Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amekutana mjini Vatican Ijumaa tarehe 24 Januari 2020  na Makamu Rais wa Marekani Bwana Michal Pence Papa Francisko amekutana mjini Vatican Ijumaa tarehe 24 Januari 2020 na Makamu Rais wa Marekani Bwana Michal Pence   (Vatican Media)

Papa Francisko amekutana na Makamu Rais wa Marekani Bwana Mike Pence

Ijumaa tarehe 24 Januari 2020 mjini Vatican, Papa Francisko amekutana na Makamu Rais wa Marekani Bwana Michael Richard Pence

Ijuma tarehe 24 Januari 2020 Papa Francisko amekutana na Makamu Rais wa Marekani, Bwana Michael Richard Pence, mjini Vatican. Wakati wa mkutano wao, Papa amemkabidhi Makamu huyo nakala  ya Ujumbe wa Siku ya Amani Duniani.

Katika Ujumbe wake Papa Francisko anatoa mwakko wa kusaidia kujenga Amani, kukuza haki zaidi ulimwenguni na kuunga mkono ndugu wote kwa sababu leo hii kuna makovu mengi ya vita na matokeo hasa huathiri maskini na wanyonge.

Mara baada ya kukutana na Papa Francisko, Makamu Rais wa Marekani Bwana Pence pia amekutana na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na ushirikano wa chi za Nje wa Vatican.

25 January 2020, 09:33