Tafuta

Vatican News
Papa Francisko ametoa matashi mema na heri ya mwaka mpya alipokutana na wanadiplomasia na wawakilishi wa mashirika mjini Vatican tarehe 9 Januari 2020 Papa Francisko ametoa matashi mema na heri ya mwaka mpya alipokutana na wanadiplomasia na wawakilishi wa mashirika mjini Vatican tarehe 9 Januari 2020  (Vatican Media)

Uhalisia na matumaini!

Kwa mujibu wa Bwana Andrea Tornielli Mkurugenzi mkuu wa uhariri Vatican akifafanua kuhusu hotuba ya Papa Francisko kwa viongozi wa kidiplomasia amebainisha kuwa ufunguo wa hotuba hiyo ni uhalisia na matumaini.

Hotuba ya Papa Francisko imejikita kutazama hali halisi ya dunia kwa mwaka huu na maneno yaliyo wekwa umakini yalikuwa kwa namna ya pekee kuhusu mivutano kati ya Iran na Marekani. Hata hivyo wito huo umejirudia na ambao Papa alikuwa tayari ameshazungumzia juu ya mada hiyo kunako Dominika, tarehe 5 Januari  ambapo aliurudia kutoa wito akiwaalika wazime mapambano, huku wakiwasha moto wa majadiliano, kujithibiti na kuheshimu sheria za kimataifa”. Wito huo ni kwa ajili ya sehemu zote ambazo zipo katika migogoro na ambayo inatafakarisha  hali halisi juu ya hatari inayoikabili nchi za Mashariki na ulimwengu mzima kwa ujumla katika mgogoro wenye kuleta madhara yasiyo hesabika.

Lakini hata kama leo hii kama mwonekano juu ya kile kinachoendelea katika kipeo kati ya Marekani na Iran, na hata hatari kubwa zinazowakilishwa na hayo , bado  kuna hukosefu wa msimamo wa Iraq, inayogandishwa na vita na ugaidi, kwa maana hiyo Papa Francisko haoneshi uwepo wa urahisi wa hali halisi. Anakumbusha hata vita nyingi na vurugu ambazo mara nyingi zimesahurika. Analaani hata ukimya juu ya uharibifu mkubwa wa Siria, kuhusu migogoro ya Yemen, ambayo inaendelea kuishi kipeo kikubwa cha kibinadamu na sintofahamu za Jumuiya ya Kimataifa. Anataja nchini ya Libia, lakini pia vuguru hata nchini Burkina Faso, Mali, Niger na Nigeria. Papa Francisko anakumbusha vurugu dhidi ya watu wasio kuwa na hatia na miongoni mwao, hata wakristo wengi waliouwawa kwa ajili ya kutetea imani yao katika Injili, na waathirika wa kigaidi na itikadi kali.

Katika hotuba yake kwa hakika haiwezekani kubaki bila kuguswa aliyesikiliza au kusoma kwa kirefu orodha ya vipeo hivi , ikiunganishwa na vile vinavyozidi kutoa cheche za moto barani Amerika ya Kusini na ambavyo vimesababaishwa na hukosefu wa haki, ufisadi na rushwa. Tendo la kumfanya Papa aanze na hotuba yake kwa mtazamo wa matumaini ni kutokana na yale matumaini ambayo kwa wakristo ,ndiyo fadhila msingi, lakini pia ambayo haiwezi kuondolea uhalisia jinsi dunia inavyokwenda au ilivyo. Kwa maana hiyo Papa ameeleza inahitaji kupaya majina matatizo hayo na  kwamba inahitaji kuwa na ujasiri wa kukubaliana nayo.

Papa pia hakusahau majanga ya vita ambayo yalifanyika wakati uliopita na kuacha madhara yake makubwa. Bila kusahau upuuzi na vifo vilivyotokana na mbio za silaha za kinyuklia na hatari za dhati za uharibifu wa ulimwengu.  Kadhalika hakusahau pia kutaja  hukosefu wa heshima kwa maisha na hadhi ya  binadamu; hukosefu wa chakula, maji na matibabu kwa watu wengi wanaoteseka, kipeo cha kiekolojia ambacho walio wengi sana wanajifanya vipofu vya kutotazama na kuwa makini.

Licha ya hayo yote, Papa amebainisha kuwa , inawezekana kutumainia  kwa sababu katika dunia hii ambavo utafikiri imehukumiwa kuwa na chuki na kujenga kuta, bado kuna wanawake na wanaume ambao hawakati tamaa na dhidi ya migawanyiko iliyopo  na wala kugeukia sehemu nyingine mbele ya yule anayeteseka.

Inawezakana kutumaini, kwa sababu bado kuna viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ambao wanakutana na kutafuta kujenga dunia ya amani. Inawezekana kutumaini kwa sababu  bado kuna vijana ambao wanatafuta kuhamasisha watu wazima kuhusu  hatari ambayo inaikabili mazingira hadi kufikia hatua ya kutorudia tena katika hali yake. Inawezakana kutumainia kwa sababu katika usiku wa Betlehemu, Mungu Mwenyezi, alichagua kujifanya mtoto, mdogo, madhaifu, mnyenyekevu ili kushinda na kufanya dunia ishinde kwa njia ya upendo wake mkuu sana na huruma yake.

https://nemo.vaticannews.va/editor.html/content/vaticannews/sw/vatican-city/news/2020-01/mabalozi-wampongeza-papa-kuwapa-matumaini-watu-wengi.html

09 January 2020, 13:04