Tafuta

Vatican News
Tarehe 15 Januari 2020 itatolewa toleo la kitabu kinachohusu suala la useja kikuhani kwa mujibu wa  Baba Mtakatifu Mstaafu na Kardinali wa Baraza la Kipapa la Ibada na Sakramenti za Kanisa Tarehe 15 Januari 2020 itatolewa toleo la kitabu kinachohusu suala la useja kikuhani kwa mujibu wa Baba Mtakatifu Mstaafu na Kardinali wa Baraza la Kipapa la Ibada na Sakramenti za Kanisa 

Mchango juu ya suala la useja kikuhani kwa utii wa Papa!

Baba Mtakatifu Mstaafu na Kardinali wa Baraza la Kipapa la Ibada na Sakramenti za Kanisa Katika Kitabu kipya wanakabiliana na mada ambayo Papa Francisko amezungumza mara kadhaa kwamba:"mimi binafsi nafikiri useja ni zawadi kwa ajili ya Kanisa”.

Katika ufafanuzi wa Kitabu kipya kwa mujibu wa Dk. Andrea Tornielli Mkurugenzi wa Uhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican anasema, Kitabu kipya juu ya ukuhani chenye sahini ya Baba Mtakatifu Mstaafu Joseph Ratzinger na Kardinali  Robert Sarah,Rais wa Baraza la Kipapa la Ibada  na Sakramenti za Kanisa  kitatangazwa tarehe 15 Januari nchini Ufaransa. Katika utangulizi uliotolewa na Le Figaro, inaeleweka kuwa waandishi wa kitabu hicho wanaingia na hatua zao katika mjadala juu ya useja na uwezekano wa kuweka  wakfu makuhani waliooa. Ratzinger na Sarah, ambao wanajiita wote wawili maaskofu  katika “utii wa dhati kwa Papa Francisko” na ambao “wanatafuta ukweli” katika “roho ya upendo wa moja wa Kanisa, wanatetea nidhamu ya useja na kutaja sababu ambazo kwa maoni yao wangeshauri kutoibadilisha. Suala la kutokuwa na ndoa yaani useja  linajikita katika kurasa 175 za kitabu zikiwa na  vitabu viwili , kimoja kutoka  kwa Papa na kingine  cha Kardinali, pamoja na utangulizi na hitimisho.

Sarah, katika kitabu chake anakumbusha kuwa kuna uhusiano asili wa kisakramenti kati ya ukuhani na useja. Kudhoofishwa kwa aina yoyote uhusiano huo unaweza kuleta mjadala wa huduma ya Mtaguso na  Mapapa, Paulo VI, Yohane Paulo II na Benedikto XVI. “Ninamsihi Papa Francisko atulinde kwa dhati  kutokana na tukio hili kama ni kutoa uamuzi wowote, unaweza kudhoofisha sheria ya useja wa ukuhani hata ikiwa sababu ina kizingiti kimoja au kingine”. Kadhalika Kardinali Sarah anafikia kufafanua kama kwamba ni “janga la kichungaji na mchangayo wa kidini na giza la ufahamu wa kikuhani” hasa ule uwezekano wa kuwekwa wakfu wanaume walioa.

Benedikto XVI, katika mchango wake mfupi, akitafakari juu ya mada hiyo, anarejea kwenye mizizi ya Ukristo wa Kiyahudi. Anathibitisha kwamba ukuhani na useja tayari vimeunganishwa tangu mwanzo wa “Agano jipya” la Mungu na wanadamu, lililoanzishwa na Yesu. Anakumbuka kuwa tayari katika Kanisa la kizamani, ambalo ni, milenia ya kwanza, “wanaume walioowa wangeweza kupokea sakramenti ya wakfu ikiwa tu walikuwa tayari kuheshimu na kutokufanya tendo la ndoa. Useja wa kikuhani siyo na wala haitakuwa dogma. Hii ni nidhamu ya kiinjili ya Kanisa Katoliki ambayo inawakilisha zawadi yenye thamani, iliyoelezwa kwa njia hii na Mapapa wote wa mwisho. Katika Kanisa Katolike, wenye ibada ya  Nchi za  Mashariki hutoa uwezekano wa kuweka wakfu makuhani walioa na tofauti maalum hizi pia zimeruhusiwa kwa Kanisa la Roma na Benedikto XVI katika Katiba ya Kitume ya kiangilikani “Anglicanorum coetibus” kwa ajili ya waangilikani wanaoomba ushiriki kamili na Kanisa Katoliki, ambapo inaruhusiwa kwa kesi hiyo kukubali  sakramenti ya wakfu wa kikuhani hata kwa wanaume waliooa kulingana na vigezo vya kusudi vilivyoidhinishwa  na makao Makuu Vatican.

USEJA WA KIKUHANI
14 January 2020, 10:20