwa kwa ajili ya Mtakatifu Francis wa Sales na ambao ni mkutano wa kimataifa umefanyika katika Madhabahu ya Mama Maria wa Lourdes nchini Ufaransa kwa mara ya tatu mfululizo, kuanzia tarehe 22-24 Januari 2020. Mkutano huo umewaunganisha waandishi wa habari Katoliki karibia  mataifa 30 duniani kote. Shirikisho  la vyombo ya habari katoliki ni pamoja na ushirikiano wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican.

Kard.Ouédraogo, Askofu Mkuu wa Ouagadougou amkabidhi tuzo Bwana Jovanovic

Shirikisho la Vyombo vya habari Katoliki tangu mwaka 2017 walitangaza Tuzo ya Padre  “Padre Jacques Hamel”  kwa ajili ya kazi ya uandishi katika huduma ya amani na majadiliano  ya kidini.  Mwaka huu Kardinali Philippe Ouédraogo, Askofu Mkuu wa Ouagadougou, na Mwenyekiti mpya  wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar, amemkabidhi Mwandishi wa habari Pierre Jovanovic kwa ajili ya makala yake kuhusu “Kayla Jean Muller,Mfia mema” lililotangazwa katika gazeti la kila wiki liitwalo: ‘La Vie’ la tarehe  7 Novemba 2019. Hata hivyo Kardinali ameongoza hata misa ya kufunga siku hizi tatu hizo kabla ya kumkabidhi Tuzo mwandishi wa habari.

Tuzo kwa ajili ya huduma ya kutenda  wema "Kayla"

Pamoja na kutekwa nyara huko Iraq kunako 2015 daima alikataa kuacha imani yake ye kikristo. Na kwa maana hiyo kikundi cha kijhadi kilimuua. Katika shambulio la Amerika lililofanywa dhidi ya serikali ya  Kiisilamu mnamo Oktoba 2019 lilileta jina la Kayla Jean Mueller, na hivyo kulipatia heshima kwa msichana huyu wa miaka 26 ambaye hakutaka tamaa ya kuwa na matumaini. Yeye alikuwa ni wa  Kanisa la Kiinjili, Kayla alifanya kazi yake nchini Indiana  Ukingo wa Magharibi katikati ya vijiji vya Palestina, katika nchi za Amerika na wanawake wasio na makazi ... Wakati wa kifungo chake nchini Siria, alionyesha nguvu ya ndani isiyo ya kawaida, ambayo imethibitishwa katika Makala ya Mwandishi Pierre Jovanovic. Makala hiyo imesomwa katika vyombo vya habari Jumanne 22 Janauri na Shirikisho la vyombo vya habari Katoliki (FMC).

Chombo cha kuenzi Padre Jacques kiliundwa 2017

Chombo kilichoundwa kunako 2017 kwa ajili ya kumuenzi Padre Jacques Hamel aliyeuwawa, kinajihusisha katika kutambua kazi ya waandishi katika (makala , kitabu na hati…) ambazo uonesha hatua mbali mbali za shughuli zote zinazohusu  amani na kusaidia mchakato wa majadiliano ya kidini. Kwa maana hiyo tuzo hiyo imetolewa na Kardinali Philippe Ouédraogo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu  Katoliki la Ouagadougou (Burkina Faso) alhamisi 23 Januari 2020 huko Lourdes,katika hafla fupi ya toleo la 24 la Siku za Kimataifa zilizowekwa kwa ajili ya Mtakatifu Francis wa Sales na akiwapo hata Bi Roseline Hamel, dada yake Padre Jacques  aliyeuawa huko Mtakatifu Étienne wa Rouvray kunako  26 Julai 2016.

Vyombo vya habari virudishe imani na  kuwa karibu na watu

Kati ya mambo mengi ambayo yameweza kuzungumzwa katika mada wamebainisha kuwa wakati wa mitandao ya kijamii inaendela na kazi yake “waandishi wa habari wanashutumiwa kwa kufanya kazi zao na kuonewa kiukweli katika uchumi na kijamii, wamesisitiza waandaaji wa Siku ya za Mtakatifu Francis wa Sales. Mgogoro huu unakuza mashtaka ya kupambana na vyombo vya habari vyenye mipango ya watu ambao wanapata faida katika ardhi ya mabara yote. Siku hizi za Kimataifa zimejikita pia kwa namna kutafakari jukumu la vyombo vya habari Katoliki mbele ya matukio haya wakati suala la ukaribu kwa umma ndiyo limepewa uzito sana kwa ajili ya waandishi hao.

Ushiriki wa Kimataifa

Kwa mara nyingine tena Toleo la 24 limekuwa na tabia ya kimataifa na kuhusisha wawakilishi wa Baraza ka Kipapa la Mawasiliano Vatican huko Lourdes kama vile waliowakilishwa ni kutoka:Ujerumani, Burkina Faso, Ufaransa, Italia na Slovenia. Hata wakuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano wametoa hotuba zao katika toleo hili.

24 January 2020, 12:06