Vatican News
Jumapili ya Neno La Mungu itaadhimishwa tarehe 26 Januari 2020.Biblia“Sio katekisimu au mtaala wa Taalimungu;sio Neno la Mungu tu,bali ni mazungumzo kati ya Mungu na mwanadamu. Jumapili ya Neno La Mungu itaadhimishwa tarehe 26 Januari 2020.Biblia“Sio katekisimu au mtaala wa Taalimungu;sio Neno la Mungu tu,bali ni mazungumzo kati ya Mungu na mwanadamu. 

Kard.Ravasi:Liturujia na Biblia vinapaswa kurudi mikononi mwa walio rahisi!

Siku chache kabla ya siku ya Jumapili ya Neno La Mungu itakayoadhimishwa tarehe 26 Januari 2020,kwa utashi wa Papa Francisko Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni wa Kardinali Gianfranco Ravasi anatoa utambulisho wa Biblia akisema,Sio katekisimu au mtaala wa Taalimungu;sio tu Neno la Mungu;sio lazima iwe mada ya usomaji wa kiroho,bali ni mazungumzo kati ya Mungu na mwanadamu kwani Mungu anasubiri maneno yetu.Ni Neno la uzima.Ni kitabu cha watu.

Na Padre Richard Kashinje - Vatican

Papa Francisko, kupitia barua yake ya kitume kwa njia ya Motu proprio “Aperuit Illis” iliyotolewa tarehe 30 Septemba 2019, alitoa mwito wa kuadhimisha Jumapili ya Kwanza ya Neno la Mungu ambayo itaadhimishwa tarehe 26 Januari 2020. Kardinali Gianfranco Ravasi, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni anasema kwamba nchini Italia Maandiko Matakatifu yanasahauliwa sana na kwamba Bibilia haipatikani sehemu nyingi. Na katikati ya karne ya 20, Paul Claudel aliweka bayana ukweli kuwa Wakatoliki wanazidi kupunguza heshima kwa Bibilia, wakiiweka mbali na kwa sasa haiongelewi tena sehemu nyingi. Hatua ya Papa ni ya muhimu sana ili kutufanya tugundue tena dhamana, nguvu na umilele wa Maandiko Matakatifu.

Mambo Makuu Matatu ya kufikiria kuhusu Biblia Takatifu

Jambo la kwanza katika tafakari: Kwanza kabisa, hitaji la kurudi kwenye ufahamu wa Maandiko kwa nguvu na kwa na shauku kubwa ambayo ilitokea mara tu baada ya Mtaguso wa Pili wa Vatikano ambao uliyaleta Maandiko Matakatifu karibu sana na waamini. Kupitia siku hii ya Neno la Mungu, Papa anataka kupendekeza kwa mwamini kurudia uhai wa Maandiko, kwani katika mtiririko wa historia, shauku ya maswala ya kijamii yanachukua nafasi kubwa zaidi kuliko kurejea katika Maandiko Matakatifu. Kwa hiyo rai ya Papa Francisko ni kuifanya tena Biblia iwe taa ya kuangaza hatua za mwanadamu. Na siku chache zilizopita, kupitia ujumbe wake wa mafundisho ya dini katoliki mashuleni, Mwenyekiti wa CEI alisisitiza umuhimu wa kujifunza Biblia kutoka katika mtazamo wa kitamaduni.

Jambo la pili katika tafakari: ni kwamba, Bibilia kama mhimili mkubwa wa tamaduni za Magharibi, nyota ya maadili na tabia, ni muhimu kwa mtu yeyote anayeuliza maswali ya maana. Miaka michache iliyopita kulikuwa na msisitizo mwingi juu ya mizizi ya Kikristo ya Ulaya; mada ambayo haisikiki sana leo lakini ambayo haiwezi kupuuzwa kuwa ni ya dini tu bali ni suala la kitamaduni. Umberto Eco alijiuliza:

Katika malezi ya kitamaduni, zote hizi ni za msingi. Lakini kupitia mwito huu wa Papa Francisko Bibilia inahitajika kupendekezwa tena ndani ya mashule kama taswira ya kitambaa cha kitamaduni, kihistoria na kisanii, na zaidi. Ikiwa utaingia kwenye nyumba ya sanaa Ulaya bila kujua Maandiko Matakatifu, una hatari ya kutoelewa kazi nyingi zinazoonyeshwa; lakini ni sawa kwa sanaa zote kwa ujumla, pamoja na muziki.

