Tafuta

Kardinali Turkson kwa niaba ya viongozi wengine wa dini katika mkutano wa uchumi huko Davos Uswisi amesema:Ardhi inalia,hata masikini wanalia na hivyo kuna haja ya kufanya mabadiliko! Kardinali Turkson kwa niaba ya viongozi wengine wa dini katika mkutano wa uchumi huko Davos Uswisi amesema:Ardhi inalia,hata masikini wanalia na hivyo kuna haja ya kufanya mabadiliko! 

Kard.Turkson katika Jukwaa la Uchumi:ni lazima kusikiliza kilio cha maskini!

Huko kijiji cha Davos nchini Uswisi mahali ambapo Jukwa la uchumi kimataifa linaendelea hadi 24 Januari,Kardinali Turkson,Patriaki wa kiekumeni Bartolomeo I na Mkuu wa Kiyahudi wa Moscow,Goldschmidt,wameomba serikali za nchi duniani kutumia teknolojia kwa ajili ya ustawi wa pamoja na kwa sababu hakuna sayari ya pili ya kuishi.

Huko kijiji cha Davos nchini Uswisi mahali ambapo Jukwa la uchumi kimataifa linaendelea hadi 24 Januari 2020,Kardinali Turkson, Patriaki wa kiekumeni Bartolomeo I na Mkuu wa Kiyahudi wa Moscow, Goldschmidt, wameomba serikali za nchi duniani kutumia teknolojia kwa ajili ya ustawi wa pamoja na kwa sababu wanasema: "hakuna sayari ya pili ya kuishi".

Ardhi inalia, hata masikini wanalia. Kwa maana hiyo viongozi wa kidini wamekwenda katika kijiji cha Davos nchini Uswisi kuzungumza katika moyo wa matajiri wakuu wa kiuchumi duniani na kutoa chachu ya utambuzi wa dunia iliyopo kwenye mabadiliko. Hayo yamethibtishwa  na Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya watu katika hotuba yake na waandishi wa habari, Jumatano mchana tarehe 22 Januari 2020  katika mantiki ya Jukwaa la Uchumi duniani litakalo hitimishwa  tarehe 24 Januari 2020, akiwa pamoja na Patriaki wa kiekumeni Bartolomeo I na Mkuu wa Kiyahudi wa Moscow Goldschmidt.

Ikiwa kama anavyosema Papa Francisko kwenye Wosia wake wa Kitume wa  Laudato Laudato Si, kwamba ardhi na maskini wanalia ina maa kuwa haja ya dharurua ambayo lazima isikilizwe na lazima wote kutafuta namna ya kutuliza kilio hiki. Amesema Kardinali Turkson, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya watu katika hotuba yake na waandishi wa habari, Jumatano mchana tarehe 22 Januari 2020  katika mantiki ya Jukwaa la Uchumi duniani litakalo hitimishwa  tarehe 24 Januari 2020, akiwa pamoja na Patriaki wa kiekumeni Bartolomeo I na Mkuu wa Kiyahudi wa Moscow Goldschmidt. “Washiriki wote tuliomo kwenye Jukwaa la Uchumi duniani, tupo hapa kwa sababu tutaka uzaliwe kwa upya ule utambuzi wa dunia kwa ajili ya mabadiliko yake” Amesisitiza  Kardinali. Kwa Mujibu wake pia  anasema teknolojia mpya lazima ziwe na msimamo wa kile ambacho “sisi tumeitwa, yaani kwa “kuitumiwa  kwa ajili ya wema wa wote, yaani wema wa ubinadamu na wakazi wake”. Na kwa sababu “hakuna sayari ya pili ya kuweza kuishi amethibitisha Kardinali.

