Tafuta

Kardinali Turkson amesema iwapo hakuna imani,huwezi kuzungumza na hakuna kile ambacho Papa anaita utamaduni wa makutano ni wazi kila yuko katika kona aamawaza ya kwake Kardinali Turkson amesema iwapo hakuna imani,huwezi kuzungumza na hakuna kile ambacho Papa anaita utamaduni wa makutano ni wazi kila yuko katika kona aamawaza ya kwake 

Shinda tamanio la kulipiza kisasi kwani amani ni ushindi dhidi ya vita!

Kwa upande wa kimataifa,baada ya kuuawa kwa Soleimani,Jenerali mkuu wa Iran, watu wanaishi kipindi kinachoongeza hofu kubwa.Katika mahojiano na Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya watu,Kardinali Peter Turkson anasema licha ya yote hayo amani inashinda ishara za vita.Na ni huzuni kusikia bado tukiwa mwanzoni mwa mwaka,unakaribishwa na matukio ya vurugu,mauaji na umwagaji damu

Na Sr. Angela Rwezaula Vatican

Mvutano unaendelea baada ya ushambulizi ulioamriwa  na Rais wa Marekani Bwana Donald Trump na kuuwawa watu wanane, akiwemo Jenerali Qassem Soleimani wa Iran. Hatua za kijeshi zilifanyika karibu usiku wa manane katika eneo la uwanja wa ndege wa Baghdad huko Iraq. Na tarehe 3 Januari 2020 makumi elfu ya watu walishuka katika mitaa ya Teheran, nchini Iran, ili kushiriki katika maandamano makubwa. Kwa mujibu wa mamlaka ya Iran, uvamizi huo ni kitendo cha ugaidi.

Kardinali Tukson amani inashinda ishara za vita: Hata Kanisa linafuatilia kwa wasi wasi mkubwa juu ya hali halisi inayoendelea nchini Iran. Kardinali  Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu katika mahojiano na Vatican News, kufuatia na tukio hilo yeye anashuri  zaidi ya kutokwenda mbali na mchakato wa safari ya amani na ili kushinda vishawishi vya kutoaminiana na hofu. Jukumu la Diplomasia ya Vatican, amesema ni muhimu kwa ajili ya kuhamasisha amani na mapatano kati ya mataifa. Sala anasisitiza Kardinali Turkson ni  kama mzizi wa safari ya amani.

Kardinali  Turkson amesema, mwaka huu umeanza kwa shauku, ari na matumaini makubwa kwa njia ya Ujumbe wa Amani, kwa kutumaini ili kuishi mwaka na amani, na ustawi wa mtu. Kwa hakika ni huzuni kusikia bado tukiwa mwanzoni mwa mwaka, unakaribishwa  na matukio ya vurugu, mauaji na umwagaji damu… Na tunajua kuwa sehemu hizi za nchi za Mashariki ya Kati, hasa katika Iraq, kwa  siku hizi, tunathibitishwa jinis gani wanavyopenda kulipiza kisasi na ishara zote zinazoelezea hali ya mivutano na vita.

Pamoja na hayo yote, Kardinali amesema, tunaalikwa kila wakati  kama ujumbe wa Siku ya Amani ya mwaka huu  unavyosema,   kutambua ukweli kwamba njia ya amani ni ndefu. Hii ndiyo sababu inazungumziwa juu ya njia ya amani, njia inayoungwa mkono na tumaini kwa sababu ya ukweli kwamba Mkuu wa Amani, ambaye ni Yesu, alishuka duniani.  Ni matumaini kuwa kama Yeye alivyoshinda  dhdi ya kifo, tutashinda pia vurugu na  juu ya mizozo hii yote. Hata hivyo Kardinali pia mefafamu juu ya ukosefu wa imani na hofu kama vizingiti vya kuweza  kushindwa. Na hii ni kutokana na kwamba  kimoja kinauhumiza kingine, kwa sababu iwapo hakuna imani, na ikiwa huwezi kuzungumza na ikiwa hakuna kile ambacho Papa anaita utamaduni wa makutano, ni wazi kuwa kila mmoja yuko katika kona yake na kuanza  kutunga mawazo yake ambayo baadaye yanazaa hisia hizi za hofu.

Hata hivyo  Papa Yohane XXIII, wakati wa kipindi cha mivutano kati ya Marekani na Urusi kwa ajili ya kipeo cha Quba, jambo moja lililosaidia kidogo kushinda hali hii ya mivutano ilikuwa ni diplomasia ya kisiasa. Hii iliruhusu kushinda kizingiti cha kutokuwa  na imani kati ya nchi hizi mbili. Kwa njia ya diplomasia ya Vatican,imewezesha kuanzisha imani kidogo, ya  tumaini kidogo, ya urafiki kidogo kati ya mataifa haya mawili na kwa njia hiyo anathibitisha “tumeweza kushinda tishio hili kuu”.

Kutokana na hilo hata leo hii nafasi ya Vatican inayo jukumu kubwa la kuhamasisha imani na urafiki kati ya watu. Ni muhimu kwa sababu kwamba Mungu alikabidhi Kanisa utume mmoja. Utume huo unaunganisha na  si kuhubiri Injili tu, lakini hata kuwa wafuasi na wahudumu wa amani na mapatano kati ya mataifa.  Hivyo ndivyo  alifanya Papa Yohane XXIII, na ndivyo hata leo hii Kanisa linaendelea kujikita katika safari hiyo kwa dhati. Kanisa linaendelea kuwa kisima cha amani kati ya mataifa tofauti. Na tunamshukuru Mungu kutokana na miili kadhaa tuliyo nayo katika Kanisa ambayo  inayotusaidia kueneza ujumbe huu wa amani. Anabainisha Kardinali na kuongeza: “Papa Francisko anakumbusha katika Ujumbe wa Siku ya kuombea Amani duniani 2020 kwamba “Amani ni safari ya matumaini mbele ya vizingiti na majaribu”. Na ili kuanza mchakato wa safari hiyo, hatua moja msingi ya kufanya ni sala…”

Kwa maana ni mzizi na mwanzo wenyewe wa mchakato wa amani, kwani inaeneza tabia hii na fadhila hii ya matumaini, inasaidia isiangukie kamwe mbele ya vizingiti. Katika sala ni kipindi cha kuunganika moja kwa moja na Mfalme wa Amani na ni Bwana mwenyewe anayetuhuisha, anayetuimarisha  na kututia nguvu. Kwa njia hiyo bila kuwa na amani hatuwezi kusonga mbele, amehitimisha Kardinali Peter Turkson.

03 January 2020, 14:51