Jambo la tatu katika tafakari: ni lile la tafsiri ya Biblia japo halijatiliwa mkazo wa kutosha. Ni jambo la msingi sana kwa kuwa dini ya Kiyahudi-Kikristo ni dini ya kihistoria, ya Umwilisho. Mtu anaposema "Neno la Mungu" ukweli unathibitishwa, lakini hiyo haijakamilika kwa sababu Bibilia ni Neno la Mungu na neno la mwanadamu. Kwa maana hiyo ni mazungumzo. Zaburi ni sala, ishara kwamba, kama mwana taalimungu wa Kiprotestanti Dietrich Bonhoeffer anavyoendelea kusema, Bibilia sio tu neno la Mungu linalotulenga lakini pia Neno letu ambalo sisi tunapaswa kulielekeza kwa Mungu.

Tunapofikiria juu ya kiwango cha kitabu cha Ayubu tunabainisha kuwa Bibilia ni hadithi; inachukua hadithi ya mfano ambayo matukio yote ya kibinafsi yamelinganishwa. Mungu, ambaye ameamua kutwaa mwili kupitia historia yetu, anatuasa kujua uwepo wake, uwepo wa hukumu yake na pia kujua kuwa kuna wokovu. Kwa sababu hiyo tunaposoma Biblia lazima kuoanisha Maandiko Matakatifu na Neno mwenyewe ambaye ni Kristo.

Biblia Takatifu ni Nyenzo inayorahisisha mazungumzo ya Ekumene

Wakati Papa akichagua tarehe ya Jumapili ya Neno la Mungu alikuwa amenuia kuiweka siku hiyo ndani ya wakati wa kawaida, sio wakati wa Pasaka au Krismasi. Hii ni kwa sababu kwamba Bibilia lazima iwe mwongozo wa kawaida wa maisha ya watu na siku iliyowekwa wakfu haifai kutengwa, bali inapaswa kuwa ndani ya mwaka wa kiliturujia. Na zaidi ya hayo, katika maadhimisho ya kiliturjia, Ekaristi Takatifu na Maandiko Matakatifu haviwezi kutenganishwa. Hali kadhalika Papa Francisko anaongeza kuwa, Biblia Takatifu ni nyenzo, fundo la dhahabu ambalo linafanya wepesi wa mazungumzo ya pamoja kati ya Waorthodox na Waprotestanti na hasa Wayahudi kwa kusudi moja la kuleta umoja katika Kristo.

Biblia Takatifu ni Kitabu cha watu

Papa Francisko alikazia akisema kwamba Biblia lazima itumike kila siku, lazima kiwe ni kitabu mikononi mwa watu kwa sababu ni kitabu cha watu. Aidha anaongeza kuwa, katika zama za kati ndani ya makanisa makubwa kulichorwa picha na maandishi. Ni wale tu ambao walifahamu kusoma Biblia ndiyo walioweza kufahamu maana yake. Katika siku zetu, tunashuhudia matangazo mengi ya Biblia. Maandishi madogo ya chini pamoja na maoni pia husaidia wasomaji ambao hawana nyenzo japo inahitajika kufanyika kitu zaidi katika ufahamu wa Biblia Takatifu.

Vitu vya kufanyika ili watu waelewe Biblia

Tunapaswa kuelezea sanaa na muziki kwa kuonyesha kanuni ya msingi, lakini pia "kuandika" Bibilia kwa lugha mpya kulingana na sarufi za kitamaduni za leo: sinema, televisheni, sanaa ya video, pamoja na tamaduni za kidijitali. Siku hizi pia ni muhimu kuamsha tafakari juu ya mada kuu za kidini kupitia sanaa, utamaduni, sinema na lugha mpya. Vyote hivyo vinahitaji weledi wa hali ya juu, umahiri na ujasiri.

23 January 2020, 09:57