Kardinali Sandri akiwa na viongozi wa dini wa Ethiopia mara baada ya Ibada ya Misa ya maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Tassisi ya Kipapa ya Kiethiopia tarehe 12 Januari 2020 Kardinali Sandri akiwa na viongozi wa dini wa Ethiopia mara baada ya Ibada ya Misa ya maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Tassisi ya Kipapa ya Kiethiopia tarehe 12 Januari 2020 

Miaka 100 ya Taasisi ya Kipapa ya Kiethiopia:Mchakato wa upatanisho na mageuzi ya liturujia!

Kardinali Leonardo Sandri,Rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki, wakati wa salam zake mwanzoni mwa Mkutano wa Papa Francisiko na ambaye baadaye alimwomba abariki mchakato wa safari ya amani na mapatano kati yao, amebainisha kuwa licha ya Ethiopia na Eritrea kwa bahati mbaya kuishi kwa vita kwa muda mrefu,Makanisa ya nchi hizi pamoja na tofauti zao za kisheria wameendeleza msingi wa umoja

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wakati Ethiopia na Eritrea kwa bahati mbaya waliishi kwa vita kwa muda mrefu, Makanisa ya nchi hizi pamoja na tofauti zao za kisheria, waliendeleza  msingi wa umoja. Ndiyo tamko la Kardinali Leonardo Sandri, Rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki, wakati wa salam zake mwanzoni mwa Mkutano wa Papa Fracinsiko tarehe 11 Janauri 2020 ambapo baadaye alimwomba abariki mchakato wa safari yao ya amani na mapatano kati ya watu.  Hata hivyo ni matarajio yake kwamba mchakato wa mafunzo ya manafunzi hawa utaweza kuwakuza ile hekima ya moyo ambayo ni ya  lazima katika hatua zao za uchungaji wa Kanisa. Aidha ameeleza matumani kwa wale ambao wamepewa majukumu ya kuwa karibu na vijana wengi  wa Ethiopia na Eritrea ili waweze kukua wakitazama wanaheshimiwa ndoto zao kwa ajili ya wema na kwa ajili ya huru wa dini katika mantiki zake zote.

Kusasisha liturujia na mageuzi

Aliyeunganisha Ukleri katoliki katika nchi hizo mbili kwa dhati Kardinali Sandri amebainisha kwamba ni kuhusu tafakari ya baadhi ya mfano wa usasishaji na mageuzi ya kiliturujia kwa pande zote mbili. Na Maaskofu wakuu waliokuwapo hapo katika maadhimisho ya miaka 100 ni mashuhuda. Vile vile baadhi ya mapadre wanafunzi wamrsema kwamba wameweza kuishi katika Taasisi ya Kipapa ya Ethiopia  mjini Vatican  (Pce), wakiwa wote karibu wakisali na kuadhimisha misa pamoja huku wakiomba zawadi ya ile amani ambayo ni zawadi ya Mungu na ambayo kwa hivi karibuni watu wa Mungu wameweza kuipokea. Na kwa maana hiyo Kardinali Sandri ameweza kugusia wanafanzi wengi waliopitia hapo katika Jumuiya ya Wakapuchini ambao wamekabidhiwa Taasisi hiyo miaka ya hivi karibuni kuisimamia.

Sifa kubwa kwa Mapapa waliopenda nchi ya Ethiopia kwa heshima hii

Amewakumbuka watawa wa kike pia ambao wanasindikizwa katika mafunzo hasa katika Taasisi ya Kipapa ya nchi ya Mashariki ya (PIO). Na kwa hitimisho la tafakari hiyo amethibitisha kwamba mapadre wengi waliopitia katika taasisi hiyo  ni wasimamizi wa Makanisa madogo ya Jumuiya nchini Italia na Ulaya kwa ujumla kuwasaidia waamni wengi ambao waliishi kipindi cha majaribu na mateso kutokana na uhamiaji na safari za kupitia baharini. Na wakati wa hitimisho za maadhimisho ya Jubilei ya miaka 100 Tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya kipapa katika kuta za Vatican, Kardinali Sandri akijikita kutazama siku tatu za ambazo wamefanya Mkutano katika Taasisi ya Kipapa ya nchi za Mashariki , kukutana na Papa Francisko, sikukuu ya pamoja  na kwa kuhitimisha na Ibada ya misa Takatifu  ameshukuru Bwana kwa zawadi ya kuwa Watu wa Mungu katika safari ndefu ya historia.

Wapeleke baraka kwa wote watakaokutana nao waliyoipokea kutoka kwa Papa

Akiwagusa wote amebainisha ni kwa jinsi gani wanaishi kwa namna ya pekee ya imani ya Watakatifu waliyoridhishwa kwa kizazi na katika kizazi cha leo nchini  Ethiopia na Eritrea, kinachotajirishwa na muungano unaodumishwa na Kharifa wa Mtume Petro. “Ninyi kwa hakika mpo na utamaduni wa Alessandrino Geez na kwa hakika katoliki! Ninamshukuru Mungu kwa miaka hii 100 ya Taasisi ya Kipapa na kwa ajili ya karne zilizopita ambazo tayari inaoneshwa  kwa upendo mkuu na wafuasi wa mtume Petro kwa ajili ya Kanisa lenu”. Wanafunzi na waamini wote  wanaalikwa kuonesha kwa namna ya pekee ile  nguvu na baraka za Bwana ambayo wameipokea kutoka kwa njia ya Kharifa wa Mtume Petro Papa Francisko , ili waipoleke kwa watu wote watako kutana nao iwe Italia na Ulaya na wale wote wanaoishi nao, wanafanya kazi na zaidi mapadre wanaojikita katik ahuduma mbalimbali za kikuhani, lakini pia wanaweza kuwapelekea  hata katika nchi pendwa ya Eritrea na Ethiopia.

Watu wasikie huruma ya mungu hasa kwa wahitaji

Anawatuma waweze kuwafanya wasikie ile huruma ya Bwana na nguvu yake haswa kwa wahitaji, maskini wa chakula na matumaini, kwa vijana ambao wakati mwingine wanakata tamaa dhidi ya wakati endelevu. Wawafanye nguvu ya amani na mapatano ambayo ni zawadi ya Mungu lakini ambayo inawekewa vizingiti vya aina nyingi na ili kuweza kuonekana kwa nguvu za matendo hai na uamuzi mzuri kwa hao maadui, badala ya kuzuia wema utendeke wa matendo ya hisani na upendo.Mafunzo kama haya kwao ni mchao wa ujenzi wa ustawi wa wote. Wao wawe mashuhuda wa upendo wa Bwana Yesu daima na kila mahali, kama ilivyokuwa mbele ya mauaji ya mfiadini wa kwanza Stefano ambaye ni msimamizi wa Kanisa walimokuwa.

13 January 2020, 12:20