Taadhari aidha amesema, kabla ya kuomba dunia ya kisiasa na serikali za nchi kutambua nafasi msingi ya dini na imani, kwa kuacha mazoea na kuendelea uenezi hasa katika Nchi zilizobobea ulimwengu,  ambapo wanapeana dini kuitumia katika uwanja wao binafsi, na kukana uwepo wao  katika maisha yao siyo jambo zuri

Hata hivyo Rais Donald Trump wa Marekani amewashutumu wanamazingira kama “manabii wa kutabiri mabaya” kwenye hotuba aliyoitoa katika jukwaa la Kiuchumi Duniani, huko Davos ambapo lengo lango la mkutano huo ni Uendelevu. metoa wito wa kutupiliwa mbali kwa utabiri alioufananisha na ufunuo wa Apokalipsi, na kusema Marekani itatetea uchumi. Bwana Trump hakumtaja moja kwa moja mwanaharakati Greta Thunberg, ambaye alikuwa miongoni mwa waliokusanyika. Baadaye akalaumu viongozi wa kisiasa na kusema “iwapo hamkua mnalifahamu, kwa sasa dunia ipo pa bay”". Uharibifu wa mazingira kwa sasa ndiyo ajenda kuu ya mkutano huo unaofanyika kila mwaka ambao mwaka huu uko eneo la kitalii la Swiss ski.

Katika hotuba yake, Bwana Trump amesema kwamba ni wakati wa kuwa na matumaini wala siyo kutazamia mabaya, kwenye hotuba ambayo imesifu mafanikio ya kiuchumi katika utawala wake na sekta ya nishati ya Marekanii ambayo imeimarika. Akizungumzia wanaharakati wa mazingira, amesema: “Wazushi hawa kila wakati hutaka yale yale - nguvu ya kutawala, mabadiliko na kudhibiti kila sehemu ya maisha yetu.”

Hata hivyo nafasi alipewa pia ya Bi.Thunberg  kuzungumza.Baada tu kumaliza kuzungumza, Bi. Thunberg, mwanaharakati wa mazingira wa Sweden mwenye umri wa 17 ambaye amekuwa akiongoza vuguvugu linalotoa wito kwa wanafunzi kuandamana  duniani kote wakitoa wito wa hatua haraka kuchukuliwa dhidi ya uharibifu wa mazingira, kufungua kikao kilichofahamika kama “Kuepuka mazingira ya Apokalipsi”.Alijizuia kumtaja Trump lakini akatoa onyo hili kwa viongozi wa dunia: “Sijui ni sababu gani mtakayotoa kwa watoto wenu kwamba kilikuwa chanzo cha kero za mabadiliko ya tabia nchi ambazo nyinyi mmezileta? ambacho kilionekana kuwa kibaya zaidi kwa uchumi kiasi cha kuamua kuachana na wazo la kuhakikisha mnatengeneza mazingira mazuri ya baadaye?

Akiendelea Greata amesema:“Bado nyumba yetu inaungua. Kutochukua hatua kwenu kunachochea zaidi moto huo kila baada ya saa, na kile tunachowaambia ni kwamba, mchukue hatua zinazoonesha kuwa mnajali watoto wenu.”Ameshutumu wanasiasa na wafanyabiashara kwa kile alichokitaja kuwa ni ni maneno matupu yasiyokuwa na ukomo” Ninye “Mnasema: 'Tutafanya munayotaka. Msiwe watu wa kutazamia mabaya.' Na baada ya hapo, munanyamaza.”

Katika  Mkutano wa 50 wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) unaofanyika katika kijiji cha Davos nchini  unaongozwa na kauli mbiu kwa  mwaka huu ni “ Ulimwengu wenye pande zinazopatana na endelevu”. Mkutano huo unahudhuriwa na idadi ya watu elfu 3 kutoka mataifa 117, miongoni mwa watu hao ni wafanyabiashara, wanasiasa, wanataaluma na wawakilishi kutoka asasi za kiraia. Na zaidi washiriki hauo ni  wawakilishwa na Rais au waziri mkuu wa taifa husika.

 

23 January 2020, 10:07