Hii ndiyo ishala ya Picha inayowakilisha Maadhimishao ya Doniminika ya Neno la Mungu.Anaonekana Yesu akiwa ameshikilia Kitabu na wafuasi wawili wakiwa njiani kuelekea kijiji cha Emau. Hii ndiyo ishala ya Picha inayowakilisha Maadhimishao ya Doniminika ya Neno la Mungu.Anaonekana Yesu akiwa ameshikilia Kitabu na wafuasi wawili wakiwa njiani kuelekea kijiji cha Emau. 

Dominika ya Neno la Mungu:Soma Biblia ili imani iwe hai!

Askofu Fisichella amewakilisha mpango wa maandalizi ya Dominika ya Neno la Mungu itakayoadhimishwa tarehe 26 Januari 2020 katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro Vatican.Bada ya Misa Papa Francisko anakabidhi Biblia 40 kwa wawakilishi wa vitengo mbalimbali vya kijamii.Mpango huu unakusudia kukuza ufahamu wa Neno kwa Wakristo wote na inawakilisha hatua ya kina katika

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kutoa mwelekeo katika umoja wa mipango mingi ambayo Kanisa Katoliki ulimwenguni linahamasisha, katika ngazi mahalia, kueneza Neno la Mungu; kutoa msukumo mpya kwa usomaji wa Bibilia katika muktadha wa matendo ya kichungaji; kuanzisha hatua zaidi katika mazungumzo ya kidini; kuwahimiza Wakristo waondoe katika kabati au nyumba zao mambo mengi yasiyo na maana na kuwajali wengine,ni kama zana ya kuamsha kwa upya imani yetu. Haya na mengine mengi ndiyo utajiri mkubwa na maana ya maadhimisho ya Dominika ya Neno la Mungu ambayo itaadhimishwa tarehe 26 Januari 2020 kwa mara ya kwanza, na ambayo imewakilishwa kwa vyombo vya habari na Askofu Rino Fisichela Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Uinjilishaji Mpya Ijumaa tarehe 17 Januari 2020.

Siku iliyoanzishwa na Papa

Katika ufunguzi wa mkutano na wanahabari Askofu Fisichella amekumbusha kuwa Dominika ya Neno la Mungu ilianzishwa kwa matashi ya Papa Francisko na ambaye anawakabidhsi Makanisa yote ili “Jumuiya za Kikristo ziweze kujikita kwa kina kwa kutoa thamani kubwa ambayo Neno la Mungu linaangaza katika maisha ya kila siku ( Rej (Aperuit illis 2). Ikumbukwe tarehe 30 Septemba 2020 katika fursa ya maadhimisho ya maiaka 1600 tangu kifo cha Mtakatifu Girolam, msomi mkuu wa Maandiko Matakatifu na mtafsiri wa vitabi vingi vya lugha ya Kilatino kutoka maandishi asili Na  Papa Francisko Barua ya kitume ya kwa Motu proprio, Aperuit Illis,  ambayo alitoa mwelekezo kuwa itakuwa ni Dominika ya III ya kipindi cha kawaida cha mwaka ambayo aliichagua kuadhimishwa, kutangazwa na kutafakari Neno la Mungu. Katika Barua ya Motu Proprio “Aperuit illis” ya tarehe 30 Septemba Baba Mtakatifu inasisitiza sababu ya kutangaza hati hiyo, ikiwa pia ni kugundua kwa upya maana ya Pasaka na wokovu kwa njia ya Neno la Mungu na ambapo Dominika hiyo ikachaguliwa. (https://www.vaticannews.va/sw/pope/news/2019-09/barua-ya-kitume-ya-baba-mtakatifu-francisko-ya-motu-proprio-ape.html

Mipango mingine ya uinjilishaji

Askofu Fischella amebanisha kuwa katika mwanga wa mipango mingi inayohusu na usomaji na ufahamu wa Biblia uliohamasishwa katika jumuiya nyingi za kikristo  na ambapo Papa alipendelea kujibu maombi mengi yalimfikia kutoka kwa watu wa Mungu na ili Kanisa lito liweze kuadhimisha muungano ikiwa na maana ya Dominika ya Neno la Mungu. Domininka hii ya Neno la Munu ameongeza kusema, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Uinjilishaki mpya ya kuwa inajikta kama mipango ya kichugaji katika nafasi ya Uinjilishaji Mpya kwa lengo la kuuisha na kutoa ari kwa wahusika ambao kwa waamni wanaufahamu wa Maandiko Matakatifu na kuweza kutunza uhai huo kwa nnia ya matendo ya kudumu ya kueneza na uwelewa wake.

Thamani ya kiekumene

Mpango mzima huu hauweze kubaki katika ukimya hata  kwa sababu ya thamani ya Dominika iliyonayo ya kiekueme. Na kwa hakika ndiyo maana Papa Francisko alitaka ifanyika Diminika ya tatu ya Kipindi cha kawaida cha kiliturujia  cha Mwaka ambacho kinaangukia katika Siku ya Majadiliano Kati ya Wyahudi na wakatoliki, na Wiki ya sala ya Kuombea Umoja wa Wakristo. Ndiyo ni wazi, kuwa siyo tukio ambalo ni la muda mfupi, lakini pia  ni chaguo ambalo linalokuzudia kuweka alama zaidi katika majadiliano ya kiekumene kwa kuweka Neno la Mungu moyoni mwa dhamira ambayo Wakristo wameitwa kufanya kila siku .

Alama inayowakilisha Dominika ya Neno la Mungu

Katika mchakato wa kuwakilisha siku hii ya Dominika ya Tatu ya Neno la Mungu kwa waandishi wa habari, Askofu Fischella baadaye amewakilisha alama inayowakilisha kutoka katika tukio la Kibiblia hasa baada ya ufufuko wa Bwana na ambayo inajulikana sana. Na hii ni “ safari ya wafuasi wa Yesu walipokuwa wakitembea katika kijiji cha Emau (Rej  Lc 24,13-35),  ambapo katika safari hiyo kwa ghafla anatokea Yesu Mfufuka katikati yao. Picha inaonesha mantiki nyingi ambazo zinahusiana na Dominika ya Neno la Mungu. Hapa unaweza kutambua awali ya yote watu pamoja na Kristo ambaye mikononi mwake ameshikilia kitabu, yaani Andiko Takatifu linalotimilizaka kwa uwepo wake na wapo mitume wawili, kama unavyoeleza katika Injili ya Luca, kuwa Cleopa na kwa upande wa wachambuzi wanasema mtu wa pili  lbada alikuwa ni mke wake. Nyuso zao zote zinaelekeza kwa Bwana  Yesu Kristo kwa kuthibithisha kuwa ni Yeye ndiye utimilifu wa ahadi ya Agano la kale na Neno jipya ambalo linatakiwa litangazwe duniani kote.

18 January 2020, 11:56