Majadiliano ni muhimu katika kupata muafaka wa amani Nchi za Mashariki!
Na Sr, Angela Rwezaula- Vatican
Vatican inahakikisha ushirikano wake na Jumuiya ya Kimataifa katika kuendelea kutoa msaada kwa wajili ya kuanzisha kwa mara nyingine tena kutafuta suluhu la mchakato wa majadiliano na jitihaza za amani. Hayo yamesikika katika hotuba yake Monsinyo Fredrik Hansen, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za umoja wa Mataifa akiwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililofanyika kuanzia tarehe 21-22 Januari 2020 jijini New York, kuhusiana na suala la Nchi za Mshariki pamoja na masuala ya kipalestina
Mwongozo wa maneno yake, umekuwa ni kutoka katika hotuba ya hivi karibuni ya Papa Francisko alikukutana na wanadiplomasia kutoka nchi za nje wanao wakilisha nchi zao Vatican, ambapo Papa Francisko alipyaisha tena juu ya wasiwasi wake wa duniani, mahali ambapo mwanzoni mwa mwaka umefunguliwa na habari za wasiwasi wa kivita. Kwa namna ya pekee wa kuongezewa n aule wa tishio kati ya Iran na Marekani na pia ule wa Iraq na Lebanon, na si tu nchi hizo lakini katiia vita ambavyo vimegawanyika vipande vipande katika mabara yote, kuanzia kkaskazini, kwenda kusini, mashariki na magaharibi. Na kwa maana hiyo alisema tunatamani kwa dhati kuzuia hilo”.
Akiongeza umuhimu zaidi Monsinyo Hansen, amesema , hata changamoto hizo lazima zikabiliwe kwa kusilikizwa na kama ilivyo jitihada ya Jumuiya ya kimataifa kuhusu kukabiliana nazo lakini kwa njia ya zana ya majadiliano yaliyo wazi, ya kujenga yanayojikita katika misingi ambayo Umoja wa Mataifa umejisimika kwa miaka 75.
Vatican na Papa, bado bado wanaendelea kwa nguvu zote kudumisha kwa namna ya pekee umakini na Mji Mtakatifu Yerusalemu, anaongeza Monsinyo Hansen, katika wito wake juu ya mji wa amani. Na kwa maana hiyo anasisitizia wito na kurudaia hivyo kama walivyo kwisha rudia mara nyingi hata kwa Shirika hili ili kuweza kutunza, kudumisha hali ya mahali patakatifu Yerusalemu, kwa ajili ya ndugu wapendwa Wayahudi, Wakristo na Waislam na muhimu kwa urithi wa kitamaduni wa familia nzima ya wanadamu
Dharura ambayo Jumuiya nzima ya kimataifa inapaswa ni ile jitihada ya kusaidia mchakato wa amani kati ya Isreli na Palestina ambao tayari ulikuwa imezungumzwa kwa nguvu zote na Papa Francisko katika hotuba zake na wanadiplomasia. Na pia hata katibu mkuu wa mahusiano na Nchi za nje wa Vatican katika ripoti ya Desemba mwaka jana alithbitisha hayto hayo ya dharura ambayo lazima ipatiwe suluhisho la serikali mbili kulingana na miongozo ya mwaka 1967. Kile ambacho Papa alithibitisha hivi karibuni juu ya Israeli na Palestina na kwamba inaweza kutumika kwa mikoa yote.